Makanisa Nchini Mjitafakari

Bora Umelitambua hilo Mkuu. Usione Watu wanaanzisha Makanisa Kila Mara. Wameshatambua Siri iliyopo kwenye Makanisa Haya Makubwa.

Yanajilimbikizia Mali sana. Yanaanzisha Miradi mikubwa mikubwa. Vyuo vikubwa.. Makanisa makubwa..Shule.. Mashamba.. mifugo...Viwanja.. Kumbi za Sherehe

Sasa Jiulize Mapato yanamfaidisha Vipi muumini Wa Kawaida. HUTOPATA JIBU. Ukihoji sana Wanakuambia Wanasambaza Injili maana Yake Wanasambaza zaidi Miradi maana Huko wanakosambaza Wakifika Wananunua Maeneo makubwa na Mapori halafu wanafungua Kituo Kidogo au Shule Wana target ya Miaka 100 mbele. Maeneo waliyonunua Yanapanda Thamani mara 1000
 
Ndio machoni pa watu wanaonekana watakatifu ila kwa MUNGU ni wenye dhambi
Hata wewe unaweza Kujiita Tu Mtakatifu. Maana Kamili ya Neno Takatifu ni Kitu Kilichofuliwa Kikatolewa uchafu na Kikawekwa Mahala pake au Mtu kuwa Nadhifu. Ila Si kwamba Neno Mtakatifu lina Maana Hana Dhambi..

Dhambi ni kufanya Jambo ambalo Unajua kuwa ni Dhambi ila Ukafanya Wewe unakuwa Umechuma dhambi. Ila Kufanya Jambo ambalo hujui Kuwa Ni Dhambi unakuwa umefanya Ovu. (Maovu)
 
Et eeeh
 

Nakumbuka kuna siku waliweka maspika nje ya kanisa wakawa na ugeni
Yule mgeni rasmi akapewa mic
akawasalimia na sisi tuko mbali kidogo na mambo yetu
Akasema ni lazima mnunue mashamba kwa jina la kanisa hata ekari 1000 kwa vizazi vijavyo

Hawa jamaa ni matapeli sana kwenye maduka yao walipa kodi wengi ni waumini wao na kila miaka 5 kodi inapanda na ujenzi unajenga wewe na ukarabati juu yako

Biashara inalipa hii

Sasa siku hizi hawahubiri upendo wala kuwaambia hao waumini wasiuwe na wasiibe ila sasa unakuta wauwaji wengi ni wao (rejea matukio ya mauwaji sasa hivi )

Watu kila leo wanawaza sadaka atapeleka nini jumapili hasira anaamua kuuwa tu [emoji23][emoji23]
Watamalizana sana mpaka waje kugundua mchawi yumo humo ni miaka

Mkuu hawa hawaelewi kabisa na wanaona kabisa akienda hospitali zilizojengwa kwa hela zao hapewi hata panadol ya bure akiwa hana hela

Ni mambo ya ajabu sana
 
Mkuu maagizo hayo yalilenga hasa wakati wa agano la kale ili kuwapatia makuhani na walawi mahitaji Yao maana kati ya kabila 12 za Israeli, kabila la Lawi halikugawiwa urithi wa ardhi. Wao alikuwa na jukumu la kuhudumu hekaluni. Katika agano jipya hakuna zaka na hata ukisoma vema historia ya kanisa hapakuwa na zaka katika kanisa la mwanzo. Ikija baadae baada ya kanisa kuanza urafiki na utawala wa Waroma. Kwa Sasa hatuna Tena makuhani wala walawi wala hekalu halipo. Tupo kwenye zama zingine.Ni uchu wa pesa tu unawafanya watu kulazimisha zaka na kwa sababu waumini wengi hawayajui maandiko wala historia vema basi ndio watu watumia mwanya huo kupiga pesa.
 
Nilishawahi kupost hilo andiko miaka ya nyuma watu wiokuwa wanashabikia zaka wakakimbia. Mtu anaambiwa tu toa fungu la kumi leta kanisani wala hajui hata wakati wa agano la kale zaka ilikuwa inatumikaje. Hatuna fungu la kumi kwenye agano jipya.
 
Ukweli siku zote Huja Taratibu na Hudumu Ila Uongo huja Kwa Kasi na Hupotea Kwa Kasi. Sasa Watu washawagundua Kwamba ni waongo

Barakiwa kwa Kutambua Hilo
 
Hata Hayo Maagizo ya Kumbukumbu ya Torati ya Chunguze kwa Makini. Utaona Ni Kwamba Aliyeandika ana Uchu na Mali

Mungu hana Uchu wa Mali maana Yeye Si Binadamu kama Wewe ulivyo na Hata Siku Moja Hawezi kutaka Kitu Kutoka kwako
 
Exactly......🤜
 
Bibilia inasema fungu la kumi itakuwa wewe na familia yako sasa mbona wachungaji wanakula wenyewe.
 
Nimeipenda hiyo

Sent from my Infinix X573 using JamiiForums mobile app
 
kutoa natoa lakini sio kiwango cha kutaka sifa kama wewe
 
Bibilia inasema fungu la kumi itakuwa wewe na familia yako sasa mbona wachungaji wanakula wenyewe.
Ni wakristo wachache mno wanaoijua biblia vema. Asilimia 99 wao ni kusikiliza ikisomwa na mhubiri na kupewa tafsiri atakayo mhubiri kwa maslahi yake. Ujinga huu sijui utatuisha lini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…