Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230823_063023_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230823_063045_Opera%20Mini.jpg
 
BAYERN Munich na Liverpool zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester City, Kalvin Phillips, 27, dirisha hili. Phillips amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man City tangu aliposajiliwa dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Leeds United.
.
Mapema kwenye dirisha hili aliweka wazi mpango wake ni kuendelea kusalia Man City na kupambania nafasi kwenye kikosi cha kwanza ingawa uwezekano unazidi kuwa mdogo siku hadi siku. Munich inataka kumsajili staa huyu kutokana na msukumo mkubwa kutoka kwa kocha wao Thomas Tuchel anayedaiwa alihitaji huduma yake tangu alipokuwa anaifundisha Chelsea.
.
Liverpool yenyewe inamhitaji ili kuboresha eneo lao la kiungo na mara kadhaa ilijaribu kuwasajili Moises Caicedo na Romeo Lavia lakini wakazidiwa kete na Chelsea.
Phillips ambaye hajacheza hata mechi moja tangu kuanza kwa msimu huu.
Screenshot_20230823_064331_Instagram.jpg
 
[emoji599] BRUNO Gomez, ni mingoni mwa wachezaji ambao wapenzi wa Yanga walitamani kumuona kikosini mwao msimu huu, chanzo changu ndani ya Singida FG, kimefunguka kuwa pamoja na watu wa Yanga kumtamani Bruno, lakini Mbrazil huyo hakubaliki na uongozi wa juu pamoja na makocha wao.
.
“Kuna viongozi wa juu kabisa Yanga hawamkubali Bruno. Wanasema bado anahitaji muda zaidi wa kukomaa kumudu kucheza Yanga japo wanaukubali uwezo wake. Nadhani hata makocha (wa Yanga), hawamkubali sana ndio maana hukuona nguvu ikiwekwa kumsajili,”
.
Kocha wa Singida, Hans van der Pluijm alipoulizwa iwapo kiungo huyo ana nafasi katika kikosi cha Yanga, alisema: “Bruno ni mchezaji mzuri, ila bado anahitaji kukua zaidi kuweza kuhimili kucheza Yanga. Kuchezea Yanga au Simba si kitu kidogo, kule unahitaji uwe umekomaa hasa kuweza kukabiliana na presha za mchezo na mashabiki. “Kule Yanga anaweza kukosea mara moja, mara mbili, mara tatu... mashabiki wakamzomea na kumtoa kabisa mchezoni, hivyo anatakiwa kubaki hapa (Singida) ili aendelee kukomaa zaidi.
Screenshot_20230823_064444_Instagram.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema shughuli za kununua fedha za kigeni nchini zinatakiwa kufanyika na Taasisi za fedha zilizoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania pekee hivyo Mtu au Taasisi (isiyoidhinishwa) kununua au kuuza fedha za kigeni ni kinyume cha sheria.

“Shughuli za kununua au kuuza fedha za kigeni nchini zinatakiwa kufanyika na Taasisi za fedha zilizoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania pekee ili kukabiliana na biashara haramu ya fedha za kigeni ikiwemo soko lisilo rasmi (black market or parallel foreign exchange market), hivyo Mtu au Taasisi inayofanya biashara ya kuza au kununua fedha za kigeni ni kinyume cha sheria”

“Benki Kuu pia inatoa wito kwa Wananchi kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa Nchini ili kupunguza mahitaii ya fedha za kigeni, kuimarisha shughuli za uchumi na kuongeza kipato kwa Wananchi.”

“Vilevile Benki Kuu inatoa wito kwa Wazalishaji nchini kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa na huduma zinazozalishwa, hatua hii itapunguza uhitaji wa kuagiza bidhaa au huduma kutoka nje na kuongeza mapato ya fedha za kigeni” imeeleza taarifa ya BOT leo kuhusu sakata la kupotea kwa dola.
Screenshot_20230823_064640_Instagram.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema uchumi wa Tanzania unaendelea kumarika na kuna viashiria vya kupungua kwa changamoto za upungufu wa fedha za kigeni Nchini.

“Mwenendo wa uchumi wa Tanzania umekuwa wa kuridhisha ambapo ukuaji wa uchumi ulifikia asilimia 4.7 mwaka 2022 na asilimia 5.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, mfumuko wa bei umeendelea kupungua kufikia asilimia 3.3 mwezi Julai 2023 ukilinganisha na asilimia 4.9 mwezi Desemba 2022”

“Urari wa malipo ya huduma na bidhaa nje ya Nchi ulipungua kufikia asilimia 6.3 ya pato la Taifa ukilinganisha na aslimia 7.3 ya pato la Taifa kwa mwaka unaoishia December 2022, vilevile mwenendo wa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani umekuwa wa kuridhisha kuanzia mwanzoni mwa mwezi Agosti 2023 baada ya Benki Kuu kuchukua hatua mbalimbali na kuanza kwa msimu wa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya Nchi na utalii”

"Mwenendo huu umedhihirika katika soko la rejareja la fedha za kigeni, ambapo kiwango cha kubadilisha shilingi kwa dola ya Marekani umepungua kufikia shilingi 2,550 kwa dola ya Marekani Kutoka shilingi 2,610 mwezi Juni na Julai 2023 ambapo mwenendo huu wa kuridhisha unatarajia kupunguza changamoto ya upungutu wa dola ya Marekani nchini, hali hii pia inajidhihirisha katika kuimarika kwa nakisi ya urari wa malipo na huduma nje ya Nchi (current account deficit)“ ——— imeeleza taarifa ya BOT.
Screenshot_20230823_064732_Instagram.jpg
 
Serikali ya Tanzania pamoja na Benki Kuu zimesema zinaendelea kutekeleza hatua mbalimbali kukabiliana na upungufu wa fedha za kigeni nchini ikiwemo hatua ya kuongeza kiwango cha kuuza fedha za kigeni katika soko la fedha za kigeni, kuongeza vyanzo vya upatikanaji wa fedha za kigeni ikiwemo ununuzi wa dhahabu.

Taarifa iliyotolewa leo kwa Waandishi wa Habari imesema hatua hizo ni pamoja pia na mikakati ya kuongeza mauzo Nchi za nje na kuzalisha bidhaa mbadala wa zile zinazoagizwa nje ya Nchi.

Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi kutoka Benki Kuu Dr. Suleiman Missango amesema Benki Kuu inaendelea kushirikisha Mabenki, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na Wadau wengine katika kusimamia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya fedha za kigeni nchini.

“Hatua hizo zimeanza kuleta mafanikio ikiwemo kupunguza kasi ya mabadiliko katika thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani katika soko la rejareja, vilevile kiasi cha LCs kilichokuwa hakijalipiwa na kubadlishwa kuwa mikopo (post-import loans) kimeendelea kupungua” ——— Dr. Missango.
Screenshot_20230823_064836_Instagram.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema pamoja na kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa fedha za kigeni nchini hususan dola ya Marekani, Nchi ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni na hali ya upatikanaji wa fedha za kigeni imeendelea kuwa himilivu.

“Uhimilivu huo unatokana na kuendelea kuwepo kwa akiba ya kutosha ya fedha za kigeni nchini, ambapo hadi kufikia tarehe 21 Agosti 2023, akiba hiyo ilikuwa dola za Marekani milioni 5,441, ambayo inatosheleza miezi 4.9 ya uagizali wa bidhaa na huduma kuloka nje”

“Kiasi hiki kinalingana na kipindi kabla ya changamoto za uchumi wa dunia zilizopelekea kuwepo kwa upungufu wa fedha za kigeni nchini, Benki Kuu inatarajia kuendelea kutumia akiba hiyo kuongeza ukwasi katika soko la fedha za kigeni nchini”

“Kuanzia mwezi Julai hadi tarehe 21 Agosti 2023, Benki Kuu imeuza katika soko la fedha za kigeni dola milioni 100.5 ikilinganishwa na dola milioni 62 katika kipindi cha Julai-Septemba 2022, pia tokea kuanza kwa vita ya Ukraine mwezi Machi 2022, Benki Kuu imekwisha uza katika soko la fedha za kigeni dola milioni 518.5”
Screenshot_20230823_064924_Instagram.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekiri uwepo wa upungufu wa fedha za kigeni hususani dola ya Marekani katika Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kunakochangiwa na uchumi kukabiliwa na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine, covid-19, mabadiliko ya tabia Nchi na mabadiliko ya mwelekeo wa sera ya fedha katika kubaliana na ongezeko la mfumuko wa bei duniani.

“Athari za vita kati ya Urusi na Ukraine (na vikwazo kwa nchi ya Urusi) zilisababisha kuvurugika kwa mnyororo wa ugavi wa bidhaa na upungufu wa bidhaa duniani, hali hii ilipelekea kupanda kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hivyo mahitaji ya fedha za kigeni ya kununua bidhaa kutoka nje yaliongezeka hapa nchini na kuwepo kwa upungufu wa fedha za kigeni, hususani dola ya Marekani.

“Baada ya janga la Covid 19 kuisha, biashara na wekezaii duniani uliongezeka hali hii ilisababisha ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni katika Nchi nyingi, ikiwemo Tanzania, hivyo kupelekea kuwepo kwa upungufu wa dola ya Marekani”

“Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, hali hii inasababisha mafuriko, ukame na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi mbalimbali, hivyo kumekuwepo na ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni katika Nchi nyingi kukabiliana na hali hiyo, ikiwemo kujenga au kukarabati miundombinu” —— imeeleza taarifa ya BoT.
Screenshot_20230823_065025_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu nchini Thailand imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa Nchi hiyo Thaksin Shinawatra adhabu ya kifungo cha miaka nane jela.

@DW_Kiswahili imeripoti kuwa Shinawatra alikamtwa saa chache aliporejea nchini humo baada ya kuwa nje kwa muda wa miaka 15 ambapo adhabu aliyopewa inahusiana na hukumu zilizotolewa dhidi yake wakati alipokuwa nje ya Nchi.

Makosa yanayomkabili ni pamoja na matumizi mabaya ya mamlaka, kuiagiza benki inayoendeshwa na Serikali kutoa mkopo kwa Mteja wa nje kinyume cha sheria na pia kumiliki hisa kinyume cha sheria kwa kuwatumia Mawakala binafsi.
Screenshot_20230823_065118_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Comrade Kheri James @comradekheri ameupokea ujumbe wa Taasisi ya Viva con Agua na ENVISOL kutoka Chuo cha Nelson Mandela Arusha ambazo zimekusudia kupeleka huduma ya maji katika Shule tatu za Wilaya ya Mbulu, kupitia mradi wake wa uvunaji wa ukungu.

Akiongea na DC wa Mbulu pamoja na Wataalamu wa Mamlaka za Maji katika Wilaya ya Mbulu, Kiongozi na Mratibu wa Mradi huo Profesa Karoli Njau, amesema Wilaya ya Mbulu ni miongoni mwa Wilaya zenye utajiri mkubwa wa ukungu hivyo wameona ni vizuri na busara kutumia ukungu huo kama fursa ya kupunguza tatizo la maji katika maeneo ya huduma yalio mbali na huduma ya maji lakini yenye utajiri wa ukungu.

Mradi huu hauna masharti yoyote kwa Shule zitakazonufaika, isipokuwa kigezo kikuu ni Shule hiyo iwe eneo lenye ukungu wa kutosha na ambalo halina huduma kabisa ya maji, mradi utaanza mapema mwezi ujao na utaanza kwa kuwajengea uwezo na uelewa Viongozi na Watumishi wa maeneo yote yatakayonufaika na mradi huo.

Shule zitakazo mnufaika na mradi huo ambao utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa Matumizi ya kibinaadamu na kitaaluma ni Shule ya Sekondari Nambis na Shule ya Msingi Haysali zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, na Shule ya Msingi Hayseng iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Screenshot_20230823_065213_Instagram.jpg
 
Mbunge wa jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangay anashikiliwa na Jeshi la Polisi kuanzia jana Agosti 21, 2023 kutokana na tuhuma za kuhusishwa kupanga tukio la kushambuliwa waandishi wa habari.

Shangay alijisalimisha polisi baada ya kupokea wito wa kufika polisi ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) na baadae alitakiwa kuripoti kituo cha Polisi Karatu.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngorongoro, Lucas Ole Seina amethibitisha leo Agosti 22, 2023 kwamba ni kweli mbunge huyo alikamatwa alipokwenda kuripoti polisi ili kuhojiwa kwa sababu kuna shida ilitokea mnadani wa Eblini kwa waandishi wa habari kupigwa.

“Baada ya kuhojiwa, ndugu na jamaa waliambiwa waende kesho asubuhi (leo) kwa ajili ya kuwekewa dhamana lakini walipofika asubuhi, hakuweza kujulikana mahali alipo. Kwa hiyo hatujui kama yupo kituoni Karatu au Arusha, kwa hiyo bado tunafuatilia kujua yuko wapi,” amesema Seina.

Hata hivyo, jitihada za Mwananchi kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo kuzungumzia kushikiliwa kwa mbunge huyu hazikuzaa matunda.

Hata hivyo, diwani wa CCM kata ya Elelai, James Moringe amedai wakati wakiwa njiani na mbunge huyo kukaribia Karatu katika eneo la Rhotia walisimamishwa na Polisi ambao walimchukuwa mbunge huyo kwenye gari lao.

Wakili Joseph Ole Shangay ambaye alikuwa ameambatana na mbunge huyo amedai baada ya mbunge kufikishwa polisi alielezwa anashikiliwa kwa tuhuma za kujeruhi watu wawili.

Hata hivyo, Wakili anayemtetea mbunge huyo, Simon Mwambo kupitia Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) amesema kuwa walipata taarifa ya mbunge huyo kufikishwa kituo cha Chekereni Arusha.

Screenshot_20230823_065325_Instagram.jpg
 
[emoji599] KITENDO kilichofanywa na mashabiki wa Simba cha kupaza sauti kumtaka Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ampe nafasi kubwa ya kucheza Moses Phiri kimemfanya mshambuliaji huyo kukiri ana deni kubwa, huku akikiri kitendo hicho kimemuongezea nguvu na kuahidi kuwapa furaha.
.
“Mashabiki wana upendo mkubwa sana kwangu, jambo linalonifanya nipate nguvu ya kupambana kuhakikisha nafanya zaidi ya kile wanachokitarajia kutoka kwangu, ingawa siwezi kusema msimu huu nataka kufunga mabao mangapi, ila nitafunga kwa kadri ninavyoweza,” alisema Phiri na kuongeza;
.
“Ushindani ni mkali kwenye timu, ambao ni mzuri kwa kila mchezaji kuongeza bidii, ndio maana nani aanze kucheza na nani aanzie benchi kocha ndiye atakayeamua kulingana anavyoona mchezo husika.”
.
Phiri alisema yupo fiti kupambana kuhakikisha ligi inayoendelea anaonyesha ushindani kuanzia kwenye kikosi hadi timu pinzani na anashukuru nafasi anayopewa na makocha wa kikosi hicho na wajibu wake ni kutowaangusha.
Screenshot_20230824_153250_Instagram.jpg
 
Simon Msuva amekuwa mmoja kati ya nyota muhimu katika kikosi cha timu ya Taifa Stars na sasa anaelekea kuanza maisha mapya ndani ya JS Kabylie inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria [emoji1026]
.
Msuva ambaye msimu uliomalizika amekuwa katika kiwango kizuri akiww Saudia Arabia amefuzu vipimo vya afya leo asubuhi tayari kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Screenshot_20230824_153350_Instagram.jpg
 
[emoji599]SIMBA kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi sita baada ya kushuka uwanjani mara mbili, huku ikielezwa kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ yupo kwenye mipango ya kufyeka wachezaji watatu kabla dirisha la usajili halijafungwa Agosti 31.
.
Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa wachezaji ambao wameshindwa kulishawishi benchi la ufundi na sasa uongozi unafikiria kuwatoa kwa mkopo kabla dirisha halijafungwa.
.
Chanzo cha kuaminika kutoka klabu hiyo kuwa Jimyson Mwanuke, kipa Ahmed Feruz na mshambuliaji Mohamed Mussa wapo sokoni kwa sasa kutokana na uongozi kutaka kuwatoa kulingana na mapendekezo ya kocha ili kuliwahi dirisha la usajili lililo wazi sababu kubwa iliyoelezwa ni wachezaji hao kushindwa kuonyesha ushindani wa kutosha ndani ya kikosi na pia uongozi ukitaka wakapate muda wa kutosha kwenye vikosi vingine.
Screenshot_20230824_153430_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom