Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230910_064318_Opera%20Mini.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Jumatatu Septemba 11, 2023 amepata dhamana baada ya kutoa maelezo katika kituo kikuu cha polisi Arusha akiwa pamoja na walinzi wake na ametakiwa kurejea polisi hapo baada ya mwezi mmoja.

Lissu amesema tuhuma alizodaiwa kuzitenda ni kufanya mikusanyiko isiyo halali na kufunga barabara wilayani Karatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.

Screenshot_20230911_150611_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom