Makapuku Forum

Happy Birthday to you Auntie akee Makiwendo unapoongeza mwaka leo basi zikaongezeke heri zaidi, furaha na mafanikio katika maisha yako, Happy Birthday to you mama twins, me ninachojua nakupenda mnooooo [emoji3590][emoji3590] subiria muamala wa beer mbili tatu [emoji847]
 
Kinachoendelea Gaza: Hali inatisha, mbwa waanza kula maiti [emoji50]‍[emoji100]

Hali inazidi kuwa tete katika ukanda wa Gaza. Karibu hospitali zote zinazotegemewa katika eneo hilo hazifanyi kazi ama zinafanya kazi chini ya kiwango huku zikikabiliwa na uhaba wa mafuta na madawa. WHO imeonya kwamba hospitali ya Al Shifa huenda ikageuka kuwa makaburi. Madaktari katika hospitali hiyo wanadai miili ya marehemu imejaa nje na ndani ya hospitali hiyo na kwamba sasa mbwa wameanza kula viungo kutoka katika maiti hizo.

Maisha ya watoto njiti hatarini
WHO imesema kwamba watoto njiti waliokuwa kwenye mashine maalum za kuwapatia joto huenda wakapoteza maisha baada ya mashine hizo kuzimwa kutokana na kukosekana umeme. Jana picha za watoto njiti kutoka hospitali ya Al Shifa zimekuwa zikizunguka katika mitandao baada ya watoto hao kuondolewa ICU na kuwekwa wodi ya kawaida ya upasuaji. Israel imesema itasaidiana na madaktari katika hospitali hiyo kuwahamasisha watoto hao na kuwapeleka katika hospitali nyingine waendelee na matibabu.

Israel imekuwa ikiwatuhumu wapiganaji wa Hamas kwamba wamekuwa wakitumia hospitali pamoja na maeneo mengine ya umma kama maeneo ya kijeshi. Israel inasema makao makuu na ngome ya Hamas iko chini ya majengo ya hospitali ya Al Shifa. Jana jeshi la Israel limeonyeshwa maandaki yakiwa na silaha inayodai yako chini ya hospitali ya Rantis huko Gaza.

Israel ilianza kuushambulia mji wa Gaza baada ya tarehe 7 October wanamgambo wa Hamas kuvamia na kuuwa zaidi ya watu 1200 huko Israel. Mpaka sasa huko Gaza zaidi ya watu 11,200 wamepoteza maisha huku zaidi ya nusu wakiwa ni wanawake na watoto. Karibu nchi zote zimeshindwa kutoa shinikizo la pamoja la kuishinikiza Israel kuacha mashambulizi na Hamas kuachia mateka wakiwemo Watanzania wawili..!

[emoji991]Reuters
 
Afariki baada ya mahakama kuamuru mashine ya kupumulia izimwe...![emoji3062]

Indi Gregory amefariki akiwa na umri wa miezi 8 baada ya mahakama nchini Uingereza kuamuru mashine iliyokuwa ikimsaidia kupumua izimwe.

Indi alizaliwa na ugonjwa wa kurithi unaothiri jinsi chakula kinavyovunjwavunjwa ili kuzalisha nishati za kuuwezesha mwili kufanya kazi unaojulikana kwa kitaalam kama Mitochondrial Disease.

Kwa miezi kadhaa Indi alikuwa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi akipumua kwa mashine. Kwa muda mrefu hospital pamoja na wazazi wake wamekuwa wakivutana mahakamani, madaktari wakitaka mashine izimwe kwa sababu ubongo wake ulikuwa umeisha haribika hivyo asingeweza kuishi mwenyewe na maisha yake yangekuwa yameteso sana, huku wazazi wake wakitaka aendelee kupatiwa matibabu hospitalini.

Tarehe 10 Novemba, Mahakama ya Uingereza ilitoa hukumu na kuamuru mashine izimwe ili mtoto huyo afariki kwa madai kwamba ilikuwa ni njia ya kumsaidia asiishi maisha ya mateso.

Kabla ya hukumu hiyo, Serikali ya Italia ilimpatia mtoto huyo uraia wa Italia na kuahidi kwamba itagharimia matibabu yake yote katika hospitali ya watoto ya Bambino Gesu jijini Rome.

Hata hivyo mahakama ya Uingereza iliwakatalia wazazi wake kumwamwisha mtoto huyo na kumpeleka Italia.

Indi amefariki leo jioni akiwa amepakatwa na mama yake. Wazazi wake wamesema, "tumekasirishwa sana, tumevunjika moyo na tumefedhesha sana ,wamefanikiwa kuchukua mwili na utu wa mtoto wetu, lakini kamwe hawawezi kuuwa roho yake."
 
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
Oooooooh!!!!....Nitalia mimi(Unanijua)
Nakupenda zaidi kipenzi changu, Auntie wangu...Mungu atuweke kabisa...

Namba ya Mama Twins ni ile ile....Simu iite, miamala isome[emoji1787]

Love you.
 
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
Oooooooh!!!!....Nitalia mimi(Unanijua)
Nakupenda zaidi kipenzi changu, Auntie wangu...Mungu atuweke kabisa...

Namba ya Mama Twins ni ile ile....Simu iite, miamala isome[emoji1787]

Love you.
Enjoy your day auntie akeeee me nakupenda kinomaaaa [emoji7] usilie bwanah ebu tufurahi tu

[emoji1787] Simu kuita lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…