Makapuku Forum

“Kuna uhuru wa maoni lakini, huu uhuru una mipaka yake sio tu kisheria hata kibinadamu… huwezi kusimama tukaona tu unafanya kama wengine wanavyofanya, hasa kama una dini,” Rais Samia Suluhu Hassan katika kikao maalumu cha baraza la vyama vya siasa leo Septemba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
 
Siku mbili baada ya mfanyabiashara maarufu wa tumbaku mkoani Shinyanga, Safari Manjala (54) kudaiwa kujiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu, inadaiwa marehemu alifikia hatua hiyo baada ya kufilisika.

Hata hivyo, Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kennedy Mgani alipoulizwa Septemba 9, 2023 na Mwananchi Digital, alisema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Manjala ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Kata ya Ulowa wilayani Kahama, alijiua Septemba 8, 2023 saa mbili asubuhi baada ya kurudi kutokea kwenye shamba lake la miti kijiji cha Ilomelo, Halmashauri ya Ushetu.

Akizungumza kwa njia ya simu jana kaka wa marehemu, Mihayo Manjala alisema marehemu aliyekuwa akihudumiwa na chama cha msingi (Amcos) Iginhyabalimi, aliingiziwa fedha na kampuni ya Mkwawa siku tatu kabla ya kujiua na kuwalipa wakulima wake wote.

Baada ya kukamilisha malipo hayo kwa wakulima, alianza kulalamika kuishiwa fedha.

“Sijajua vyema lakini aliwalipa wakulima wake wote fedha ikaisha, sikuongea naye tangu alipotoka kuwalipa wakulima wake. Marafiki zake waliniambia aliwapigia kuwaambia ana shida na hela,” alisema.

 
Juhudi za uokoaji nchini Morocco zimekuwa zikisuasua kutokana na miundombinu kama barabara kuharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo Septemba 9, 2023 ambalo lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,120 huku wengine zaidi ya 2,400 wakijeruhiwa.

Tetemeko hilo limesababisha mamia ya watu nchini Morocco kulala barabarani kwa siku ya tatu mfululizo huku wengine wakikosa mawasiliano kutokana na kukatika kwa umeme.

DW imeripoti kuwa kuharibika kwa miundombinu kumesababisha wananchi hao kushindwa kupata misaada kutoka kwa wasamiaria wema kutokana na barbara kushindwa kupitika kutokana na maporomoko ya mawe.

Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu 300,000 wameathiriwa na tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.8 na baadhi ya raia nchini humo wamekuwa wakilamika katika mitandao ya kijamii kuwa Serikali haikuwa ikiruhusu misaada zaidi kutoka nchi za nje.
 
Rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ametangaza kujiuzulu katika nafasi yake baada ya kuandamwa na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia baada ya kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya nchi hiyo, Jenni Hermoso.

Hermoso (33) alisema busu alilopigwa na Rais huyo halikuwa la maafikiano wala makubaliano kati yao na tayari alishawasilisha madai ya kisheria.

Rubiales alikumbwa na tuhuma hiyo siku ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake baada ya ushindi wa Hispania dhidi ya Uingereza.

Kwa upande wake Rubiales alisema amewasilisha kujiuzulu kwake kwa Kaimu Rais wa shirikisho hilo.

"Siwezi kuendelea na kazi yangu," alimwambia mtangazaji Piers Morgan kwenye kipindi chake cha televisheni.

Aidha, Rubiales pia amejiuzulu wadhifa wake kama Makamu wa Rais wa Kamati Kuu ya Uefa.

Siku ya Ijumaa, mwendesha mashtaka aliwasilisha malalamiko katika mahakama kuu ya Hispania - kufuatia ushahidi wa Hermoso siku ya Jumanne - dhidi ya Rubiales kwa unyanyasaji wa kijinsia na kulazimishwa.

Rubiales alidai busu hilo lilikuwa "la kuheshimiana na "ridhaa".
Wachezaji 81 wanawake Hispania, wakiwemo washindi wote 23 wa Kombe la Dunia, walisema hawataichezea tena timu ya Taifa kama bado Rubiales atakuwa kwenye nafasi yake.
 
Ni bandika, bandua ya mijadala, ndivyo unavyoweza kuelezea kwa yanayoendelea nchini kupitia mitandao ya kijamii, mikutano ya hadhara na ya wanahabari ambapo mambo saba yakitikisa zaidi.

Mijadala juu ya mkataba wa makubaliano (IGA) kati ya Serikali za Tanzania na Dubai kuhusu uendelezaji wa bandari za bahari na maziwa kupitia kampuni ya DP World ya Dubai na haja ya Katiba mpya, ndiyo imeshika hatamu.

Mingine inayotikisa kwa sasa ni juu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu wa 2025, kuadimika kwa Dola ya Marekani na ukosefu wa mafuta katika baadhi ya miji sambamba na bei kupanda.

Pia suala la kuhama kwa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na kukatikatika kwa umeme katika maeneo mengi ya nchi. Mkoa wa Kilimanjaro ikitajwa huenda kuna mgawo usio rasmi kwa kuwa kila siku baadhi ya maeneo hukosa nishati hiyo kwa saa 12.

 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Sept 11,2023 ameshiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo amevitaka Vyama kutumia mikutano hiyo kujijenga na sio kutukana, kutoa kashfa na kuchambua Dini za Watu.

Rais Samia amesema “Tumeruhusu mikutano ya hadhara ili Vyama vizungumze Wananchi wasikie sera zao ili Vyama vikue virudishe wale waliowapoteza tukienda kwenye Uchaguzi Vyama vimejipanga vya kutosha”

“Hatukutoa fursa ya mikutano ya Vyama vya Siasa ili Watu wakavunje sheria, wakasimame kutukana, wakasimame kukashfu, wakasimame kuchambua dini za Watu lakini sishangai kwanini haya yanatokea kwasababu ya kuzungumza hakuna”

“Tulianza oooh na Katiba ikaenda ikakatika katikati, ikaja ooh Bandari ikaenda ooh Katiba tena, hakuna na inapokuwa hakuna unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza lisilokuwepo”

“Niombe Vyama vya siasa tutumie fursa kujijenga kwa Wananchi, ili Wananchi wawaunge tena mkono tukienda kwenye uchaguzi Vyama vyote viwe vimejipanga”
 
AZAM FC juzi ilipata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Arta Solar ya Djibouti katika mchezo wa kirafiki ambao kwa mara ya kwanza beki wa zamani wa Yanga, Djuma Shabani aliitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya kukwama kusajiliwa katika dakika za mwisho za dirisha la usajili lililofungwa Agosti 31.

Sasa habari zilizopo ni kwamba, tayari pande zote mbili zimeshakubaliana zikisubiria dirisha dogo, lakini kazi ikiachwa mikononi mwa kocha mkuu Youssouph Dabo ili kumsoma kwa sasa ndani ya kikosi hicho na kuchagua mchezaji gani wa kumchomoa ili beki huyo Mkongomani achukue nafasi kulingana na kanuni.

Chanzo changu makini kimenidokeza kuwa mastaa waliokalia kuti kavu ni kipa Ali Ahamada aliyetakiwa kumpisha Djuma ila aligoma baada ya kudai viongozi walichelewa kumpa taarifa hizo.

Mbali na Ahamada, kipa mwingine Mghana Abdulai Iddrisu huenda pia akaachwa kutokana na kile kinachoelezwa kutokuwa kwenye maelewano mazuri na kocha wake wa makipa, Khalifa Ababakar Fall.

Endapo Iddrisu ataachwa itatoa nafasi kwa kipa Mnigeria, John Noble anayekipiga kikosi cha Kitayosce kusajiliwa kwani viongozi wa timu zote mbili wamewasiliana juu ya upatikanaji wake.
 
[emoji599] Licha ya kwamba Al Merrikh waliweka kambi ya maandalizi ya msimu huu ‘Pre Season’ nchini Rwanda tangu mwezi uliopita, lakini hawana matokeo mazuri
.
Merreikh ikiwa Rwanda ilicheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Bugasere ilipigwa 3-1, ikatoka suluhu na Chievo Sports na kisha kulala 1-0 kwa watetezi wa Ligi Kuu ya nchini humo, Rayon Sports.
 
[emoji599] Kocha Robertinho amesema anataka mastaa wote wa Simba kuwa kambini na kuondoka kwenye msafara mmoja kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano kikosini.
.
Kocha Robertinho anapiga hesabu za kupata USHINDI kwenye mechi hiyo ya ugenini kabla ya kurudiana nyumbani wiki ijayo, na tayari amewaita haraka mastaa wote waliokuwa timu za taifa ili wajiunge na wenzao na kupewa mifumo na namna watakavyotakiwa kucheza kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola Zambia.
.
Chanzo changu kimesema Clatous Chama alitaka kuisubiri Simba akiwa Zambia, lakini Robertinho amekataa akitakiwa kuwahi kambini Dar kama ilivyo kwa Inonga atakayetua kesho na kuingia moja moja kwenye kambi hiyo iliyopo MO Simba Arena, huku Saido akipata zali la kutakiwa kuungana na timu mjini Ndola kwani anacheza ugenini kesho. Saido atacheza mechi kesho akiwa na Burundi itakayokuwa ikiwania tiketi ya Afcon mbele ya Cameroon.
 
Iko hivi. Kutokana na kuwepo vita huko Sudan, Al Merrikh ilihamishia maskani yake Rwanda na kucheza mechi zake za kimataifa jijini Kigali dhidi ya Otoho katika mechi iliyopigwa Uwanja ya Huye, lakini safari hii imehamishia mchezo dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kigali Pele, lakini Merrikh ni kama imeitega Yanga kiaina.
.
Tayari Yanga imejaza mabasi yasiyopungua 10 ya mashabiki wanaotarajia kwenda Rwanda kuipa sapoti timu yao, lakini hadi sasa ukiachana na uongozi HAKUNA shabiki hata mmoja mwenye tiketi ya kuingia kwenye uwanja huo wa Kigali Pele unaobeba mashabiki 22,000 tu.
.
Wenyeji hao hawajatoa idadi ya mashabiki watakaoingia uwanjani kwenye mchezo huo na wala hakuna tiketi zilizoanzwa kuuzwa, hali inayoweza kuwa ni ‘kibano’ kwa mashabiki wa Yanga wanaoanza safari kesho kuwahi pambano hilo litakalopigwa Jumamosi kabla ya timu hizo kurudiana wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
.
Hata hivyo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Julius Karangwa amesema kuwa mechi ni ya Al Merrikh ambao ndio wenye uamuzi wa mambo mengi kwa sasa, lakini anachojua tiketi zitaanza kuuzwa wiki hii kwa njia ya mtandao.
 
ReKODI YA KIPEKEE
.
02—Kyle Walker (miaka 33 na siku 104) ni mchezaji wa pili mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao lake la kwanza kwa timu ya taifa ya England baada ya Jimmy Moore dhidi ya Sweden, Mei 1923 (miaka 34 na siku 10).

 
Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino ameingiwa na hofu baada ya wachezaji wake muhimu kupata majeraha na atawakosa katika mechi ijayo ya ligi dhidi ya Bournemouth.
.
Taarifa imeripotiwa kwamba staa mpya aliyesajiliwa, Romeo Lavia aliumia kifundo cha mguu wakati wa mazoezi wiki iliyopita huku Carney Chukwuemeka naye akipata majeraha.
.
Lavia hakujumuishwa kwenye kikosi tangu aliposajiliwa kwa Pauni 58 milioni kutoka Southampton ikidaiwa kwamba bado hakuwa fiti asilimia 100. Pochettino aliweka wazi kwamba kiungo huyo atakuwa fiti baada ya mechi za kimataifa lakini sasa kutokana majeraha aliyopata huenda akaongezewa muda zaidi.“
.
Wakati huo huo, Pochettino ame-pata pigo jingine baada ya nyota wake mwingine Chukwuemeka kuumia na huenda akawa nje ya dimba kwa muda mrefu. Kwa mujibu taarifa, Chukwuemeka atakuwa nje kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham. Kiungo huyo alitarajiwa kurejea wikiendi ijayo lakini sasa mambo yamekuwa tofauti.
 
Kiungo mpya wa Yanga Max Nzengeli ametajwa kama mchezaji bora wa mwezi Agosti akihusika kwenye magoli 3 kati ya 10 yaliyofungwa na Yanga kwenye mechi hizo .

Max amecheza dakika 107 katika dakika hizo ameshinda mabao mawili na kutoa assist moja !
 
Bodi ya Ligi Kuu [TPBL] imetangaza ratiba ya mechi tatu za mzunguko wa tatu ambazo awali zilikuwa hazijapangiwa tarehe.

YANGA V/s NAMUNGO FC-Septemba 20, saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

SIMBA V/s COASTAL UNION, Septemba 21, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Uhuru, Dar

AZAM FC V/s SINGIDA FG, Septemba 21, saa 1:00 usiku, Uwanja w Azam Complex, Chamazi.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imeeleza kuwa, kufanyika kwa mechi hizo kutategemea uthibitisho wa uwepo wa mechi za kuwania kufuzu CHAN ambapo CAF bado haijatangwza tarehe zake.
 
TETESI |

Dirisha la usajili limefungwa lakini Klabu zimeendelea na mipango ya kuboresha vikosi kwa madili ya nyota yaliyoshindikana kwenye dirisha lililofungwa hivi juzi.

Real Madrid wamepanga kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappé mapema mwezi Januari .

Matajiri hao wa LaLiga wamempa mchezaji huyo kipaumbele pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa tena.

Hata hivyo Plan B ya Madrid endapo watashindwa kufikia makubaliano kamili ya kumsajili watatafuta mbadala wake upande mwingine na hadi sasa machaguo yaliyopo ni Washambuliaji wa Manchester City Erling Haaland na Julian Álvarez.

Credit to ESPN
 
Al Ittihad ya Saudi Arabia wanatarajia kutuma ofa mpya ya kumsajili Mohamed Salah kutoka Liverpool wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari .

Wakati dirisha la usajili linafunguliwa maafisa wa Saudi Arabia waliidhinisha mpango wao wa kumsajili Mohammed Salah kama kipaumbele cha uhamisho pamoja na kiungo wa Juventus Paul Pogba

Al Ittihad waliandaa dau la pauni milioni 150 na juzi Mkurugenzi wa Saudi Pro League Michael Emenalo alikiri kwamba dirisha la usajili bado liko wazi ili kuweka msukumo wa kujaribu kumsajili Salah ila mpango umefeli nafasi nyingine ni mwezi Januari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…