Makapuku Forum

Kampuni ya Apple, imezindua toleo jipya la simu ya iPhone 15, ambalo linahusisha aina nne za toleo hilo ambazo ni iPhone 15, iPhone 15 Plus, iPhone 15 Pro na iPhone 15 Pro Max.

Uzinduzi huo umefanyika mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo mjini Cupertino, Jimbo la California, nchini Marekani, na kurushwa mbashara kwenye tovuti ya kampuni hiyo, saa 2:00 usiku (saa za Afrika mashariki).

kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu hizo zitauzwa bei ya kuanzia na Sh2,001,965 (iPhone 15), huku iPhone 15 Plus ikuzwa kuanzia Sh2,503,083.

Simu hizi zinakuja na rangi ya tano tofauti, ambazo ni pamoja na nyeupe, nyeusi, nyekundu, kijani na njano.

kwa upande mwingine, kampuni ya Apple, pia imetangaza uboreshaji wa camera kwa kwa simu hizo, maboresho ambayo yanajuimuisha uwezo wa picha za 'automatic' ambapo imeelezwa kuwa zitaweza kutambua wakati picha inapigwa kwa mtu mmoja, na kwamba kamera hiyo, pia ina ubora wa hali ya juu kunasa picha za mnato.

Katika uzinduzi huo ambao kampuni hiyo imeliita ‘Wonderlust,’ (ikimaanisha tukio lenye kustajabisha),
iPhone 15 inakuja na matoleo hayo manne, huku kati yake, mawili ni yenye yenye ‘skrini’ za inchi 6.1, na yaliosalia yana ukubwa was skrini ya inchi 6.7.

Mabadiliko mengine katika matoleo hayo mapya ni uwezo wa betri, mfumo wa camera na mwonekano wake, huku kwa mara ya kwanza, kampuni hiyo ikitambulisha chaja mpya za USB-C. Huku ikielezwa kuwa mabadiliko hayo yanalefanya mfumo wa kuchaji simu hizo kuwa rahisi.

Awali kampuni hiyo ilifanya mabadiliko ya kuchajisha katika bidhaa zake nyingine, lakini uzinduzi huu sana umeelekeza mabadiliko katika simu za kampuni hiyo, ambayo kimsingi ni takwa la kisheria baada ya Umoja wa Ulaya (EU) kupitisha sheria mpya, inayotaka vifaa vyote vya kielectroniki kutumia chaja hizo.
 
Mwenyekiti wa Klabu ya Watanzania waishio Nje ya Nchi (Diaspora Club), Kevin Nyamori amesema Wapiga kura hawapati nafasi ya kuwajua vizuri wagombea kwani muda wa kutangaza nia unaotolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC) ni mfupi kwani hauzidi miezi miwili.

"Mtu akitangaza leo kuwa ana nia ya kugombea Urais mwaka 2025 itamuathiri vipi Rais aliye madarakani?” Amehoji na kuongeza;

“Kukiwa na uwezo wa kufanya hivi itasaidia vyombo vya usalama na vyombo vya habari kumchunguza huyu mtu na kumwanika. Kama atakuwa hana mabaya, basi itakuwa ni sifa kwake. Kama atakuwa ana mabaya, basi atajitathmini sababu ya muda mrefu ambao Watu wamemfuatilia na kumwelewa vizuri.”

Nyamori ameyasema hayo leo Jumanne 12, 2023, katika kikao cha wadau wa demokrasia, kilichoandaliwa na Baraza la Vyama Vya Siasa nchini na kufunguliwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan.

 
Umekatisha ndoto yangu, nilikuwa naota nimeokota hela. Ndio nataka nianze kuzitumia unaniita ita kama unanidai figo!!
 
Kikuu lini sasa maeneo yako ya kujidai hii itakuwa tayari?
 
Wakati uharibifu wa mazingira ukiongezeka katika maeneo mbalimbali hasa ya vyanzo vya maji, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema ikiwa mvua za vuli zitachelewa kutakuwa na uhaba wa umeme kutokana na kupungua kwa maji.

Hata hivyo amesema kukua kwa teknolojia na ongezeko la viwanda kumeongeza matumizi ya umeme kwa kiasi kikubwa.
Katika Bwawa la Mtera, Kihansi na Kidatu kupungua kwa kina cha maji ni kati ya changamoto zilizojitokeza.

Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Chande amesema licha ya matumizi ya umeme kuwa makubwa na maji kupungua siku hadi siku Uzalishaji wa umeme bado upo vizuri.

"Vituo vyetu vinafanya kazi ila tusipopata mvua kutakuwa na upungufu wa umeme na kwa sasa tunaomba mvua zinazotegemewa zinyeshe haraka kwa sababu kama hazitanyesha vituo vyetu vinaendelea kudhusha uzalishaji na tutapata upungufu," amesema na kuongeza;

"Kunapokuwa na upungufu wa umeme unatokea mgao, hali hiyo inapotokea huwa tunawaambia wateja wetu kuwa upungu na ndio maana tunasema mvua zisipokuja mapema kutakuwa na upungufu wa umeme," amesema.

Amesema kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na kasi ya matumizi ya umeme kwa sababu ya ongezeko la uwekezaji kwenye viwanda.
 
Mkazi wa Kiwalani jijini hapa, Yusuph Abeid, amefariki dunia leo Jumanne Septemba 12, 2023 baada ya kuligonga basi la 'mwendokasi'.

Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo imehusisha basi la mwendokasi lilokuwa likitokea Kimara kwenda Kivukoni na bodaboda ambaye alikuwa akitokea barabara ya Fire katika makutano ya mataa ya Lumumba na Barabara ya Morogoro.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Christina Sunga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhiwa mmoja.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Kamanda Sunga amesema katika ajali hiyo majeruhi ni mmoja na alipelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu.

"Aliyefariki ni dereva wa bodaboda ambaye mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili," amesema Kamanda Sunga.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema taarifa kamili kuhusu ajali hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, huku akisema atakuja na ajenda maalumu kuhusu watu kukatisha kwenye barabara za mwendokasi.

 
Hivi Atoto utaendelea kusuka mabutu mpaka lini? Nimekutaftia mchumba umekataa kuolewa 😂 unang'ang'ania kulalia masofa hapa nyumbani.
Aaah wewe mwenyewe umeshindwa kutafuta mchumba wako unazurura tu kama kuku alopoteza vifaranga. Huyo wa kunitafutia mie unamtoa wapi? Wewe ndio uhame nyumbani, mama kasema tukunyime chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…