KERO Makanisa kupiga kelele usiku kucha na mchana kutwa Kahama/Lugera

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa kazi wanafanya saa ngapi
 
Huko hakuna misikiti?
 
Sasa kazi wanafanya saa ngapi

Yani hawa jamaa wamerudia tena na maspika yao! Nakumbuka hapo nyuma walikua wanakodi maeneo kama sikosei, wanaweka maspika yao unapigwa mziki kelele tupu eti wanaabudu, kuna siku hizo spika wajanja watapitanazo
 
Mchina kawaboost sana hawa jamaa ,,....wengine town wanatembea na ka spika akifika sehemu anakitua.....ni injili kwenda mbele
 
Naomba kwa ruhusa yako na kwa unyenyekevu mkubwa ikikupendeza nikuite mpumbavu
 
Cha kushangaza unaweza kuta mchungaji yeye anaishi mbali na eneo hilo na analala usingizi mnono ila kawawekea flush halafu ameenda kulala zake huko😁😁😁
 
Makanisa yawe regulated na serikali. Kelele zao zinasumbua sana. Au waende mapolini au jangwani huko. Nonsense kabisa. Mimi ji mkristo kwa ubatizo. Ila upuuzi huo siukubali hata kidogo. Ni kuvunja haki za watu.
 
Serikali itoe tamko mara ngapi wakati sheria zinazodhibiti mambo hayo zipo?

Furaha ama huzuni ya mtu haitakiwi kukera wengine!

Toa taarifa ya kero yako hiyo kwa mtendaji wa mtaa ama kitongoji afuatilie kero yako hiyo kwa hatua zaidi.
 
Uhuru wao wa kuabudu ndio ulete noise pollution
noise polution? Watu wanafanya ibada yao we unaona kelele, unadhani tukianza kusikia vibaya kelele za wanaoabudu miungu yao si itakuwa vurugu na kutokuvumilana? Vipi yale maspika kila mtaa saa saba, kumi kuna ambaye atavumilia makelele hayo? Kwenye kuabudu tuvumiliane isiwe kelele huko
 
Huku kimara na kibamba imekuwa ni too much aisee!!


Baada ya nyumba 2 ya tatu kuna kanisa.
Ni kelele tupu kwa kweli na haijulikani j pili wala siku za kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…