- Thread starter
- #21
I promise you hakuna elimu itakayosaidia kuwatoa watu kwenye huu utapeli wa kiimani. Ni law enforcement pekee yenye nguvu hiyo. Mamlaka ifanye kama ilivyokataza genital mutilation kwa wanawake.Kwa mujibu wa katiba ya nchi kuna uhuru wa kuabudu, serikali haingilii ibada za raia wake japo kama kunahatarisha amani na usalama wa raia hapo serikali huingilia kati. Hili la abrakadabra za maji na mafuta ya upako na sadaka za ajabuajabu raia watajua wenyewe huko wanakoamini madikodiko hayo. Hata maganga ya kienyeji nayo yanawapiga wananchi wenye shida na matamanio fulani. Cha maana ni elimu tu ndio mkombozi wa kadhia zote hizo