Makapuku Forum

Real Madrid imepanga kuanza mazungumzo na Bayern Munich ili kuipata huduma ya beki wa timu hiyo, Alphonso Davies, 22, kwenye dirisha lijalo. Madrid inataka huduma ya beki huyo kwa sababu inaamini ataenda kuwa tiba sahihi ya tatizo la beki wa kushoto.
.
Beki huyu kisiki wa Timu ya Taifa ya Canada [emoji1063] licha ya kupewa ofa ya kusaini mkataba mpya na Bayern alikataa kufanya hivyo jambo linalotoa ishara kwamba anafikiria kuondoka.
.
Hata hivyo, Madrid haijahusika hata kidogo kwenye suala la staa huyo kugoma kusaini mkataba mpya na Munich bado haijakata tamaa ya kumsainisha.
.
Davies ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Bayern na amekuwa akisifika kwa uwezo wake ambao umefanya apewe jina la utani la pikipiki.
 
@luambano77 ameuliza swali, kwa uwekezaji uliofanywa kwenye klabu za Simba na Yanga, kuna mchezaji ambaye anapokea mshahara wa Tsh. 1,000,000 [milioni moja]?

Mkongwe @amrikiembatz akasema kwa sasa Simba na Yanga mshahara wa Tsh. 1 milioni labda kwa mchezaji ambaye amepandishwa kutoka timu za vijana lakini anaesajiliwa kutoka sehemu nyingine anachukua zaidi ya hapo.

@jr_farhanjr amesema mchezaji anaechukua mshahara mdogo Simba na Yanga pengine ni kuanzia Tsh. 2,500,000 [milioni mbili na laki tano] hapo bado posho n.k

Luambano akamaliza kwa kusema, kama kuna mchezaji wa Simba au Yanga analipwa Tsh. 1,000,000 [milioni moja] basi anapaswa kujitathmini. Kwa sababu hata timu za kati zinalipa hadi Tsh. 1,500,000 na kuendelea.

Kwa jinsi Simba na Yanga zilivyofanya uwekezaji ni sawa mchezaji kulipwa mshahara Tsh. 1,000,000 kwa mwezi________??

Note ! waliokwenye picha hawana uhusiano na hayo malipo
 
Nilipokuwa Algeria kwa ajili ya mechi ya Algeria vs Tanzania, niliwauliza mashabiki kadhaa kuhusiana na ushiriki wa klabu zetu kwenye mashindano ya CAF [Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho].

Msimu uliopita Yanga ilicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya USM Alger ya Algeria, Simba ilicheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

Waliniambia kuwa, klabu za Algeria hazitamani tena kukutana na klabu za Tanzania, lakini zamani walikuwa hadi wanatengeneza mazingira ya kupangwa na klabu za Tanzania.

Sasa hivi klabu za Tanzania zimekuwa sio salama tena kwao kuja kupita na kwenda hatua inayofata!

- Alex Luambano | #HiliGame @cloudsfmtz
 
Winga wa Manchester United Jadon Sancho anatarajia kuondoka Old Trafford dirisha la mwezi Januari, hii ni baada ya kutokuwepo kwa uhakika wa namba na maelewano kutokuwa mazuri na Ten Hag

Hivi karibuni mchezaji huyo alitumia mitandao ya kijamii kupinga maoni yaliyotolewa na kocha Erik ten Hag, ambaye alisema Sancho hapati nafasi kwa sababu hafanyi vizuri mazoezini.

Vyanzo vimeripoti kwamba wawili hao walikuwa na mazungumzo huko Carrington Jumatatu,huku ripoti ya Jarida la Star inasema mazungumzo hayo yalienda vibaya na uhusiano kati ya wawili hao sasa umevunjika kabisa

ESPN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…