Makapuku Forum

Makapuku Forum

Afariki wakati akitengeneza hips...!

Huyu anaitwa Luana Andrade. Alikuwa mwanamitindo na msanii huko Brazil. Luana amefariki katika hospitali moja huko Brazil wakati akifanyiwa upasuaji wa kufyonza mafuta kwenye magoti maarufu kama Liposuction. Wakati anafanyiwa upasuaji huo mafuta yaliingia kwenye mishipa ya damu na kuziba mshipa mkubwa wa kwenye mapafu hali iliyopelekea kifo chake hata baada ya juhudi za madaktari kujaribu kuokoa maisha yake. Liposuction pamoja na upasuaji wa kurekebisha makalio maafuku kama Brazil But lift ni mojawapo ya operesheni za hatari zaidi. Ukiacha urembo upasuaji huo huwa hauna faida yoyote nyingine kiafya. Luana amefariki akiwa na umri wa miaka 29...!
 

Attachments

  • Screenshot_20231113_144322_Instagram Lite.jpg
    Screenshot_20231113_144322_Instagram Lite.jpg
    39.1 KB · Views: 2
Kaka yenu sio mtu yule alinipiga teke la tumbo mxxxxxieee muuaji yule sina ham nae nikamtukaanaaa, nikamfutilia mbali .. ila sasa hivi nammiss eti[emoji7][emoji7]
[emoji1787][emoji1787] Lazima ummiss my wiii ila nimefurahi mnoooo kukuona kipenzi
 
Wakongwe, hali zenu ndugu zangu.

Obe juzi nimepita mwembe YANGA nikamkuta shabiki wa simba, nikaona ajabu la 7 la temeke.

Lee vipi mzee wa costant K!?

Makiwendo Nimekumiss mzee mwenzangu.

Shunie akee, unajua vile nakukubali.

Mtaalam mtu chake, nakusalim kaka
Na watu wengine wote niliowasahau kwa bahati mbaya
Nakukubali sana make nimefurahi kuona uwepo wako
 
Kwahiyo mie kivuruge daaah!! Hizi njama za kunichafua nani anawalipa?

Nilikumiss kweli auntie, nikakumbuka ili nikupate nije huku.
Makiwendo aliniambia umeachwa na lile jambazi umelazwa mloganzila.
Mimi huyu wa kulazwa kabisa kisa mapenzi [emoji1787] niache kutafuta maokoto nilazwe na mapenzi woiiiii sio mimi
 
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha tope lote ambalo lipo chini ya daraja lililipo katika eneo la Jangwani linazibuliwa ili maji yaweze kupita badala ya kupindukia barabarani na kupelekea eneo hilo kutopitika ambapo amemuambia Meneja huyo kuwa hicho ni kipimo chake kama anatosha kubaki kwenye nafasi yake ama laah!.

Akiongea leo November 13,2023 baada ya kukagua eneo la Jangwani Jijini Dar es salaam, Bashungwa amesema “Nimemuelekeza Meneja wa TANROADS ambaye ameripoti hapa hana hata mwezi nimemwambia kipimo chake kama anatosha ni kuhakikisha tope chini ya daraja hili linazibuliwa ili maji yanapokuja kabla hayajapindukia barabarani, tope liwe limeondolewa maji yapite, labda yawe mengi sana ndio maji yanaweza kufunika juu ya daraja”

“Watanzania waiamini Serikali ina mipango ya muda mrefu ambayo ni ujenzi wa daraja jipya na mipango ya muda mfupi ikiwemo ya kuondoa tope na kusafisha mifereji, niipongeze Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa tahadhari mapema lakini mabadiliko ya tabianchi hakuna anayejua kesho yatakuja kwa njia zipi, tunawaahidi Watanzania tutaendelea kujipanga kama Serikali kujua tunakabiliana nayo vipi”

“Tumekuja hapa tumeona sehemu ya changamoto ni takataka kuziba chini ya daraja na wote Mimi na Waziri Mchengerwa tunawaelekeza Ma-RC na Ma- DC maeneo yote kusimamia na kutoa elimu kwa Watanzania kuzingatia usafi, ukiwa kwenye basi au chombo chochote cha usafiri au unatembea kwa miguu ukinywa maji ukamailiza sio ustaarabu kutupa tu chupa, inazalisha takataka ambazo zinaziba mifereji na madaraja”
Screenshot_20231113_145705_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema bangi ni dawa haramu inayoongozwa kwa kupatikana na kutumiwa zaidi nchini ikifuatiwa na heroin, mirungi na cocaine na hivi karibuni methamphetamine ambapo amesema dawa hizo zina madhara ya kiafya ikiwemo Mtu kuona visivyokuwepo na kupelekea kufanya vitu visivvyofaa kwenye Jamii.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Kamishna Msaidizi wa Kinga na Huduma za Jamii DCEA, Moza Makumbuli amesema bangi ni miongoni mwa vileta njozi ambapo humfanya Mtumiaji kuhisi, kuona au kusikia vitu visivyokuwepo au tofauti na uhalisia.

Makumbuli amewataka Watanzania kujiepusha na matumizi ya bangi na dawa nyingine za kulevya kwakuwa zina madhara huku akishangaa Watumiaji wa mitandao kutofurahia pale madhara ya bangi yanaposemwa au bangi ikikamatwa “Suala la bangi ni mtihani inaonekana wengi wanatumia, hata ukiangalia habari mfano ile ya biskuti za bangi mtandaoni comment za Watu ni kama vile wanaona bangi inachelewa kuhalalishwa, bangi haifai tujiepushe kutumia”
Screenshot_20231113_145945_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom