Makapuku Forum

.
[emoji408] 02—NIGERIA [emoji1184] imekuwa taifa la kwanza la Afrika kutoa wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa upande wa wanaume na wanawake baada ya Victor Osimhen na Asisat Oshoala kutajwa katika orodha.
 
ALGERIA MALALAMIKO KIBAO
.
Kocha wa Algeria, Djamel Belmadi ameonekana kutofurahishwa na uamuzi wa Chama cha soka nchini humo kupeleka mechi Annaba akidai ni uwanja ambao hauna ubora akitaja umeathiri ufanisi wa timu yake.
.
“Uwanja hauko tayari kuandaa mechi ya timu ya taifa, hivyo tunatakiwa kutafuta suluhisho lingine. Uwanja haupo kama ulivyokuwa mwezi Juni. haupo katika ubora ambao tunautaka kwa mechi ya kimataifa,” alisema Belmadi.
 
USAJILI [emoji404]

Zimepita siku nane tangu kufungwa kwa Dirisha la usajili barani Ulaya huku dirisha la usajili Saudia nalo linakaribia kufungwa siku chache zijazo.

Hawa ni baadhi ya nyota ambao walihusishwa na Klabu za Saudi Arabia lakini mambo hayakwenda sawa.

Mo Salah
Bernado Silva
Hakim Ziyech
Kylian Mbappe
Rodrigo De Paul
Alvaro Moratta
Marco Verati
Jadon Sancho .

 
Wakati bei ya Petroli Tanzania Bara ikifikia Sh3,213 kwa lita moja,hali ni tofauti visiwani Zanzibar ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), imetangaza bei mpya za mafuta huku bei ya Petroliikishuka kutoka Sh2,970 hadi Sh2,950.

Kuipitia taarifa iliyotolewa kwa umma leo Ijumaa Septemba 8, 2023 na Mamlaka hiyo imesema mafuta ya ndege na Diseli ndio pekee yaliyopanda bei.

Kulingana na taarifa hiyo, bei ya diseli imepanda kutoka Sh2,843 kwa mwezi Agosti hadi kufikia Sh3,012 kwa mwezi Septemba, huku bei ya mafuta ya taa yakibaki Sh2,921 kama ilivyokuwa mwezi Agosti.

Kwa bei ya mafuta ya ndege lita itauzwa kwa Sh2,448 kwa mwezi Septemba tofauti na Sh2,365 iliyouzwa mwezi Agosti.
 
Duniani kumekuwa na michezo ya aina nyingi sana, ambayo yote huwa na mashabiki wake na mara nyingi wanakuwa na mapenzi ya dhati kwa timu zao, hadi kufikia hatua ya kufanya chochote kwa ajili ya timu hizo pale zikifungwa ama kufunga.

Mara nyingi mashabiki huwaza matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji wao na ndiyo maana ikitokea wakapoteza katika mchezo, mashabiki hutokwa na maneno mengi ya kujitetea.

Katika mchezo wa mpira wa miguu na kama unadhani si jambo rahisi kwa timu moja kumfunga mpinzani wake goli 20 au zaidi ndani ya dakika 90, basi tambua kuwa mwaka 1950 timu ya Taifa India ilimchapa Nigeria magoli 99 - 1.
 
Katika habari kubwa za wiki hii ni pamoja na hii ya hisa za Kampuni ya Apple ya Marekani kushuka kwa asilimia 2.9 kutokana na ripoti za mipango ya China kupiga marufuku matumizi ya simu za Kampuni hiyo (iPhones) kwa Mashirika na Kampuni za kiserikali na kupelekea wasiwasi kwa Wawekezaji juu ya uwezo wa Kampuni hiyo kuendelea kufanya biashara katika uchumi wa pili kwa ukubwa duniani (China).

Apple imepoteza takriban dola Bilioni 200 ndani ya siku mbili baada ya tamko hilo la China, Taifa ambalo ndilo soko kubwa zaidi la nje kwa bidhaa za Kampuni hiyo ambapo mauzo yaliyofanyika Nchini humo yaliwakilisha karibia moja ya tano ya mapato yote ya kampuni hiyo mwaka jana.

CNN wameripoti kuwa japo Apple huwa haisemi ni Nchi gani zimeongoza kwa kununua simu zake, Wachambuzi katika kampuni ya utafiti ya TechInsights wanakadiria kuwa kulikuwa na mauzo makubwa ya iPhone nchini China kuliko hata Marekani kwenyewe mwaka uliopita huku ikikumbukwa kwamba Apple inatengeneza iPhones zake nyingi katika Wiwanda vya China.

Wachambuzi wa Benki ya Amerika Alhamisi wiki hii walisema kuwa uwezekano wa kupiga marufuku iPhone umekuja kutokana na ujio wa simu mpya na ya hali ya juu iliyotengenezwa na Kampuni ya China ya Huawei.
 
Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo September 08,2023 amefunga Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF 2023) akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
 
Wabunge wa Marekani wameoneshwa kuwa na wasiwasi kutokana na ongozeko la Raia wa Nchi za kigeni hususani China kununua ardhi ya Marekani japokuwa Majimbo mengi sasa hivi yapo tayari kupitisha sheria ya kupiga marufuku au kuzuia Mashirika ya kigeni kumiliki ardhi nchini humo.

Changamoto ya kupitisha sheria inayokataza Raia wa nje kumiliki ardhi nchini Marekani imetafsiriwa na Wanaharakati kuwa ni kauli ya chuki dhidi ya Raia wa kigeni kitendo ambacho hakikubaliki.

Mbunge Dan Newhouse ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Washington amesema “Tumeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya ekari zilizonunuliwa na Wafanyabiashara kutokea nchini China na ongezeko la uwekezaji limekua kwa 10% katika miongo 10, ongezeko kubwa ambalo litaendelea katika siku za karibuni, inabidi mkumbuke kuwa China sio Mshirika wetu, ni Adui”

Wabunge wengi kutokea Marekani wanahofu ya kuwa Wachina wakiweza kudhibiti ardhi na mashamba nchini Marekani, itawaongezea uwezo wa kuendesha soko la ugavi na chakula, kuchunguza taarifa nyeti za kijeshi au hata kuiba mali muhimu za kiakili za Wamekani.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) leo September 08,2023 imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli ,mafuta ya ndege na mafuta ya taa ambapo kwa upande wa dizeli kwa mwezi September imeonekana Kushuka hadi Tsh. 2950 tofauti na bei ya mwezi August ambayo ilikuwa 2,970.

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano ZURA, Mbaraka Hassana amesema dizeli imepanda kwa Tsh. 169 kutoka Tsh. 2843 mwezi August,2023 hadi Tsh. 3012 mwezi huu September.
 
...hawa jamaa wanaagiza kwingine tofauti na EWURA wanapoagiza!? (Nisome vizuri, najua wao ni wapanga bei tu na sio waagizaji )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…