Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakati Rais Samia Suluhu akiahidi kulitafutia Jeshi la Polisi Sh125 bilioni ili lisimamie vizuri uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu, wadau wameainisha mambo linalopaswa kufanya na wasiyostahili kuyafanya.

Wadau hao wakiwemo wasomi, wanasiasa na watetezi wa haki za binadamu, wametaka jeshi hilo litimize wajibu wa kikatiba na kisheria wa kulinda raia na mali zao, na lisigeuke kuwa mwamuzi wa ndondi ambaye ana bondia wake mfukoni.

Kulingana na wadau hao, dalili zinaonyesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 utakuwa na ushindani mkubwa kwa vyama na wagombea, hivyo polisi wasiwe chanzo cha vurugu kwa kupendelea upande wowote.

Wakili David Shillatu ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Mawakili nchini (TLS), kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga alienda mbali na kusema Jeshi la Polisi lina wajibu mkubwa kuhakikisha chaguzi hizo zinakuwa za haki na huru. “Kama alivyosema Rais, polisi wana dhamana ya kuhakikisha huu uchaguzi unapita salama.

Niwasihi sana wafanye majukumu yale tu yanayowahusu na wasiwe na upendeleo katika maamuzi yao,” alisema.

Chaguzi hizo mbili zinaenda kufanyika huku wadau wakiwa na kumbukumbu ya kile kilichotokea katika chaguzi kama hizo zilizopita, huku jimbo la Kawe kukiwa na taarifa za kukamatwa watu walioshukiwa kuwa polisi wakiwa na vibegi vye kura.

Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Faraja Kristomus alisema Jeshi la Polisi linatakiwa kubadilika kulingana na mabadiliko ya nyakati, kwa kuwashauri wa mamlaka za juu badala ya kupokea maelekezo.

“Wanasiasa siyo wajuzi wa masuala ya ulinzi, amani na usalama, wao matakwa yao ni kushinda uchaguzi na kuendelea kuwa madarakani, kwa hiyo hivi ni vitu viwili ambavyo mara nyingi huwa vinashindana.
Migogoro mingi Afrika inatokea kwa sababu hiyo,” alisema Dk Kristomus.

View attachment 2741711
Yaani wapewe hela then wasifuate maelekezo!!! Hiiiii baghosha 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Shunie Asante kwa kutukeep up-to-date your such a darling, a special Angel 😇 have a wonderful day and stay healthy.
 
Wanasayansi wameunda kitu kinachofanana na kiinitete cha mwanadamu, bila kutumia mbegu za kiume, mayai au tumbo la uzazi.

BBC imeripoti kuwa timu ya Taasisi ya Weizmann imesema kuwa mfano wao wa kiinitete, uliotengenezwa kwa seli shina, unaonekana kama mfano wa kiinitete halisi cha siku 14.

Pia ilitoa homoni ambazo ziligeuza kipimo cha ujauzito kuwa chanya kwenye maabara.

Matarajio ya miundo ya kiinitete ni kutoa njia ya kimaadili ya kuelewa nyakati za mwanzo za maisha ya binadamu.
Screenshot_20230907_080750_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amelaani shambulio la "makusudi" dhidi ya mji wa mani wa nchi hiyo wa Kostyantynivka.

BBC imeripoti kuwa takribani watu 16, akiwemo mtoto, waliuawa katika mlipuko huo, ambao ulitokea kwenye mtaa wa soko lenye shughuli nyingi katikati ya siku, jambo ambalo ni la nadra.

Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha mlipuko mkali mwishoni mwa barabara ambapo watu walikuwa wakifanya manunuzi na shughuli za kawaida sokoni hapo.

Russia bado haijasema lolote kuhusu shambulio hilo.

Rais Zelensky, ambaye ameilaumu Moscow, amesema waliouawa ni "watu ambao hawakufanya lolote baya" na kuonya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Takribani watu 28 wanadhaniwa kujeruhiwa. Soko, maduka ya bidhaa na dawa, vyote vimeripotiwa kushambuliwa.

Polisi na wahudumu wa uokoaji wako kwenye eneo la tukio, wakiendelea kutafuta watu walionusurika na shambulio hilo, linaloonekana kuwa baya zaidi la aina yake kwa miezi kadhaa sasa.
Screenshot_20230907_082500_Instagram.jpg
 
Mahakama nchini Nigeria, imeidhinisha matokeo ya kura za urais, yaliyomwingiza madarakani Rais Bola Tinubu, kwa kutupilia mbali rufaa ya kesi hiyo ikisema "haikuwa na sifa."

Rais huyo alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na ushindani Februari mwaka huu, ambapo wagombea walioshindwa walikimbilia mahakamani kupinga matokeo hayo wakisema ulikuwa na dosari.

Atiku Abubakar wagombea wa People's Democratic Party, na Peter Obi wa Labour Party, walikuwa wamedai ukiukaji wa sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kutokutumika mashine za kielektroniki kujaza matokeo ya vituo vya kupigia kura.

Hata hivyo, majaji wametupilia mbali madai hayo kuwa "hayafai."
"Ni dhahiri kwamba walalamikaji wameshindwa kuthibitisha," amesema Haruna Tsammani, mkuu wa jopo hilo na kuongeza;

"Hawajaweza kutoa ushahidi wowote unaokubalika, unaoaminika na unaokubalika."

DW imeripoti kuwa uamuzi huo unatarajiwa kupelekwa katika Mahakama ya Juu, ambapo Abubakar na Obi wanaweza kukata rufaa ndani ya siku 60.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Mahakama ya juu haijawahi kutoa uamuzi wa kutengua matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Nigeria tangu nchi hiyo irejee kwenye demokrasia kutoka kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999.
Screenshot_20230907_082606_Instagram.jpg
 
Dereva wa bodaboda mkazi wa mtaa wa Makoko Manispaa ya Musoma, Morice Ally (30) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi wakati akibishania chenji ya Sh1,500 kwenye kituo cha mafuta.

Dereva huyo na watu wengine wanadaiwa kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu katika kituo cha mafuta (jina limehifadhiwa) kilichopo barabara ya Majita Manispaa ya Musoma wakisubiri kujaziwa mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.

Kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda huyo alipigwa risasi tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere kwa matibabu na baadaye alifariki dunia.

Katibu wa bodaboda Manispaa ya Musoma,Shukran Mtaki alisema tukio hilo lilitokea Septemba 1, 2023 saa 2.35 usiku katika kituo hicho.

Alisema Morice aliomba kuwekewa mafuta ya Sh3,500 kisha akatoa Sh5,000 na alipodai kurudishiwa chenji, ndipo muhudumu wa kituo hicho alidai kumuwekea mafuta ya Sh5,000.

"Alipoomba chenji yule muhudumu akadai ameweka mafuta ya hela yote wakaanza kuvutana na wakajikuta wanarushiana ngumi ndipo mlinzi wa kituo alipofika kwenye eneo hilo na kumvuta bodaboda wakatoka nje kidogo ya kituo," alidai Mtaki.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Dismas Kisusi alipozungumza na Mwananchi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo, Kisusi alisema chanzo cha ugomvi huo ni baada ya dereva bodaboda kukaidi agizo la kutoka kituoni hapo ili apishe watu wengine wapate huduma.
Screenshot_20230907_082713_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom