Makapuku Forum

[emoji599] MAMELODI HAWATAKI MAZOEA
.
12’—[emoji460]️ Ribeiro
37’—[emoji460]️ Ribeiro
41’—[emoji460]️ Nku
80’—[emoji460]️ Shalulile
.
FT: [emoji1060] BUMAMURU 0-4 MAMELODI [emoji1221]
 
[emoji2424] “Sio mchezo mwepesi ila naamini kwenye maeneo matatu kuzuia, kukaba na kushambulia hiyo ni mbinu nitakayoitumia katika mchezo huo wa kesho Jumamosi,”
.
.“Mashabiki wameonyesha ushirikiano na hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo, tuna wajibu wa kuwapa furaha kabla ya mechi ya nyumbani,” alisema kocha huyo raia wa Brazil.
.
Simba watamkosa winga Aubin Kramo ambaye aliyerejea kwenye majeruhi na kuwasha moto kwenye mechi tatu zilizopita za kirafiki. Mmoja wa watu wa benchi la ufundi, alidokeza ARENA express kuwa Kramo ameumia goti na atakosa mchezo huo na hata ule wa marudiano kwa vile atakuwa nje kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurudi uwanjani.
 
USM Alger imetwaa taji la CAF Super Cup ikiwachapa vigogo wa soka la Afrika mara 11, Al Ahly ya Misri kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa King Fahd nchini Saudi Arabia.

Fainali ya CAF Super Cup imewakutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly na wa Kombe la Shirikisho USM Alger kwa msimu uliopita.

USM Alger ilitwaa taji hilo la kwanza katika historia yao katika iwanja wao wa nyumbani licha ya kupoteza mchezo huo 1-0 dhidi ya Yanga kwa bao la ugenini baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

USM Alger inakuwa klabu ya pili nchini Algeria kushinda kombe hilo baada ya Wifak Setif mwaka 2015.

Vigogo Al Ahly iliwatoa mabingwa watetezi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca kwa ushindi wa mabao 3-2.
 
“Katika maisha tunatofautiana hivyo kupitia jukwaa hili itakuwa fursa nzuri kwa wanawake wanaoanza kukutana na wale ambao wameshaendelea.
Natamani wanawake wengi wazifikie fursa hizi hasa wale wenye uhitaji zaidi,” Mkuu wa mauzo na masoko taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), Salama Somboka.

 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema Ofisi yake imepokea zaidi ya Sh6.5 trilioni ambazo zimepelekwa moja kwa moja kwa Watanzania kutekeleza miradi mbalimbali huku akitangaza kiama kwa wale watakaowachezea fedha za miradi ya Tamisemi.

Waziri Mchengerwa amesema hayo leo Septemba 15, 2023 wakati akitoa salaam za wizara yake mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Manispaa ya Mtwara.

“Katika eneo la elimu tumepokea zaidi ya Sh2 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu nchi nzima na kugharamia elimu msingi bila malipo.

“Kwenye Afya msingi tumepokea zaidi ya Sh1.5 trilioni kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Hospitali za Halmashauri, ukarabati wa Hospitali kongwe, ujenzi wa vituo vya afya, ununuzi wa vifaa tiba, ujenzi wa zahanati pamoja na nyumba za watumishi,” alisema Mchengerwa.

Aidha kwenye eneo la miundombinu, Mchengerwa amesema kuwa zaidi ya Sh3 trilioni zimetumika kujenga, kuendeleza miundombinu ya barabara za vijijini na mijini ambapo katika kipindi cha mwaka huu wa fedha 2023, ujenzi wa daraja la Jangwani na uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi utatekelezwa.

‘Kwa fedha hizo ulizotoa sisi wasaidizi wako hatuna sababu ya kutokufanya kazi, kujituma kwa bidii na weledi wa hali ya juu sisi Kazi yetu kubwa ni kupanga namna bora ya kusimamia na kutekeleza ufanisi wa kazi zilizokusudiwa kukamilishwa kupitia fedha hizo’ alisema Mchengerwa

‘Ninakumbuka siku chache zilizopita wakati unatuapisha ulitusisitiza kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu kama ilivyo dira yako nami nilipoanza kazi nilishusha wizara yako kwa wananchi na kuwataka watendaji wote walio chini yangu kujishusha kwa wananchi na kutoka maofisini kwenda kuwahudumia wananchi na kutatua kero zao.

“Yeyote miongoni mwetu atakayewachezea wananchi wako kwa uvivu, uzembe au ubadhirifu wa fedha unazozitoa (Rais Samia Suluhu) kwa ajili ya huduma za wananchi, yule ambaye ni saizi yangu, nitashughlika naye kweli kweli,” amesema Mchengerwa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…