Kufuatia kuendelea kwa vita katika Mashariki ya Kati, kumekuwepo na kusambaa kwa taarifa mbalimbali mitandaoni. Mojawapo ya taarifa hizo ni chapisho lililosambazwa kupitia mtandao wa Facebook, likidai kuwa makao makuu ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad, yaliyopo Tel Aviv yameharibiwa vibaya na makombora ya Iran usiku wa kuamkia leo.
Chapisho hilo lilionekana katika kikundi cha Facebook kinachojulikana kama jafalovestory, likiwa na ujumbe unaodai kuwa kulikuwa na mfululizo wa mashambulizi nchini Israel, na kwamba shambulio kubwa zaidi lililenga eneo la katikati ya jiji la Tel Aviv, hususan katika mifumo nyeti ya ulinzi wa anga ya Iron Dome na David's Sling.
Hata hivyo, kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words search), imebainika kuwa hakuna taarifa rasmi kutoka vyombo vya habari vinavyoaminika au mamlaka husika zinazothibitisha kuwa makao makuu ya Mossad yameshambuliwa au kuharibiwa.
Aidha, uchunguzi umebaini kuwa taarifa hiyo imechukuliwa nje ya muktadha na kuhusishwa kimakosa na matukio ya sasa. Chanzo chake ni habari iliyochapishwa tarehe 15 Juni 2025 na
Anadolu Agency,
Katika taarifa hiyo, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC) kilidai kuwa kilifanya mashambulizi yaliyolenga vituo vya ujasusi vya Israel, ikiwemo idara ya ujasusi wa kijeshi (Aman) na Mossad. Hata hivyo, madai hayo yalikuwa ni kauli ya upande mmoja wa kijeshi na hayakuthibitishwa na ushahidi huru au vyanzo vya kuaminika kimataifa.
Hivyo taarifa hiyo ni potoshi kwa kuhusisha matukio ya zamani ambayo yameanza kutokea miak ya nyuma na kile ambacho kinaendelea katika vuta nikuvute inayoendelea mashariki ya kati