Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230826_072045_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230826_072105_Opera%20Mini.jpg
 
[emoji408] 05—JUDE Bellingham amehusika moja kwa moka katika mabao matano kwenye mechi tatu za Ligi Kuu ya Hispania (LALIGA), akiwa na klabu yake mpya ya Real Madrid, akifunga mabao manne na kutoa asisti ya bao jingine moja. Nyota huyo alinunuliwa kwa pesa ndefu ya Euro 103 milion kutoka Borussia Dortmund.

Screenshot_20230826_074543_Instagram.jpg
 
BRENTFORD imesisitiza inahitaji zaidi ya Pauni 80 milioni ili kumuuza straika wake, Ivan Toney, 27, ambaye Arsenal na Tottenham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya baridi Januari mwakani.
.
Toney ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha Chama cha Soka cha England (FA) baada ya kukutwa na hatia ya kubeti ifikapo wakati huo kifungo chake kitakuwa kimemalizika.
.
Timu zote zilivutiwa na kiwango cha staa huyu alichoonyesha kabla hajafungiwa msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote, kufunga mabao 21 na kutoa asisti tano.
.
Tottenham inamuangalia straika huyo kama mbadala wa Harry Kane wakati Arsenal inamataka kama mbadala wa Gabriel Jesus ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.
Screenshot_20230826_074647_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha kwanza na inasemekena atakuwa fiti kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United baada ya mechi za kimataifa.
.
Straika huyo amekosa mechi za ufunguzi za Arsenal baada ya kupata jeraha la goti katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya. Alifanyiwa upasuaji mdogo kuondoa tatizo katika eneo la goti, lakini kocha Mikel Arteta hakuweka wazi tarehe maalumu ya kurudi uwanjani, ila kuna uwezekano ajarejea baada ya mechi za kimataifa.
.
Kutokana na kinachoendelea, Eddie Nketiah ataendelea kucheza katika safu ya ushambuliaji kwani alionyesha kiwango kizuri katika michezo miwili ya mwanzo ya Ligi Kuu England kwa kufunga na kutoa asisti. Na sasa mashabiki wa Arsenal wamepata ahueni baada ya straika huyo kuanza mazoezi ya kujiweka fiti kabla ya kurejea kukiwasha.
Screenshot_20230826_074741_Instagram.jpg
 
[emoji599] Kinda wa Barcelona, Pedri Gonzalez anaweza kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja zaidi baada ya kuumia nyama za paja wakati anafanya mazoezi. Kiungo huyo alikuwa tegemeo la ushindi wa Barcelona dhidi ya Cadiz wikendi iliyopita akifunga bao katika mechi iliyokuwa na upinzani mkali.
.
Hata hivyo, Pedri kwa mara nyingine alipata jeraha ambalo linaweza kumfanya kuwa nje ya uwanja muda mrefu. Jeraha la Pedri ni pigo kwa Barcelona, ingawa kocha Xavi Hernandez bado ana machaguo mengi ya wachezaji kwani lkay Gundogan, Gavi, Frenkie de Jong na Oriol Romeu anaweza kuwatumia kuelekea mechi zijazo.
Screenshot_20230826_075402_Instagram.jpg
 
Ufaransa imesema Wanajeshi wa Niger ambao wamempindua Rais wa Nchi hiyo hawana mamlaka ya kumtimua Balozi wa Ufaransa, mtandao wa France 24 umeripoti, kauli ya Ufaransa inakuja baada ya Jeshi la Niger kumpa saa 48 Balozi wa Ufaransi nchini Niger awe ameondoka nchini humo .

Ufaransa imesema “Watu waliofanya mapinduzi hawana mamlaka ya kumfukuza Balozi wetu, Balozi alipewa kibali cha kuwa Niger na Serikali halali iliyochaguliwa na Wananchi kidemokrasia na sio Jeshi, tunafuatilia kwa ukaribu ulinzi na usalama wa Balozi yetu”

CGTN na AFP zimeripoti kuwa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Niger imesema sababu ya kuwatimua Balozi wa Ufaransa na wa Nchi nyingine kadhaa ni kutokana na msimamo wao wa kutoiunga mkono Niger na kutaka Rais aliyepinduliwa arejeshwe madarakani.

Sababu nyingine ni Wizara za Mambo ya Nje za Mataifa hayo ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa kukataa mwaliko wa Maafisa wake kukutana na Waziri mpya wa Mambo Nje wa Niger.
Screenshot_20230826_075505_Instagram.jpg
 
Jeshi la Niger ambalo linaongoza Nchi hiyo baada ya kumpindua Rais limetoa saa 48 kwa Balozi wa Marekani nchini humo na Mabalozi wa Nchi nyingine nne za Ufaransa, Ujerumani , Ivory Coast na Nigeria kuondoka Niger.

CGTN na AFP zimeripoti kuwa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema sababu ya kuwatimua Mabalozi hao ni kutokana na msimamo wao wa kutoiunga mkono Niger na kutaka Rais aliyepinduliwa arejeshwe madarakani.

Sababu nyingine ni Wizara za Mambo ya Nje za Mataifa hayo ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa kukataa mwaliko wa Maafisa wake kukutana na Waziri mpya wa Mambo Nje wa Niger.
Screenshot_20230826_075818_Instagram.jpg
 
Mabaki ya mwili wa Mwalimu wa Shule ya awali meneo la Shabaha Kata ya Bomambuzi Mkoani Kilimanjaro ambaye alikuwa hajulikani alipo kwa siku 30, Lightness Elia (29), yamefukuliwa na mbwa katika shamba la miwa TPC na kuburuzwa hadi pembezoni mwa barabara kando na shamba hilo.

Diwani wa Kata ya Bomang'ombe, Juma Raibu ambaye alifika eneo la tukio na kuliita Jeshi la Polisi amesema alipokuwa eneo la tukio walikuta rasta zake na pochi lakini fuvu lake au kichwa chake bado havijaonekana.
Screenshot_20230826_080049_Instagram.jpg
 
Ikulu ya Urusi (Kremlin) imekanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote na ajali ya ndege inayosemekana kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ikisema tuhuma hizo ni uzushi usiokuwa na maana.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema shutuma dhidi ya Nchi yake hazina mashiko yoyote na badala yake ametizupia lawama nchi za Magharibi kwa kusambaza uvumi usio maana.

"Tazama, kwa sasa kuna uvumi mwingi sana kuhusiana na ajali hii ya ndege na vifo vya abiria wa ndege hiyo akiwemo Yevgeny Prigozhin, bila shaka, katika Nchi za Magharibi, uvumi huo unawekwa kwa njia fulani na wote ni uongo mtupu na bila shaka ni muhimu kutumia ukweli unaporipoti kuhusiana na suala hili, kwa sasa ukweli ni mchache kwa sababu uchunguzi bado unaendelea”
Screenshot_20230826_080206_Instagram.jpg
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kupiga marufuku nguo za mitumba kuingizwa Uganda akisema lengo ni Watu wa Uganda wanunue nguo mpya kutoka kwenye viwanda vinavyozalisha mavazi vya Uganda.

Rais Museveni ameagiza pia kuanzia September 01,2023 cable na metres za umeme zisiingizwe kutoka nje ya Nchi ili Watu wanunue kwenye viwanda vya Uganda.

Amesema hayo akiwa eneo la viwanda la Sino-Uganda Mbale Industrial Park, lengo likiwa ni kufanya Watu wanunue bidhaa za Uganda ili kuijenga Uganda, (Buy Uganda, Build Uganda - BUBU).
Screenshot_20230826_080331_Instagram.jpg
 
Jeshi la Kujenga Taifa JKT limetangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2023 kwa Vijana wa Tanzania Bara na Visiwani kuanzia August 28,2023 na watakaofanikiwa wataripoti kwenye makambi kuanzia Septemba 26 hadi 29, 2023

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Tawi la JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ambapo amesema utaratibu wa kuomba na kujiunga unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako Mwombaji anaishi.

Akisisitiza namna ya kujiunga ametoa rai kwa watanzania kuepuka Matapeli “Inasisitizwa nafasi hizi zinatolewa bure hakuna malipo yoyote yatakayoambatana na nafasi hizi hivyo Wazazi na Walezi wote nchini waepukane na Matapeli wanaojitokeza kwamba nafasi hizi zinauzwa”

Kuhusu sifa Brig. Jen. Mabena amesema nafasi hizo zimezingatia Vijana wenye taaluma za Uhandisi wa Ujenzi (Civil Engineers),Ufugaji, Umwagiliaji, Uvuvi, Saikolojia na Wanyamapori ambao wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao.
Screenshot_20230826_081428_Instagram.jpg
 
Samwel Nduluhundu (38) Mkazi wa Mtaa wa Ramadhani Mjini Njombe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la mauaji ya Felister Danda (24) ambae alikutwa ameuawa Ijumaa iliyopita na mwili wake kutelekezwa katika msitu wa kupandwa wa TANWAT huku Mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili akiwa hai karibu na mwili wa Mama yake.

RPC wa Njombe John Makuri amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo Ferister Danda na Mtuhumiwa Samwel Nduluhundu walikuwa Wapenzi lakini baadae marehemu aliamua kukataa kuendelea na mahusiano hayo “Samwel hakukubaliana na maamuzi ya Felister na kumtaka amrudishie vitu ambavyo amewahi kumnunulia ambapo nae alikataa kurudisha akimwambia hata yeye amemtumia”

Kamanda Makuri amesema jibu hilo lilimfanya Mtuhumiwa baada ya siku kadhaa kumrubuni Felister kwa kumshauri ampeleke kwa Mtaalamu wa tiba asili Wilaya ya Wanging’ombe kwa usafiri wa pikipiki akatibiwe ugonjwa aliokuwa nao eneo la shingo uliokuwa ukimsumbua muda mrefu ambapo Felister alikubali”

“Alhamisi usiku Mtuhumiwa alimchukua nyumbani kwake Felister akiwa na Mtoto wake ambaye alizaa na Mwanaume mwingine sio Samwel na wakaelekea Wanging’ombe lakini walipofika eneo la msitu ndipo inadaiwa alitekeleza mauaji hayo”
Screenshot_20230826_081531_Instagram.jpg
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema Kiongozi wa Jeshi binafsi la Wagner, Evgeny Prigozhin alikuwa ni Mtu mwenye vipaji vingi aliyetoa mchango mkubwa dhidi ya Utawala wa Nazi Mamboleo nchini Ukraine .

Akiongea na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kuhusu kifo cha Prigozhin, Putin amesema alimfahamu Prigozhin tangu mwaka 1990 na kumtaja kama Mtu aliyekuwa na mwisho tata usiotabirika.

“Alifanya makosa makubwa kwenye maisha yake lakini nilipomuuliza miezi ya hivi karibuni alikuwa na majibu kwa ajili yake na ushirikiano wetu, alikuwa ndio kwanza amerejea kutoka Afrika na alikutana na Viongozi kadhaa wa Urusi, alikuwa ni Mtu mwenye vipaji aliyefanya kazi Afrika na Urusi kwenye masuala ya gesi, mafuta na madini”

Kiongozi huyo na wenzake tisa wanaaminika kuwa wamefariki kwenye ndege iliyopata ajali Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Urusi, Moscow ambapo Mamlaka ya Anga ya Urusi imesema Kiongozi Mkuu wa Kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin ni miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Itakumbukwa June 24,2023 Prigozhin, Mmiliki na Mwanzilishi wa Wagner alitoa wito wa uasi wa kutumia silaha na kutishia kufanya vurugu Jijini Moscow ili kumtimua Waziri ambaye alimtuhumu kwa kuamuru kulipuliwa kwa kambi za vita za wagner group nchini Ukraine na baadaye Ikulu ya Urusi (Kremlin) ikasema Prigozhin alikubali kwenda uhamishoni nchini Belarus hii ni baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuafikiana na makubaliano ya msamaha kwa Kiongozi huyo ili kusitisha uasi.
Screenshot_20230826_081725_Instagram.jpg
 
Mwanamke mmoja nchini Kenya amefariki baada ya kutumbukia mtoni alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi katika Kaunti ya Kakamega.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo, Hellen Kadogo (35) alitumbukia kwenye Mto Yala na kuzama kufuatia msako wa wauza pombe haramu maarufu Chang’aa ambayo imepigwa marufuku katika eneo hilo.

"Alipowaona maofisa hao, aliogopa kukamatwa kwa sababu hakuwa na pesa za kuwapa, hivyo aliamua kuwakimbia," mzee mmoja katika eneo hilo alisema.

"Nilimsikia akijiuliza ni nini atafanya baada ya kusikia kuhusu msako huo mwishowe alianguka mtoni katika jitihada za kuwakimbia polisi," shuhuda mwingine alieleza.

Kutokana na kifo cha mwanamke huyo, wakazi wa eneo hilo wamemlaumu kiongozi wa eneo hilo.

Screenshot_20230826_081857_Instagram.jpg
 
Wakati mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ukifikia asilimia 91, Menejiment ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imeongeza wafanyakazi wengine 24 katika bwawa hilo, na hivyo kufikishwa wataalam 92, wanaondaliwa kuendesha mradi huo pindi utakapokamilika Juni mwaka 2024.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Agosti 25, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande alipotembelea mradi huo, akiambatana na timu ya menejementi ya Tanesco.

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia mwenendo wa ujenzi wa mradi na tathimini ya hali ya mvua za vuli zinazotarajiwa kunyesha kati ya Oktoba hadi Disemba.

Amesema maendeleo ni mazuri hadi Julai tulifikia asilimia 90.19 na tunatarajia mwishoni mwa Agosti tutafikia asilimia 91, akisema tayari wameshaongeza wafanyakazi zaidi ya 20 kwa ajili ya kujiandaa kuendesha mradi utakapokamilika.

Chande amesema ili mradi huo uanze kufanya kazi, wafanyakazi 221 wanahitajika kuuendesha, na kwamba kwa sasa wanapelekwa kwa awamu kulingana na hatua ya mradi unapofikia.

"Watu 221 huwezi kuwaleta kwa wakati mmoja, bali kwa makundi yatakayokuja kwa wakati husika, mfano sasa hivi kundi hili lililokuja linahusika uhandisi wa umeme kwa sababu mitambo ndio inafungwa. Kwa hiyo huko mbeleni kukiwa na uhitaji wa watalaamu wa aina hii basi wapo.

"Kwa sababu mradi upo nje ya mji, kutakuwa na wafanyakazi madaktari, walimu wa shule za awali, wahasibu. Tutaendelea kuongeza wafanyakazi kwa makundi kulingana na hatua ya ujenzi wa mradi utakapofikia," amesema Chande.
Screenshot_20230826_082001_Instagram.jpg
 
Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa mpira wa miguu kuvutiwa na ushangiliaji wa baadhi ya wachezaji, kuna wakati mchezaji hupendwa na mashabiki kutokana na aina ya ushangiliaji wake.

Ukimzungumzia aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele watu wengi wanaelewa aina ya ushangaliaji mara tu baada ya kutikisa nyavu, jambo ambalo si wakubwa tu bali hata watoto wanalielewa.

Staa wa zamani wa Barcelona, PSG na mshindi mara saba wa Ballon d’Or, Lionel Messi wengi wamemzoea kwa aina ya ushangiliaji wake wa kunyoosha vidole angani bila kujua maana yake.

Aina ya ushangiliji wa staa huyo anayechezea kwa sasa Inter Miami ya Marekani imekuwa ikivutia watu wengi, huku akitumia ishara hiyo ya kunyoosha vidole angani akiamini kuwa anatoa salamu za heshima kwa marehemu bibi yake.

Screenshot_20230826_082103_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom