Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Kampuni ya Apple, imezindua toleo jipya la simu ya iPhone 15, ambalo linahusisha aina nne za toleo hilo ambazo ni iPhone 15, iPhone 15 Plus, iPhone 15 Pro na iPhone 15 Pro Max.
Uzinduzi huo umefanyika mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo mjini Cupertino, Jimbo la California, nchini Marekani, na kurushwa mbashara kwenye tovuti ya kampuni hiyo, saa 2:00 usiku (saa za Afrika mashariki).
kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu hizo zitauzwa bei ya kuanzia na Sh2,001,965 (iPhone 15), huku iPhone 15 Plus ikuzwa kuanzia Sh2,503,083.
Simu hizi zinakuja na rangi ya tano tofauti, ambazo ni pamoja na nyeupe, nyeusi, nyekundu, kijani na njano.
kwa upande mwingine, kampuni ya Apple, pia imetangaza uboreshaji wa camera kwa kwa simu hizo, maboresho ambayo yanajuimuisha uwezo wa picha za 'automatic' ambapo imeelezwa kuwa zitaweza kutambua wakati picha inapigwa kwa mtu mmoja, na kwamba kamera hiyo, pia ina ubora wa hali ya juu kunasa picha za mnato.
Katika uzinduzi huo ambao kampuni hiyo imeliita ‘Wonderlust,’ (ikimaanisha tukio lenye kustajabisha),
iPhone 15 inakuja na matoleo hayo manne, huku kati yake, mawili ni yenye yenye ‘skrini’ za inchi 6.1, na yaliosalia yana ukubwa was skrini ya inchi 6.7.
Mabadiliko mengine katika matoleo hayo mapya ni uwezo wa betri, mfumo wa camera na mwonekano wake, huku kwa mara ya kwanza, kampuni hiyo ikitambulisha chaja mpya za USB-C. Huku ikielezwa kuwa mabadiliko hayo yanalefanya mfumo wa kuchaji simu hizo kuwa rahisi.
Awali kampuni hiyo ilifanya mabadiliko ya kuchajisha katika bidhaa zake nyingine, lakini uzinduzi huu sana umeelekeza mabadiliko katika simu za kampuni hiyo, ambayo kimsingi ni takwa la kisheria baada ya Umoja wa Ulaya (EU) kupitisha sheria mpya, inayotaka vifaa vyote vya kielectroniki kutumia chaja hizo.