EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Habarini za Leo wapendwa.
Kama kichwa kinavyo someka hapo juu. Ni juu ya makanisa yetu mbalimbali yaliyopo Tanzania.
Sote tunajua jinsi makanisa yetu yanavyo toa mchango katika sekta ya elimu na afya. Kuna shule nyingi sana zinazotoa elimu bora kwa wototo wetu zilizojengwa na makanisa. Lakini pia si hivyo tu kuna vyuo vingine pia vimejengwa na makanisa na hivi navyosema vinaendelea kudahili na kutoa elimu bora kwa watoto wetu.
Katika swala la upande wa afya, nako pia tunaona mchango wa haya makanisa jinsi yalivyo fanya kazi kubwa, fedha zao za michango kanisani zimejenga hospitali ambazo ndugu zetu na Sisi wenyewe tunapata huduma za afya.
Hivyo basi kutokana na mchango muhimu namna hii wa makanisa katika maendeleo ya nchi yetu mimi Nadhani yanaweza pia kuwekeza kwenye kuanzisha baadhi ya viwanda ambavyo havihitaji mitaji mikubwa mfano viwanda vya madawa n.k.
Viongozi wa dini kama mpo humu ndugu zangu tunawategemea sana katika taifa letu maana kazi zenu zinatembea na mkono wa bwana siku zote na ndio maana zinafanikiwa.
Wekezeni pia kwenye viwanda, ili watoto wanaosoma katika vyuo na shule zenu waajiriwe kwenye viwanda hivyo hivyo. Hili swala linawezekana ndugu zangu. Pia watapata nafasi kufanya mazoezi ya vitendo kwenye viwanda vyenu wenyewe.
Tunajua mnaweza, binafsi mimi nimeshiriki sana katika vikao vya wababa kanisani kiukweli huwa tunajiwekea malengo makubwa sana na kwa mkono wa bwana huwa mambo yetu yanafanikiwa.
Tunaona jinsi ambavyo mnaweza kujenga makanisa makubwa ya ghorofa kwa uvumilivu na ustahimilivu wa hali juu bila kuchoka tena kwa muda mrefu kwa moyo mmoja na ushirikiano kwa kutumia nguvu ya kanisa.
Kwakweli Mungu awabariki sana. Amen.