Makapuku Forum

Beki wa Real Madeid, Dani Carvajal amekiri wachezaji wenzake walidhani Kylian Mbappe angejiunga nao katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
.
Straika huyo wa Paris Saint-Germain alihusishwa na Madrid baada ya kugoma kusaini mkataba mpya PSG, lakini alibaki. Lakini kwa mujibu wa beki huyo, waliona kila dalili kwamba Mfaransa huyo angetua Santiago Bernabeu baada ya kujadili na wenzake.
.
Carvajal alisema: “Siwezi kudanganya kwamba hatukujadili, lakini wakati tupo katika ziara Marekani maneno mengi yalizungumzwa. Nilidhani angejiunga (Madrid) na nilijua Mbappe angechagua timu yetu. Baada ya kukosa ziara ya PSG niliamini anatua kwetu, lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia.”

Mbappe alitatua mzozo na mabosi wake PSG ambao ulidumu muda mrefu bila kupata muafaka kuhusu hatima yake.Taarifa zilidai angesaini mkataba mpya PSG utakaodumu hadi 2026.
 
[emoji599] KIUNGO mpya wa Manchester United, Sofyan Amrabat yupo fiti na amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Morocco [emoji1173] kwa ajili ya mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
.
Taarifa ya awali zilidai kiungo huyo vipimo vyake viligundulika kuwa ana tatizo la mgongo kama straika mpya Rasmus Hojlund wakati anajiunga akitokea Atalanta. Jambo hilo lilizua taharuki kwa mashabiki, lakini imeripotiwa kwamba kiungo huyo hatakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita kama ilivyoelezwa siku chache baada ya kutambulishwa.
 
Nyota wa timu ya taifa ya wanawake Hispania Jenni Hermoso alitoa taarifa ya kunyanyaswa kihisia usiku wa Agosti 27 ambapo amemtuhumu bosi wa soka wa nchi yake ambaye alionekana kumbusu kwa nguvu baada ya ushindi wao wa mwisho kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uingereza.

Rais wa Shirikisho la soka Hispania Luis Rubiales (46) alimbusu Hermoso kwenye midomo na pia alionekana akishika mgongo wa binti huyo bila ridhaa ya binti.

Hermoso aliibuka na kusema kuwa hakukubali busu na akamshutumu Louis na FA ya Hispania kwa kuunda mazingira ya 'ujanja' kumnasua kiongozi huyo ambaye awali iliaminika pengine angeachia ngazi kutokana na kashfa hiyo badala yake alivituhumu vyombo vya habari na mchezaji huyo huku akisisitiza kwamba hatajiuzulu na busu hilo lilikuwa la makubaliano.

Baada ya kukataa kuacha kazi yake na kulaumu chama cha ufeministi cha nchi hiyo ,

Siku ya jana Kocha wa timu hiyo ya taifa Jorge Vilda amefutwa kazi na chama cha soka cha nchi hiyo licha ya kuipa taji timu hiyo kutokana na ukaribu wake na Luis

Hadi kufikia leo Wachezaji 15 wa timu ya soka ya wanawake ya Hispania nao wamesema hawataichezea nchi yao tena hadi rais Luis Rubiales atakapoondolewa kwenye nafasi yake.

Mbali na wachezaji raia na vyama mbali mbali vipo upande wa Hermoso wakimtaka Louis aachie ngazi kwa kufanya unyanyasaji kwa binti huyo
 
[emoji2424] Kocha Mkuu wa Al Merreikh, Osama Nabieh ::
.
“Wenzetu (Yanga) ukiangalia mechi zao wanaonekana wako tayari. Ni timu ambayo iko fiti na kitu kibaya zaidi kwetu ni kwamba wameshinda mechi za ligi na mbili za Afrika” alisema Nabieh, raia wa Misri.
.
“Tunalazimika kucheza mechi kama hizi za kirafiki ambazo sawa zinaweza kutusaidia, lakini sio kwa ukubwa kama utakapocheza mechi za ushindani kama ligi. Tutaendelea kujipanga zaidi tukiangalia kama tutapata mechi nyingine hapa karibuni ya kirafiki.“
.
“Ubora wao mkubwa uko eneo la kiungo mechi ambazo tumeziangalia kama hatutakuwa na ubora wa kuwadhibiti eneo hilo tunaweza kufanya makosa, lakini pia kwenye ulinzi pia ni timu nzuri.
.
“Haitakuwa mechi rahisi kwetu na hata kwao, nimewaambia wachezaji wangu hii ni sawasawa na FAINALI kwetu itakayoamua safari yetu kwenye mashindano haya, tunatakiwa kucheza kama wanajeshi.”
 
[emoji187] lNasikia Morrison alijaribu kuwasiliana na viongozi wa Simba lakini wakamfungia milango. Rafiki zangu Singida Fountain Gate wakamkwepa kwa sababu walizifahamu tabia zake. Hatimaye ameangukia Morocco. Sio nchi nzuri sana kwake. Afrika Kusini na Tanzania zilikuwa nchi nzuri kwake kuishi, lakini sidhani kama atafurahia maisha ya Morocco.
.
Nadhani maisha ya Morocco yapo kwa ajili ya wachezaji walio ‘serious’ na maisha ya soka kama Saimon Msuva. Ukiwauliza kina Chama watakwambia jinsi maisha ya Waarabu yalivyo magumu. Kwa mchezaji anayependa POMBE na WANAWAKE maisha ya Morocco hayawezi kuwa mazuri kwake.
.
Zaidi ya yote Morrison amekwenda katika timu ambayo imeweka makazi yake katika kambi ya JESHI. Kuna taratibu nyingi pia za Kiislamu ambazo kwa namna ninavyomuona mchezaji kama Morrison sijui kama atawezana nazo. Nasema hivi kwa sababu nimewahi kwenda Morocco mara mbili na najua tamaduni zao zilivyo.
.
Morrison alipaswa kutulia Tanzania na kucheza kwa miaka mingi ijayo kwa sababu ana kipaji kikubwa. Tatizo lake kubwa lilikuwa kuzichukulia poa timu za Tanzania.
 
[emoji2424] Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema ubora wa Luis Miquissone na Aubin Kramo unamuongezea upana wa kikosi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na African Super League.

.“Nimetoa nafasi kwa wachezaji wote ili kupata nafasi ya kuona uwezo wa kila mmoja. Nafurahi kuona Miquissone ameanza kuonyesha uwezo mzuri kama leo nimempa dakika zote na ameonyesha kiwango bora.

“Kwa upande wa Kramo licha ya kuingia kipindi cha pili kwenye mechi zote mbili za kirafiki, pia amenipa kitu kikubwa akifunga mabao mawili. Nitaendelea kumpa nafasi zaidi ili kuwa bora zaidi ya alipo sasa,”

“Ni mchezaji mzuri lakini bado naendelea kumpa muda zaidi ili apate uzoefu wa ligi ya Tanzania. Tayari nimeanza kumpa dakika chache kwenye mechi za kirafiki na ameonyesha uwezo mkubwa kwani ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na naamini watatusaidia,”

 
Osama🤣🤣
 
Wakati Rais Samia Suluhu akiahidi kulitafutia Jeshi la Polisi Sh125 bilioni ili lisimamie vizuri uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu, wadau wameainisha mambo linalopaswa kufanya na wasiyostahili kuyafanya.

Wadau hao wakiwemo wasomi, wanasiasa na watetezi wa haki za binadamu, wametaka jeshi hilo litimize wajibu wa kikatiba na kisheria wa kulinda raia na mali zao, na lisigeuke kuwa mwamuzi wa ndondi ambaye ana bondia wake mfukoni.

Kulingana na wadau hao, dalili zinaonyesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 utakuwa na ushindani mkubwa kwa vyama na wagombea, hivyo polisi wasiwe chanzo cha vurugu kwa kupendelea upande wowote.

Wakili David Shillatu ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Mawakili nchini (TLS), kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga alienda mbali na kusema Jeshi la Polisi lina wajibu mkubwa kuhakikisha chaguzi hizo zinakuwa za haki na huru. “Kama alivyosema Rais, polisi wana dhamana ya kuhakikisha huu uchaguzi unapita salama.

Niwasihi sana wafanye majukumu yale tu yanayowahusu na wasiwe na upendeleo katika maamuzi yao,” alisema.

Chaguzi hizo mbili zinaenda kufanyika huku wadau wakiwa na kumbukumbu ya kile kilichotokea katika chaguzi kama hizo zilizopita, huku jimbo la Kawe kukiwa na taarifa za kukamatwa watu walioshukiwa kuwa polisi wakiwa na vibegi vye kura.

Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Faraja Kristomus alisema Jeshi la Polisi linatakiwa kubadilika kulingana na mabadiliko ya nyakati, kwa kuwashauri wa mamlaka za juu badala ya kupokea maelekezo.

“Wanasiasa siyo wajuzi wa masuala ya ulinzi, amani na usalama, wao matakwa yao ni kushinda uchaguzi na kuendelea kuwa madarakani, kwa hiyo hivi ni vitu viwili ambavyo mara nyingi huwa vinashindana.
Migogoro mingi Afrika inatokea kwa sababu hiyo,” alisema Dk Kristomus.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…