Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa kuwa Mkuu wa KKKT mpya mteule akichukua nafasi ya Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozi wa awamu mbili.

Askofu Malasusa anarejea tena kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2015 alipomaliza na kuikabidhi kwa Askofu Shoo.

Mwenyekiti wa Uchaguzi huo uliofanyika Jijini Arusha, Askofu Amon Mwenda, amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3.
Screenshot_20230825_075804_Instagram.jpg
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa siku saba kuanzi leo August 24,2023 kwa Wananchi kusalimisha mavazi ya Jeshi au yanayofanana na sare za Jeshi ambapo baada ya siku saba Wanajeshi watakuwa mtaani kukusanya mavazi hayo na atajayekutwa nayo atakuwa ni Mwanakulitafuta na hivyo atageuka kuwa Mwanakulipata.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema “Tunatoa siku saba kuanzia leo iwe mwisho wa kuyavaa, kuyatumia au kuyauza, kwa wale Wasanii wao watafuata utaratibu wa kuomba kibali ili waruhusiwe kutumia mavazi hayo, baada ya siku saba atakayekutwa na mavazi hayo atachukuliwa hatua kali ambayo itakuwa fundisho kwa wengine”

“Mavazi yawasilishwe kwenye makambi ya Jeshi, Vituo vya Polisi au kwa Wajumbe wa Serikali za Mitaa, hatutokuuliza umeipata wapi na ukifika wakati wa chai tutakunywa nae chai pamoja, tunatoa siku saba kuyasalimisha na ambaye hatoyasalimisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya na atakuwa na lake jambo, Waswahili wanasema Mwanakulitafuta Mwanakulipata, kwahiyo Mwanakulitafuta baada ya siku saba atakuwa Mwanakulipata”

“Zipo baadhi ya Taasisi zinazowashonea Watumishi sare za aina hiyo, wapo pia Wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia katika maduka au maeneo yao ya biashara, wapo baadhi ya Wasanii wanaovaa mavazi hayo na kuyatumia wawapo kwenye majukwaa ya kazi zao bila kufuata utaratibu”

“Baadhi ya Watu wanatumia mavazi hayo kuwatapeli Wananchi kwa kujifanya Wanajeshi na wengine kufanya vitendo viovu huku wakidhaniwa kuwa ni wanajeshi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za Nchi na hakipaswi kufumbiwa macho”
Screenshot_20230825_075907_Instagram.jpg
 
Uingereza imetengeneza historia nyingine mpya baada ya Madaktari kufanikisha kumpandikiza tumbo la uzazi Mwanamke ambaye alikuwa na matatizo ya kupata Mtoto na hivyo kumwezesha kuwa na uwezo wa kubeba mimba.

Sky News wameripoti kuwa Mabingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Churchill Oxford wamepandikiza tumbo hilo kwa Mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambapo upasuaji ulidumu kwa muda wa saa tisa na dk 20 na kwa sasa aliyepandikizwa tumbo na aliyetolewa tumbo hilo wote wanaendelea vizuri na tumbo hilo la uzazi linafanya kazi vizuri.

Upasuaji wa kuondoa tumbo la uzazi kutoka kwa Mwanamke mwingine ulidumu kwa muda wa saa nane, Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye amepongezwa kwa upendo aliouonesha kwa Mdogo wake kwa kumpa tumbo lake la uzazi, yeye tayari ameshapata Watoto wawili hivyo akaona na Mdogo wake pia apate Watoto.
Screenshot_20230825_075959_Instagram.jpg
 
“Jumapili iliyopita tulicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asas Djibouti FC kikanuni tulikuwa ugenini, Jumamosi hii tutacheza mchezo wa marudiano tukiwa wenyeji.”

“Tukishinda mechi hiyo tutakuwa tumevuka hatua ya awali kwenda hatua inayofuata ambayo itakuwa imetutenganisha na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

“Tuna zaidi ya miaka 20 hatujacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika! Kila mwanachama, kila shabiki na mpenzi wa Yanga anasubiri kwa hamu kuiona timu yetu inacheza hatua ya makundi.”

“Tulishakuwa wazi kwa mashabiki mapema kabisa kwamba, lengo letu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

“Kwa hiyo nawakaribisha mashabiki wa Yanga kwa wiki uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 11:00 jioni.”

- Ally Kamwe, Mkuu wa Habari na Mawasiliano Yanga.
Screenshot_20230825_080049_Instagram.jpg
 
“Tumeuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC, tulihitaji Kenya, Uganga, Afrika Kusini, Djibouti na mataifa yote ambapo Ligi ya Tanzania inafika waone brand ya mpira wa nchi yetu.”

“Kama ambavyo ukiwa Ufaransa unasubiri kuona PSG inacheza, ukiwa Ujerumani unasubiri kuona Bayern Munich inacheza ndivyo ilivyo Tanzania, mpira hauwezi kuzungumzwa wala kuwa na ladha kama Yanga haijacheza.”

“Yanga imecheza Afrika nzima imetambua mpira wa Tanzania uko vipi, Ligi imezinduliwa na mnara umesoma 5G.”

- Ally Kamwe, Mkuu wa Habari na Mawasiliano Yanga.
Screenshot_20230825_080153_Instagram.jpg
 
Kocha Mkuu wa KMC FC, Abdi Hamid Moallin amekiri kuwa walishindwa kuifhibiti Yanga na kujikuta wakipoteza mchezo wa jana kwa idadi kubwa ya magoli.

“Tunafahamu namna ambavyo Yanga ni timu imara, kipindi cha kwanza kilimalizika tukiwa nyuma kwa goli moja, tulikuwa na changamoto nyingi kwenye kipindi cha pili kwa sababu tulifanya makosa mengi kitu ambacho kilitokana na uchanga wa timu yetu.”

“Lakini bado ninajivunia sana vijana wangu, walipambana sana ila bado tuna vitu vingi vya kuvifanyia kazi.”

“Niwapongeze Yanga kwa kucheza vizuri na hiyo inaonesha kwa nini wao ni mabingwa kwa misimu miwili mfululizo na wamezidi kuwa bora tangu nilipoanza kuwaona.”
Screenshot_20230825_080235_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemuhukumu Agustino Kahise, mkazi wa Changarawe wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 30 Jela, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka mjamazito aliyekuwa amelazwa Hospital ya Mji Mafinga.

Shauri hilo la jinai namba 33, 2023 ambalo hukumu yake imetolewa jana na Hakimu Mkazi Sekela Kyungu.

Akisoma maelekezo yaliyotolewa mahakamani hapo, Kyungu amesema kuwa mnamo April 13, 2023; majira ya usiku katika eneo la choo cha wodi ya wazazi katika hospitali hiyo, bila uhalali mshtakiwa alimbaka msichana huyo, bila ridhaa yake.

Aidha Hakimu Kyungu amesema tukio hilo lilitokea baada ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 18, kumaliza kujisaidia, na kwamba wakati anatoka chooni kuelekea wodini, ndipo alipokutana na mshtikiwa mlangoni ambaye alimzuia asitoke huku akimziba mdomo kisha kumbaka.

Hakimu huyo amesema Kahise ameshtakiwa kwa kosa la ubakaji ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na kifungu 131(1) cha sheria za kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022.

Hata hivyo aliposomewa shtaka lake, Kahise alikana kutenda kosa hilo ndipo mahakama ikaalika upande wa mashtaka ili waweze kuthibitisha, ambapo waliwasilisha vielelezo viwili pamoja na mashaidi watano.

Kyungu amesema kuwa baada ya ushaidi ambao umetolewa na pande zote mbili, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka yeyote na hivyo ikamtia hatiani kwa kifungu namba 235(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 rejeo la mwaka 2022.

Aidha Hakimu Kyungu ameeleza kuwa, kulingana na kosa ambalo Kahise amelifanya, mahakama hiyo inampa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela chini ya kifungu 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022; ili iwe fundisho kwake na watu wenye tabia kama hiyo.
Screenshot_20230825_080402_Instagram.jpg
 
View attachment 2727926
Duh

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom