Makapuku Forum

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Libya limetangaza kutokea kwa vifo vya watu 200 baada ya kimbunga ‘Daniel’ kuikumba nchi hiyo.

Hata hivyo, mashirika mbalimbali ya tathmini yanadai huenda vifo vilivyotokea vikafika zaidi ya 2,000.

Kimbunga na dhoruba hiyo kilianza siku ya Jumapili, na kusababisha mamlaka kutangaza hali ya hatari iliyokithiri.

Wanajeshi saba wa jeshi la Libya wametoweka wakati wa juhudi za uokoaji zinazoendelea. Maafisa mashariki mwa Libya wameweka amri ya kutotoka nje, huku shule na maduka yakiamriwa kufungwa.

Miji ya iliyoathiriwa zaidi na kimbunga hiko ni pamoja na; mashariki ya Benghazi, Sousse, Derna na Al-Marj.

Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vifo, Shirika la Msalaba Mwekundu la Libya lilitoa taarifa na kusema kuwa takriban nyumba 150 zimeharibiwa.

Mkuu wa mtandao wa misaada ya kibinadamu wa ‘Red Crescent’ amesema takriban vifo 150 vimetokea Derna pekee, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Video ambazo hazijathibitishwa za dhoruba hiyo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni, ikiwa ni pamoja na klipu inayoonyesha mafuriko yakisomba mtu. Picha zingine zinaonyesha madereva wakiwa wamekwama kwenye juu ya magari yao.
 
Dereva mmoja wa bodaboda amefariki baada ya kugongwa na Basi la ‘mwendokasi’ kwenye mataa ya kuelekea Lumumba katikati ya kituo cha mwendokasi cha Fire na DIT Jijini Dar es salaam.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ambao watatoa taarifa kamili ya tukio hili hapo baadaye, wamethibitisha kifo cha Dereva huyo ambaye imeelezwa kuwa aliingia kwenye barabara hiyo maalum ya Mabasi hayo.
 
Nahodha wa Tottenham Hotspurs Heung Min-Son ambaye ni Raia wa Korea Kusini amemuomba radhi Shabiki aliyeomba kupiga nae picha (Selfie) kwa kukataa kuishika simu ya Shabiki huyo kutokana na kuwa ni iPhone kwasababu ya mkataba wake wa Ubalozi na Samsung kumbana kufanya hivyo.

Son ambaye ameingia mkataba wa Ubalozi na Samsung majira ya kiangazi haruhusiwi kushika kifaa chochote ambacho ni bidhaa shindani na kampuni ya Samsung ila anaruhusiwa kupiga picha (Selfie) na Shabiki akiwa na simu ya kampuni nyingine nje ya Samsung pasipo yeye kuishika simu hiyo kama alivyoombwa na Shabiki huyo aliyekuwa kashika jezi ya Son ya Spurs.

Baada ya tukio hilo Son baadae alipiga picha (selfie) na Shabiki huyo kwa Son kushika simu nyingine ya Shabiki huyo aina ya Samsung na kisha Son kukubali kuishika na kupiga nae picha.
 
Ubora waliouonyesha Moses Phiri na Luis Miquissone katika kipindi hiki cha mapumziko kwenye mechi tatu za kirafiki ni kati ya sababu zinazompa jeuri kocha Robertinho na kuanza kupiga hesabu za kuwapa mechi dhidi ya Dyanamos.
.
Washambuliaji hao hawakuwa kwenye kiwango bora mwanzoni mwa msimu kwani Phiri alikuwa ametoka kuuguza majeraha huku Luis akikosa uti-mamu wa mchezo (match fitness) kutokana na kukaa muda mwingi bila kucheza lakini sasa wamejipata.
.
Nafasi yao kuachiwa mechi dhidi ya Dyanamos inazidi kuwa kubwa kwani Simba ipo nusu nusu, kukosa huduma ya mshambuliaji wake hatari wa kikosi cha kwanza Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’, aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa msimu uliopita akitupia mabao 17, kutokana na kubanwa na ratiba ya timu ya taifa lake.
.
Saido yupo nchini Cameroon na timu yake ya taifa (Burundi), na leo usiku watakuwa wakicheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2023) dhidi ya Cameroon na baada ya hapo ataanza utaratibu wa kujiunga na timu.
.
Hata hivyo, huenda akakwama kujiunga na timu ndani ya muda tarajiwa jambo ambalo kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amelishtukia na sasa anatafuta mchezaji atakayeziba pengo la Saido kati ya Phiri na Luis.
.
“Simba ina wachezaji wengi, Luis na Phiri ni miongoni mwao na uzuri wanaweza kucheza maeneo tofauti uwanjani. Nafurahi wapo kwenye kiwango bora na nipo tayari kuwatumia kwa mechi zijazo,” alisema Robertinho
 
Madereva Bodaboda wengi ni wapumbavu sana
Bila Ustaarabu wa madereva wa mwendokasi,Bodaboda wengi sana wangekuwa wamekufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…