Makapuku Forum

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda @baba_keagan amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limepokea taarifa kuwa November 29,2023, saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni Askari wawili walimjeruhi kwa risasi Mtu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 Mlinzi binafsi wa Bar iitwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.

Jeshi la Polisi limesema tayari limewakamata Askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi”
 
Watu wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa kwa kuangukiwa na ukuta kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Chato Mkoani Geita.

Akitolea Ufafanuzi wa vifo hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mganza James Kongwa amesema chanzo kinatokana na kuangukiwa na ukuta ambapo Mama na Mtoto wa miaka 6 wamevunjika mguu pamoja na Mtoto kuumia sehemu za kichwani.

Akiongea mbele ya RC wa Geita, Martine Shigela, Afisa Mtendaji huyo amesema “Nyumba nyingi zimeanguka na mpaka sasa hivi, Mkuu wa Mkoa tuna Watu wawili wamepoteza maisha waliangukiwa na ukuta lakini pia tunao Majeruhi tuna Watu watatu ambao walijeruhiwa kutokana kuangukiwa na ukuta”

RC Shigela ametembelea na kuona hali halisi katika eneo hilo na kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia kwa Wafiwa pamoja na Majeruhi wote huku akiwataka Wananchi wote waliojenga katika maeneo yanayopita maji kuhama huku akimuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato kuhakikisha wote waliopatwa na majeraha wanapatiwa matibabu kwa uharaka zaidi bila malipo yoyote.
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limethibitisha kutokea kwa ajali ambapo basi la abiria lenye namba T178 DVB mali ya kampuni ya Ally’s Star Bus limepata ajali baada ya kugonga kichwa cha treni chenye namba V951 9006 kilichokuwa kikitokea Stesheni ya Aghondi kuelekea Manyoni katika makutano ya reli na barabara eneo la Manyoni mkoani Singida mapema leo na kusababisha vifo vya Watu 13.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk imesema “Ajali imehusisha basi la abiria lililokuwa likivuka njia ya reli eneo la Kilomita 587 Manyoni na kugonga kichwa cha treni na kusababisha Majeruhi 25 (Wanawake saba, Wanaume 18) pamoja naa vifo vya Watu 13 (Wanawake 6 na Wanaume 7).

“Shirika litaendelea kuutaarifu umma kadiri taarifa zinavyopatikana na linaendelea kuwasihi Madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria na alama za usalama katika njia ya reli na barabarani zilizowekwa ili kuepusha ajali, Shirika linatoa pole kwa Ndugu wa Marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi waweze kuendelea na shughuli za kujenga Taifa”
 
Hii kitu imenisikitisha sana ,ulikua ni uzembe wa hali ya juu
 
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) leo December 01, 2023 Jijini Dar es salaam imezindua rasmi APP ya Air Tanzania uzinduzi ambao pia umeambatana na uzinduzi wa kampeni ya “Appy Skies” itakayozawadia Wateja wake wanaotumia APP hiyo punguzo maalumu kwenye msimu huu wa sikukuu.

Mgeni rasmi katika tukio hilo, Mussa Mbura ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), amesema uzinduzi wa ‘Air Tanzania App’ ni muendelezo wa Air Tanzania katika matumizi ya teknolojia kwenye utoaji wa huduma zao ———> Air Tanzania APP itasaidia Wateja kupata huduma mbalimbali ikiwemo tiketi, mizigo na kupanga safari zao kupitia simu zao za mkononi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislausi Matindi amesema pamoja na kumiliki soko la anga nchini, Kampuni ya ATCL imeendelea kuboresha huduma zake ili kuongeza furaha kwa Wadau wake haswa Wasafiri na Watumiaji wa huduma za ndege “Punguzo hili ni la asilimia 5 hadi 10 ya bei halisi za tiketi, na ni kwa Wateja wanaokata tiketi zao kupitia “Air Tanzania App” tu ambalo linatolewa msimu huu wa sikukuu ambapo mauzo ya tiketi hizo za punguzo yameanza leo tarehe 1 Desemba, 2023 na ofa itaenda hadi tarehe 1 Januari, 2024”

“APP ya Air Tanzania inayopatikana kwenye App store na Playstore imekuja na urahisi na uharaka kuliko kawaida ambapo itamuwezesha Mteja kukata tiketi ya safari kwa urahisi, kupokea taarifa mbalimbali kuhusu safari, kufanya ukaguzi kabla ya safari, kuhakiki taarifa na kufanya mabadiliko popote alipo” ———imeeleza taarifa ya air Tanzania.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Ripoti ya Hali ya Uchumi Nchini imeonesha Pato la Mtanzania mmojammoja (GDP Per Capital Income) limeongezeka kutoka USD 399.5 (Tsh. 322,397) kwa thamani ya dola mwaka 2000 hadi kufikia USD 1,200 (Tsh. 2,880,000) Mwaka 2022.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam Mkumbo amesema “Tuelewane hapa tukisema hivi Watu wanasema mbona hiyo hela sina mfukoni, hesabu zake unazipata kwa kukusanya mapato ya Nchi nzima Watu wote milioni 61.7 mapato yao yote ambayo yanakaribia kufikia Tsh. Trilioni 141 unagawanya kwa idadi ya Watu ndio unapata pato la kila Mtanzania mmojammoja”
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam imemhukumu Mjasiriamali Bahati Malila kwenda jela miezi sita baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matano yakiwemo ya kughushi cheti cha uongo kikionesha kimetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Pia, imewaachia huru Mshtakiwa Godfey Mtonyi (30), baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitsha mashtaka dhidi yake ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate wa Mahakama hiyo, ambapo amesema Mashahidi 10 wa upande wa mashtak wameweza kuthibitsha bila kuacha shaka lolote kuwa Malila ametenda makosa yote matano.

Katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa inadaiwa kuwa Januari 14 mwaka 2020 Washtakiwa wakiwa wanafahamu, waliwasilisha nyaraka za uongo kwa Biao Lin Tang ambazo ni vyeti vya utoaji wa msaada vyenye tarehe Januari 13, mwaka 2020 vikionesha vimetolewa na Waziri Mkuu.
 
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema matokeo ya uchunguzi wA DNA (kuhakiki uhalali wa Watoto kwa Wazazi) ni ya uhakika na kwamba gharama ya uchunguzi ni Tsh. Laki moja kwa sampuli ya Mtu mmoja hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla ni Tsh. Laki 3 na malipo yote hufanyika Benki.

Akiongea leo November 30,2023 Jijini Dar es salaam Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dr. Fidelis Mafumiko amesema ili kupata huduma ya uchunguzi zipo taratibu za kuzifuata ambapo Mteja haendi moja kwa moja kupima DNA ila anawakilishwa na Taasisi zilizotajwa kisheria ili kumuombea Mteja huduma ya uchunguzi, Taasisi hizo ni Ustawi wa Jamii, Mawakili, Mahakama, Jeshi la Polisi kwa masuala yanayohusu jinai n.k.

“Taasisi hizo zitaandika barua ya maombi ya kupatiwa huduma kwa niaba ya Mteja husika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na baada ya kulipia gharama sampuli zitachukuliwa na uchunguzi utafanyika na majibu yatatolewa kwa Taasisi iliyoandika barua ambapo Mteja atapata majibu kupitia Taasisi hizo ndani ya wastani wa siku 27 za kazi (kutegemea na aina ya sampuli).
 
Mmoja wa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa kwenye zoezi la uokoaji kufuatia maporomoko ya tope yaliyosababishwa na mvua katika Mlima Hanang mkoani Manyara.

Maporomoko hayo yalianza jana Jumapili Desemba 3, 2023 ambapo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 63 na wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa baadhi ya miili ya waliofariki maporomoko ya matope jana Desemba 3,2023 Hanang' mkoani Manyara.

Hadi sasa idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko hayo vimefikia 63 huku wengine 116 kujeruhiwa.

 
Watu wanne wamefariki dunia na wengine watano wamelazwa kwa matibabu baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika Kijiji cha Buchurago Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ametangaza kutokea kwa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mjini Bukoba leo Desemba 4, 2023.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mlipuko wa ugonjwa huo umegundulika tangu Novemba 29, 2023 katika Kijiji cha Buchurago, Kata ya Bugorola Wilaya ya Misenyi.

"Mlipuko huo umebainika Novemba 29, 2023 katika kijiji cha Buchurago baada ya watu wawili kutoka nchi jirani ya Uganda kuingia kijijini hapo….hadi sasa, watu wanne wamefariki dunia na wengine watano wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kajunguti wilayani Misenyi,’’ amesema Mwassa.

 
“Kuna Jose Luis Miquissone. Sijui kimemtokea nini. Zamani katika mechi kama hii, Miquissone alitazamiwa kuwa mtu wa kuiteketeza Galaxy. Leo anaingia uwanjani dakika ya 70 na bado hakuna anachofanya. Alipokuja mwanzoni ilitajwa kwamba alikuwa ameongezeka kilo katika mwili wake.Miquissone wa sasa amerudi kuwa na umbo lile lile, lakini anashindwa hata kutuliza mpira uwanjani achilia mbali kukokota.
.
Imekuwa, ghafla sana na sasa tunajiuliza kama kweli ataweza kurudisha makali yake yaliyowahi kuifanya Al Ahly kutoa kiasi kikubwa cha pesa kupata huduma zake miaka michache iliyopita. Simba walilia arudi lakini hadi sasa hawaamini wanachokiona. Kama uongozi utaamua kuachana naye mwishoni mwa msimu sidhani kama kuna Mwanasimba ambaye atapigwa na butwaa.
.
Amekuwa miongoni mwa wageni mizigo katika klabu hii ambayo ilimtambulisha zaidi barani Afrika. Naanza pia kupatwa na wasiwasi na Jean Baleke. Ni kweli anaibeba Simba kwa kutupia mabao, lakini nje ya mabao hana mchango mkubwa uwanjani. Inabidi abadilike kama kweli anataka kuibeba Simba. Asisubiri mabao ya kugusa tu mpira uende wavuni.” — Mchambuzi Edo Kumwembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…