Makanisa yaliyopo Tanzania yakiamua yanaweza kujenga viwanda

Shule,Hospitals na Universities vinatosha.
 
Kweli tumeshindwa kupata watu binafsi au wawekezaji mpaka tunataka makanisa ... tunarudi zama zile za wamissionari ....aaahhhhh ...Kanisani Kazi yake ni kuhubiri na kuleta amani
Tujijemge wenyewe na think tank wetu tutafika mbali
Ndipo tilipofikia mkuu
 
Yesu aliacha agizo kwa kanisa "lihubiri injili, wampokee Yesu na kuokoka " na si kujenga viwanda[ufalme wa dunia hii]
 
Kufilisika kifikra kunaanzia hapa.
 
Mlokole na biashara wapi na wapi???---- wao kazi yao ni kutoa mapepo kwa wanawake tu.
umetendwa na kuja hapa jukwaani kuhara.
Siku mumeo /hawara wako akipagawa na mapepo utawakumbuka hao walokole unaowasema hapa.

Mlokole ni mtu aliyempokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha uake.

Mlokole wito wake ama wito wa wakristo wote ni "kuwafanya mataifa/gentiles kumwanini Yesu " maana wameagizewa kujenga ufalme wa mbinguninambao ni wa kudumu tofauti na huu wa dunia wenye mwisho
 
Umenena kweli, hasa kwa madhehebu ya tuliokoka (walokole)!
 


Swali langu moja kwako ni hili: je wewe umeokoka??
 
Kiwanda siyo kusudi kuu la kanisa
 
Kiwanda siyo kusudi kuu la kanisa
Umewai kwenda kanisani mkuu? Umewahi kuhudhuria vikao vyovyote vya wababa au wamama au vijana, umewahi kusikiliza mikakati ya kanisa ili kuwaongezea kipato waumini wake waendelee kutoa sadaka makanisani na kuwa na maisha bora?
 
Umewai kwenda kanisani mkuu? Umewahi kuhudhuria vikao vyovyote vya wababa au wamama au vijana, umewahi kusikiliza mikakati ya kanisa ili kuwaongezea kipato waumini wake waendelee kutoa sadaka makanisani na kuwa na maisha bora?
Kabisa mkuu,mimi ni mdau mkubwa ila kusudi kuu la kanisa siyo kiwanda
 
Mleta mada ulichoandika ndo kazi za dini zilizopaswa kufanya tangu mwanzo hata ajira za ualimu na matibabu ni kazi za wito zilipaswa kufanywa kiupendo na siyo Kama ajira, tatizo linakuja kwa watunga Sheria wanawaogopa hao watu waliotakiwa kuwasimamia, kwasasa dini inatakiwa itofautishwe na wafundishaji wa kuvuta waumini yaani wale NGO ndo waitwe dini wafungue shule, hospital, na kufungisha ndoa, na maziko kwa msamaha wa serikali hivyo watu watachangia Kama sadaka kupata huduma hizo, tuje kwenye mafundisho wao wapewe kazi ya kufundisha neno la Mungu kwa malipo Kama mishahara ya mwisho wa mwezi kwa kuchangiwa Kama Ada, yaani kusema ukweli sadaka zingejenga huduma nyingi za jamii tofauti na Sasa.
 
Na ndo maana kwenye mashule Kuna somo la dini kulingana na walioanzisha na mahopital muda wa ibada kuombea wagonjwa kulingana na walioanzisha.
 
Akili ya mtanzania imewekeza kujenga misikiti na makanisa kushne!.Kama mkoloni angewafundisha kujenga viwanda basi Leo tungekuwa na vya kutosha.
Makanisa makubwa misikiti mikubwaa tazama shule za serikali/wananchi zinazozunguka makanisa na misikiti nu magofu!! Waafrika tunatia aibu sana, kuchangia darasa hadi mkuu wa mkoa akukamate ili hali anasoma mwanao.
Sehemu ambayo unaenda masaa mawili kwa wiki ina Maru Maru lakini sehemu ambayo mtoto anafanyia makuzi yake siku nzima ni ya hovyo kweli kweli.
Wake up black man!!!
 
Kwani ni ajabu makanisa kuwekeza wakuu, mbona mataifa yote yamejengwa na nguvu ya kanisa, tawala zenyewe zimeanzia kanisani. Chanzo cha mataifa yote si ni kanisa au.
Hiko unachokiwaza unazani makanisa hawajawahi kuwaza mkuu? Wao wamejispecialise katika kutoa huduma za kijamii (Upendo katika kumhidumia) kama mashule na hospitals kwa muda wa Karne na karne. Hata biblia imeandika dini ya kweli ni kuwajulia mayatima na wajane katika dhiki zao.
Upande wa kuboresha vipato vya watu kwa kuwapatia ajira labda waanze baada ya kukusikia wewe, Ila jua kuwa walishawazaga hilo tangia Karne ya 18 huko Uingereza kipindi cha industrial Revolution na bado hawakufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…