Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora usiku huu December 17,2023 Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kwenye suala la changamoto ya uhaba wa dola linalozikabili Nchi nyingi duniani, Tanzania ipo vizuri ukilinganisha na wengine na Serikali inaendelea kupambana ili kuhakikisha Tanzania haiendi chini kwenye uhaba kama Nchi nyingine.

“Suala la dola nataka niwape faraja pamoja na changamoto tulizonazo Tanzania tupo vizuri na tumewaacha wengine mbali kwenye ukanda wetu, angalau sisi tunamudu kama alivyosema Waziri ninapokwenda naambatana na Wafanyabiashara pamoja na kwamba Wafanyabiashara wanajilipia lakini dola zilezile zinatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) lakini tunakwenda wengi , angalau tumeongeza kiwango cha kutoa kwa siku “

“Ilivyokuwa crisis kali tulikuwa tunatoa dola laki 5 kwa Mtu kwa siku tukapandisha milioni 1, tukapandisha milioni 2 , we are far far better, kuna Majirani zetu leo hata dola laki 5 kwa Mtu kwa siku hakuna, hawana kwahiyo tuko vizuri”

“Na kwenye hili suluhisho tunaweza tukalipata humuhumu ndani, Serikali tumeanza kuchukua hatua ya kupunguza kwa kiasi kikubwa yale mambo tunayoagizia nje ni mpango wetu kuangalia njia zote za kupunguza gharama za uagiziaji ili tupunguze matumizi ya dola, pia tumeanza kujihusisha na mambo yatakayoleta dola harakaharaka na ndio maana mnasikia tumejihushisha sana na Sekta ya Kilimo hususani kinacholeta mazao harakaharaka ili tunavuna, tunauza na dola inaingia harakaharaka”

“Lakini nyinyi ni Mashahidi kwamba Sekta ya Utalii imekua sanasana sana na ile imetusaidia kuleta dola ndani ya Nchi kwahiyo tunachukua hatua na hali yetu sio mbaya sana pamoja na kwamba hampati jinsi mnavyotaka lakini Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba hatuendi chini kama walikofika wenzetu, imani yangu wenye viwanda mtatusaidia kupunguza uhaba wa dola mtakapozalisha na kuuza nje”
Screenshot_20231218_082326_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora usiku huu December 17,2023 Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia miezi ya katikati mwakani 2024 malalamiko kuhusu umeme yatakuwa yamepungua kwakuwa vinu viwili vitawashwa katika Bwawa la Nyerere na kuongeza umeme kwenye gridi ya Taifa hivyo Nchi itakuwa na umeme wa kutosha.

“Itakapofika January mwakani tunaanza kuwasha kinu cha kwanza cha umeme pale kwenye Bwawa la Nyerere, jumla vinu vyote viko tisa, cha kwanza kitawaka January, cha pili hatutozidi April tutakuwa tumewasha kinu cha pili na vile viwili tukiwasha tutakuwa na umeme wa kutosha sana”

“Kwahiyo pamoja na jitihada nyingine za gesi, solar na mambo mengine lakini kwenye umeme wa maji ambao tunautegemea, nadhani katikati ya mwakani na ni malalamiko mengi (ya umeme) yatakuwa yamepungua, tutawasha vinu viwili tutaongeza kwenye gridi ya Taifa umeme mkubwa”
Screenshot_20231218_082430_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora usiku huu December 17,2023 Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kwenye suala la changamoto ya uhaba wa dola linalozikabili Nchi nyingi duniani, Tanzania ipo vizuri ukilinganisha na wengine na Serikali inaendelea kupambana ili kuhakikisha Tanzania haiendi chini kwenye uhaba kama Nchi nyingine.

“Suala la dola nataka niwape faraja pamoja na changamoto tulizonazo Tanzania tupo vizuri na tumewaacha wengine mbali kwenye ukanda wetu, angalau sisi tunamudu kama alivyosema Waziri ninapokwenda naambatana na Wafanyabiashara pamoja na kwamba Wafanyabiashara wanajilipia lakini dola zilezile zinatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) lakini tunakwenda wengi , angalau tumeongeza kiwango cha kutoa kwa siku “

“Ilivyokuwa crisis kali tulikuwa tunatoa dola laki 5 kwa Mtu kwa siku tukapandisha milioni 1, tukapandisha milioni 2 , we are far far better, kuna Majirani zetu leo hata dola laki 5 kwa Mtu kwa siku hakuna, hawana kwahiyo tuko vizuri”

“Na kwenye hili suluhisho tunaweza tukalipata humuhumu ndani, Serikali tumeanza kuchukua hatua ya kupunguza kwa kiasi kikubwa yale mambo tunayoagizia nje ni mpango wetu kuangalia njia zote za kupunguza gharama za uagiziaji ili tupunguze matumizi ya dola, pia tumeanza kujihusisha na mambo yatakayoleta dola harakaharaka na ndio maana mnasikia tumejihushisha sana na Sekta ya Kilimo hususani kinacholeta mazao harakaharaka ili tunavuna, tunauza na dola inaingia harakaharaka”

“Lakini nyinyi ni Mashahidi kwamba Sekta ya Utalii imekua sanasana sana na ile imetusaidia kuleta dola ndani ya Nchi kwahiyo tunachukua hatua na hali yetu sio mbaya sana pamoja na kwamba hampati jinsi mnavyotaka lakini Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba hatuendi chini kama walikofika wenzetu, imani yangu wenye viwanda mtatusaidia kupunguza uhaba wa dola mtakapozalisha na kuuza nje”
View attachment 2845652
Ss tena kila sehemu tuko vizuri[emoji847]
 
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), limemtangaza Sheikh Walid Omar kuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo baada ya uteuzi wa mtangulizi wake Sheikh Alhad Mussa Salum, kutenguliwa.

Februari 2023, Bakwata kupitia Baraza la Ulamaa lilitengua uteuzi wa Sheikh Alhad na kumteua Sheikh Walid Omar kukaimu nafasi hiyo.

Lakini leo Sheikh Walid ametangazwa rasmi na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Hamid Jongo katika maadhimisho ya miaka 55 ya kuzaliwa kwa baraza hilo.

Tukio hilo lilifanyika leo Jumapili Desemba 17, 2023 katika ukumbi wa Mfalme Mohamed VI uliopo katika ofisi za makao makuu ya Bakwata wilayani Kinondoni.
Screenshot_20231218_082719_Instagram.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema mchakato wa hadhi maalumu kwa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) utakamilika mwakani.

Amesema hadhi maalumu itaanza kutumika mwakani ambapo kupitia hadhi hiyo Watanzania wataanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya Tanzania.

“Tutatangaza hadhi maalumu na stahili mahususi kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wenye asili ya Tanzania ambao wana uraia wa nchi nyingine kuanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya nchi yao.
“Lakini pia na ustawi wao binafsi ambao unawaunganisha wao na nchi yao,” amesema Waziri Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Desemba 17, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo kuhusu utekelezaji wa Dipromasia ya Tanzania.

Katika kuhakikisha hilo, Waziri Makamba amesema kitafanyiwa mabadiliko kifungu cha sheria ya uhamiaji kinachohusu suala hilo katika Bunge lijalo.

Akizungumzia hilo, alipotafutwa na Mwananchi Digital, Adolph Makaya, Mtanzania aishie nchini Sweden amesema ni jambo la furaha kwakuwa wameanza kupeleka maombi muda mrefu kwaajili ya kuwekeza nchini.

Screenshot_20231218_082906_Instagram.jpg
 
Wakati mjadala ukiendelea wa uamuzi wa Mahakama Kuu kufuta uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema, dhidi ya waliokuwa wanachama wake 19 wa kuwafukuza uanachama, Halima Mdee ameonesha matumaini yake juu ya kumalizika kwa mgogoro huo.

Mdee aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), amesema wanachama wengi wa Chadema, wanatamani mgogoro huo umalizike lakini kuna wachache kwa maslahi yao hawatamani kuona hilo likitokea.

Mbunge huyo wa viti maalum alisema hayo jana jijini hapa, ikiwa ni siku takribani tatu tangu Mahakama hiyo kutoa uamuzi huo wa kutengua uamuzi wa Baraza Kuu na kuibua mjadala wa kipi kinaendelea baada ya hapo.

Screenshot_20231218_083014_Instagram.jpg
 
[emoji2788] “Hakuna timu isiyofungika, tuondoe mawazo hasi kichwani kwetu tutaingia uwanjani tukiwa kifua mbele na lengo likiwa ni kushinda. Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa nguvu timu yao naamini baada ya mechi tutafurahi kwa pamoja,” - Kocha Abdelhak Benchikha.
Screenshot_20231218_101005_Instagram.jpg
 
[emoji2788] “Sankara ndio chaguo letu namba moja tukimpata huyo tutakuwa tumepiga hatua kubwa ya usajili wetu, ni kijana mdogo ambaye analijua goli,” alisema bosi wa Yanga na kuongeza:
.
“Chaguo la pili ni yule Sowah (Jonathan) tunataka kumuona hapa pia atakavyocheza ugenini akitushawishi tutatafuta akili ya kumalizana naye, tunaweza hata kusajili washambuliaji wawili dirisha hili.”
Screenshot_20231218_101121_Instagram.jpg
 
[emoji187] “Niliamua kwenda kasi kujua kipi ambacho kiliwakimbiza Simba na Yanga hadi Zanzibar kwenda kuinasa saini ya kinda Shekhan Ibrahim Khamis. Nimetazama video zake. Kwa haraka haraka anaonekana ana kitu. Umbo kubwa, kasi, umiliki wa mpira na ana matumizi mazuri ya miguu yote miwili.
.
Hapa karibuni Zanzibar imepotea katika ramani ya soka. Haitoi wachezaji wengi mahiri kama ilivyokuwa zamani. Zamani Zanzibar ingeweza kutoa hadi wachezaji wanne wanaoanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania. Mastaa hawa walikuwa wanatokea Malindi, KMKM, Small Simba, Jamhuri na Mlandege. Msimu uliopita nilikuwa naifuatilia Ligi ya Zanzibar SIKUONA vipaji vya ajabu.
.
Baadaye akatokea Ibrahim Bacca ambaye sijui Yanga walimuona wapi. Na wiki iliyopita wakubwa wamekimbizana kwa Shekhan. Inatokea nadra kwa wakubwa kuvuta mchezaji moja kwa moja kutoka ligi ya Zanzibar ya leo. Vipaji ni bidhaa adimu Zanzibar ya siku hizi. Na sasa najiuliza kama Shekhan atakuwa Fei Toto mwingine katika soka letu au Geofrey Mwashiuya mwingine katika soka letu.” — Edo Kumwembe.
Screenshot_20231218_101226_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom