Makanisa Nchini Mjitafakari

Hayo pia ni mawazo yako
Sema Wewe Wapi Mungu aliandika Kitabu!? Vitabu vyote Vimeandikwa na Binadamu

Yaani Kitabu ni cha Yohana ila Anayesimulia si Yohana. Kitabu ni cha Matendo ya Mitume ila Anayeyasimulia hayo Si Mitume
 
Unakuta Sa hii kuna mtu kalipa Tsh 30,000 awekewe whatsapp, Tiktok, Instergram na Facebook. Watu wapo hawaishi.
 
We kama unadhani utakatifu ni kuvaasuti basi vaa utakuja kuona
Tafuta maana Ya Utakatifu kwenye Kamusi ya Kiswahili. Mana Yake ndio hiyo Takatifu ni Nguo iliyofuliwa na Kuwa Safi na Kuwekwa Mahala pake kama Vile kabatini. Mtu akiichukua Ile akaivaa na Yeye akiwa ameoga basi Mtu huyo ndie anakuwa Mtakatifu
 
Ni wakristo wachache mno wanaoijua biblia vema. Asilimia 99 wao ni kusikiliza ikisomwa na mhubiri na kupewa tafsiri atakayo mhubiri kwa maslahi yake. Ujinga huu sijui utatuisha lini.
Utaenda Kuisha maana Sasa Hivi Makanisani Si Sehemu ya Kutatua Matatizo Ya Watu imekuwa Sehemu ya Biashara
 
Wewe ndugu Mbona Unang'ania Maisha maisha maisha.. Kwahiyo watu wasijadili Kisa Wana Maisha Magumu kuna Mtu ameweka Akaunti yake Katika hii mada na Maisha anayoishi. Jadili Mada Husika Usi attack Personal issues
Pambaneni na maisha yenu msiliangukie kanisa ni aibu sadaka yenyewe unatoa jero jumapili tu bado unalalamika unaliwa aisee umasikini mbaya sana, hama hamia din nyingine wewe mnatia kinyaa🙄🙄🙄 kwakweli mfumuko wa bei watu watakuwa vichaa kabisaa
 
Hama hamia din nyingine wewe ni nani mbaka uongee hivyo kwanza wewe sio mkristo coz wakristo hawawezi kuongea utumbo kama huu wako, kaangalie sadaka zinatumikaje na kama hujui wakristo wote unaowaona wanatoa michango hujadiliana wafanye nini kama kuna ujenzi au kitu kingine nakushangaa sana😲😲😲 hamia din nyingine itapendeza zaidi kuliko kuongea hapa uonekane mjanja kumbe unachekwa kwa dharau sana😏😏😏 wewe wawapi??
 
Hao mruki wametumwa kuuchafua ukristo..sadaka tangu lini ikamfanya mtu awe masikini..mana unatoa kadri ya uwezo wako na ulivyobarikiwa..hakuna mtu anayekushikia bunduki ili utoe..mana sio lazima.

Huyo ni mamruki tu..wakupuuza.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe mtoa mada hujui kitu kurasa ndeeefu haina hata mstari mmoja kuthibitisha uo uharo wako,Mimi naamini yote ni mawazo yako binafsi kama huna huna hela nenda Sali Rudi kwako.acha umbea eti wasomi wanaongezeka kwani huko chuo kikuu wanafundishwa kuwa makanisa ni wezi!!!,Sadaka ni lazima kwa mkristo soma Biblia.
 
Na mtu akisema hatoi... Atafanywaje... hatoi sasa kaamua..
 
hayo maandishi ya bible ndiyo yanayofanya wajinga wapigwe pesa zao..
 

Mbona Hasira Lete Hoja yako. Ni Lazima Kwako na Familia yako Ili mmpigwe zaidi na Zaidi. Si mnadanganywa Zinaenda Kwa Mungu. Endeleeni kutoa Na Muwajemgee na Wachungaji wenu Nyumba na Magari Mnunue Ambayo yatakuwa Urithi kwa Watoto wao na Si Wewe
 
Na mtu akisema hatoi... Atafanywaje... hatoi sasa kaamua..
1. Utatishwa
2. Utaonekana wa Hovyo
3. Utaambiwa Muumini Usiye Hai
4. Wataenda Mbali Zaidi na Kusema Hawakuziki

Halafu Wanasema Mungu yupo Popote. Bora Ukae Pembeni utafute Mungu wa Kweli umwabudu. Maana Mungu washambadilisha Amekuwa Mtaka Vitu asivyovihitaji
 
Wewe ndio una ufinyu wa Kufikiri. Hivi ushajiuliza Serikali yako inakusanyaje Kodi. Makampuni ya Simu yanakusanyaje Makato hizo Hizo Mia 2 na mia 5 mnazokatatwa ndio zinajenga Nchi

Tuwe na Akili zilizo timamu. Makanisa yashakusanya Kiasi Gani na Kukuwezesha wewe muumini kwa Jambo Lolote la Maana zaidi ya Kuchukua Mifukoni mwa Waumini wake Kila Uchwao

Wewe Utakuwa Unaenda Kanisani Ili Mradi uonekane Umeenda. Na Akili umeziacha Home
 
Mungu hana Dini Usilazimishe "Hama Hama Hama Hama" utadhani huyo Mungu ana Dini zote zimeanzishwa na Binadamu hazina Maana Hata Moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…