Makapuku Forum

Makapuku Forum

KIUNGO wa Simba, Mzambia Clatous Chama, amemtaka kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone, ahakikishe anampa pasi za mwisho 10 kwa ajili ya kufunga mabao katika msimu huu mpya ulioanza Agosti 15, mwaka huu.

Chama ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar ka-tika mchezo wake wa juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex ul-ioko Turiani, Morogoro.

Katika ushindi wa mchezo huo, Chama alifunga bao la nne baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Miquissone ambaye amerejea tena katika timu hiyo akitokea Al Ahly ya Misri. Chama alisema anaimani kubwa atafanya vyema na vizuri msimu huu kwa kufunga mabao kutokana na muunganyiko mzuri wa wachezaji wenzake hasa Miquissone ambaye aliwahi kucheza naye miaka ya nyuma.Chama alisema anafurahi Simba kupata ushindi wa mabao 4-2, huku yeye pia akifunga katika ushindi huo wa kwanza msimu huu.

[emoji860]“Nimefurahi kupata pasi ya mwisho na kufunga kutoka kwa Miquissone (Luis), ila nataka assist 10 kutoka kwa nyota huyo katika michezo iliyopo mbele yetu,” alisema kiungo huyo.Aliongeza kwa ubora wa kikosi chao, anaimani wanatarajia watafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita na hiyo inatokana na maboresho yaliyofanyika kwa kusajili wachezaji wapya ambao wamekuja kusaidia kufikia malengo ya kutwaa mataji mbalimbali yaliyopo mbele yao.
Screenshot_20230819_153102_Instagram.jpg
 
[emoji599] OLEKSANDR Zinchenko ametuliza presha kwenye kambi ya Arsenal baada ya kurejea uwanjani na atakuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho Jumatatu dhidi ya Crystal Palace utakaopigwa Selhurst Park.
.
Beki huyo wa kushoto kutoka Ukraine alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kigimbi tangu mwishoni mwa msimu uliopita, lakini siku mbili zilizopita alirejea mazoezini na kufanya vizuri.
.
Zinchenko, 26, sasa atampa Kocha Mikel Arteta uhakika wa kumtumia kwenye nafasi hiyo baada ya miamba hiyo ya Emir-ates kumpoteza staa wake mpya, Jurrien Timber, aliyeumia goti kwenye mechi ya kwanza ya ligi msimu huu.

Screenshot_20230820_075912_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji mpya wa Inter Miami Leo Messi ameshinda tuzo mbili kwenye kombe la ligi lililomalizika asubuhi ya leo .

Messi ameshinda tuzo ya mfungaji bora akimaliza na mabao 10 lakini pia mchezaji bora hii ni baada ya kuwa Mchezaji bora kwenye mechi tano alizocheza akiwa na timu hiyo .
Screenshot_20230820_083218_Instagram.jpg
 
Wadau wa elimu wameendelea kusisitiza umuhimu wa kodi kuondolewa katika bidhaa ya pedi ili kuwezesha Wasichana kufikia haki ya elimu huku pia wakishauri Serikali kugawa pedi bure kwa Wasichana wenye uhitaji zaidi (Wanaotoka kwenye mazingira magumu).

Wadau hao wameongea hayo wakati wa mkutano uliohusisha Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikai na mitandao mbalimbali ya kitaifa ya hedhi salama na elimu kwa Mtoto wa kike ili kujadili mifumo wezeshi kwa Wasichana kufikia haki ya elimu.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeibaini kuwa, asilimia 60 ya Wasichana wameonekana kutomudu gharama za taulo za kike na hivyo kujikuta wanatumia vifaa ambavyo si salama wakati wa hedhi na kupelekea changamoto katika afya ya uzazi, maambukizi katika mfumo wa mkojo mfano fangasi au kushindwa kuendelea na shughuli zao hivyo kuwarudisha nyuma kielimu au kimaendeleo.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2018 Serikali ilitoa kodi inayotozwa kwenye pedi, lakini ikairudisha mwaka 2019 kwa kile kilichoonekana kuwa bei haikushuka kama ilivyotarajiwa jambo ambalo Wadau wa elimu wanaamini lilihitaji muda na mikakati mingine ya ufuatiliaji kwa Wafanyabiashara ili kuleta tija kwa Watoto wa kike, pia June 18, 2023 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alinukuliwa akionesha Serikali kusikia kilio cha Wadau kuhusu kodi katika taulo za kike.

Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi Msichana Initiative amesema “Kumtoza Mwanamke/ Msichana kodi kwa kupata hedhi si sawa, hedhi ni suala la kimaendeleo, kibinadamu na kiuzazi kwenye jamii”
Screenshot_20230820_084044_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(Latra), imefungua milango Kwa wasafirishaji kuanza kupeleka maombi ili yachakatwe kwa ajili ya maandalizi na kujipanga kuanza kutoa huduma kwa saa 24.

Milango hiyo imefunguliwa zikiwa zimepita siku chache tangu Serikali kutangaza kuondoa rasmi katazo la mabasi kusafiri usiku.

Juni 28, mwaka mwaka huu wakati akitoa hoja ya kuahirisha vikao vya Bunge, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza rasmi kuondoa zuio la safari za usiku lililokuwepo tangu Mwaka 1992.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabarani kutoka Mamlaka hiyo, Johansen Kahatano imeeleza kuwa, baada ya kupokea maombi hayo hatua itakayofuata ni kuyachakata, ili kujua ukubwa wa maeneo yenye uhitaji na kupanga ratiba za kuanza huduma hiyo.

"Tunatarajia huduma hii haitachelewa sana kuanza kwa sababu uhitaji wa kutoa huduma hiyo saa 24 upo na Wizara zote mbili za Mambo ya Ndani na Uchukuzi kukaa pamoja," amesema Kahatano.

Amebainisha kuwa kama ambavyo walianza huduma ya usafirishaji saa 11 alfajiri na baadae saa tisa, ndivyo watakavyochakata na kupanga ratiba hiyo ya saa 24, na njia gani zianze kutokana na ukubwa wa uhitaji.
Screenshot_20230820_084323_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom