carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa wito wa Maombi ya Kitaifa ya Toba, Amani na Ulinzi wa Mungu kwa Taifa, ikiwa tunaelekea kutimiza mwaka mmoja (1) rasmi tangu matukio ya mauaji, umwagaji damu na uvunjifu wa amani yatokee wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29.2025
Taarifa ya CCT iliyotumwa kwa Maaskofu, Viongozi Wakuu na Wakuu wa Makanisa yote Wanachama wa Jumuiya hiyo imebainisha kuwa Kanisa lina wajibu wa msingi kuongoza maombi ya kumuomba Bwana, Mungu wetu Aturehemu na kutusamehe dhambi na makosa yetu kama Taifa na kwa kumwaga damu isiyo na hatia katika Taifa, Awafariji familia zilizopoteza wapendwa wao, awaponye waliojeruhiwa na kuleta uponyaji kwa wote walioathirika lakini pia, Tumuombe Mungu atulinde dhidi ya kurudia matukio kama hayo na atujaalie Amani, Haki, Umoja na Maridhiano ya kweli katika Taifa Ietu la Tanzania
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa CCT Rt. Rev. Dr. Stanley Hotay Oktoba 23.2026 imekumbusha imekumbusha Neno la Mungu linalosema "Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka Mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya Nchi yao" (2 Mambo ya Nyakati 7:14)
Taarifa hiyo imesema, wao kama Kanisa lililoitwa na Mungu katika Taifa la Tanzania linasihi kwa Rehema zake Mungu, Kujinyenyekeza mbele za Mungu, Kuomba, Kufuta uso wake na Kuziacha njia zetu mbaya na Mungu wetu wa Rehema, bila shaka atasikia toka Mbinguni, naye atatusamehe dhambi yetu na kuiponya Nchi yetu ya Tanzania.
Katika hatua nyingine CCT inayojumuisha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa la Menonite, Kanisa la Anglikana, Kanisa la Morovian nk, imetoa wito wa Maombi dhidi ya mvua kubwa kupita kiasi na maafa yanayotabiriwa na Mamlaka za Hali ya Hewa, ambapo imeeleza kuwa taarifa hizo zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) inakumbusha kuomba ulinzi wa Mungu dhidi ya mvua hizo zinazoweza kusababisha mafuriko, uharibifu wa mali, kuharibika kwa mazao na miundombinu, magonjwa na kupoteza maisha...
Chanzo: CCT Instagram page