Makapuku Forum

makaveli10 kumbe ndio maana unaniona kivuruge😂😂😂
 
Shirika la Afya duniani (WHO) limeonya kuhusu hali "mbaya na ya hatari" katika kituo kikuu cha matibabu Gaza, Hospitali ya Al-Shifa, ambayo inakabiliwa ukosefu wa umeme na uhaba wa chakula na maji.

Mtendaji Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema "milio ya risasi na milipuko ya mara kwa mara katika eneo karibu na hospitali imezidisha hali ambayo tayari ni mbaya na kwasasa Al-Shifa haifanyi kazi kama hospitali tena," amesema.
Jeshi la Israel limekariri kuwa liko tayari kusaidia kuwahamisha watoto kadhaa wachanga walio katika mazingira magumu wanaohudumiwa hospitalini hapo.

Mkuu wa upasuaji wa Al-Shifa, Dk Marwan Abu Saada, ameiambia BBC kwamba mtoto wa tatu aliyezaliwa kabla ya wakati amefariki kwa sababu ya ukosefu wa nguvu.

Awali akizungumza na BBC hapo, Rais wa Israel, Isaac Herzog alirudia madai kwamba Hamas ina makao yake makuu chini ya Al-Shifa, hata hivyo Hamas inakanusha kutumia hospitali hiyo kwa madhumuni ya kijeshi.

Dk Abu Saada pia alielezea madai ya Israel kuwa ni ya uongo na ametoa mwaliko kwa vikosi vyake vya karibu kuja na kukagua jengo hilo.

 
[emoji599] JUST IN: MASTAA wa Simba wanaingia kambini leo kujiandaa na mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast [emoji1081] itakayopigwa Novemba 25, jijini Dar es Salaam, huku baadhi yao wakikiri wamesikia manung’uniko ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wakiahidi kuwapa raha.
.
Wakati mabosi wa Simba wakitarajia kumalizia vikao vyao vilivyoanza tangu wikiendi iliyopita, leo Jumatatu wanamalizia mikakati ya kumleta kocha mpya, msaidizi na kocha wa viungo baada ya Robertinho, Ounane Sellami na Corneille Hategekimana kufungashiwa virago, ARENA express tunajua Simba inataka kushusha wataalamu hao watatu kabla ya mechi ya Asec Mimosas.
 
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amekiangalia kikosi kilicho kwa sasa na nyota waliopo kisha akaandika ripoti na kuikabidhi kwa viongozi akitaka aletewe winga teleza mmoja na straika anayejua kufunga mabao kupitia dirisha dogo litakalofunguliwa mwezi ujao ili amalize kazi mapema.
.
Yanga kwa sasa inajiandaa kwa ajili ya mechi sita za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikitarajiwa kuanza ugenini dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, Novemba 24 kabla ya kuikaribisha Al Ahly. Lakini pamoja na kuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya mechi hizo dhidi ya klabu kutoka Afrika Kaskazini, kocha Gamondi tayari ameshawasilisha ripoti ya benchi la ufundi kwa mabosi wa klabu hiyo, ambayo inaelezwa imeanza kufanyiwa kabla hata kabla dirisha la usajili halijafunguliwa Disemba 16.
.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna uwezekano mkubwa straika wa sasa Hafiz Konkoni kupewa mkono wa kwaheri endapo Yanga itapata nyota wanayemfukuzia kwa sasa ambaye hata hivyo jina lake limefanywa siri. Yanga inataka kuachana na Hafiz kutokana na mshambuliaji huyo Mghana kushindwa kukata kiu ya benchi la ufundi la timu hiyo.
.
Gamondi ametaja pia kuhitaji winga mwenye kasi na kujua kupangua ukuta ambaye naye akitakiwa kuwazidi mawinga wote waliopo kikosini akiwamo Mahlatse Makudubela ‘Skudu’, Maxi Nzengeli, Jesus Moloko na Denis Nkane.
 
MWAMBA SANA
.
04—Ange Postecoglou ni meneja wa nne kwenye Ligi Kuu England, kushinda tuzo ya meneja bora wa mwezi kwa miezi mitatu mfululizo, baada ya Antonio Conte (3 - Octoba-Desemba 2016), Pep Guardiola (4 - Septemba -Desemba 2017) na Jurgen Klopp (3 - Novemba 2019-Januari 2020)

 
HATARI SANA
.
17—Harry Kane ni mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga kufunga mabao 17 katika mechi 11 za kwanza za msimu. Juzi Jumamosi alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Heidenheim mchezo wa ligi kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…