Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanamke wa Uingereza aitwaye Demi Agoglia (26) amefariki dunia siku chache baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza shepu (BBL) nchini Uturuki, Magazeti ya Uingereza yameripoti.

Demi ambaye alikua Mkazi kutoka Jiji la Manchester alipata mshtuko wa moyo saa chache kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nyumbani Uingereza ambapo Mume wake alimpatia huduma ya dharura ya CPR kabla ya kumpeleka Hospitalini lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

Inaelezwa kwamba kiwango cha vifo vinavyotokana na upasuaji wa kuongeza makalio (BBL) ni kifo kimoja kati ya kila Watu 3000 ambapo upasuaji huo wa BBL ndio upasuaji wenye kiwango cha juu zaidi cha vifo vilivyorekodiwa kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.

Upasuaji wa kuongeza makalio unakadiriwa kugharimu £3,500 (Tsh milioni 11.1) nchini Uturuki lakini hadi £10,000 (Tsh milioni 32) nchini Uingereza huku utafiti ukionesha kuwa ndio upasuaji hatarishi zaidi kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.
Screenshot_20240111_152438_InstaPro%20.jpg
 
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa msamaha kwa kuwaachia huru Wanafunzi 25 (Wafungwa) wanaotumikia adhabu zao katika Chuo cha Mafunzo Zanzibar (Gerezani) hii ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hii ni kawaida kwa Rais wa Zanzibar kutoa msamaha kwa baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo katika maadhimisho kama haya ambapo kati ya waliosamehewa, Wafungwa 15 ni wa Unguja na 10 wa Pemba.
Screenshot_20240111_152606_InstaPro%20.jpg
 
Matumizi holela ya dawa za kienyeji za kuongeza uchungu kwa wajawazito yanaweza kuwaweka hatarini hata kusababisha kifo cha mama na mtoto.

Baadhi ya wajawazito kutumia dawa za kienyeji kuongeza uchungu ni jambo la kawaida.

Hata hivyo, matumizi hayo yanawaweka wajawazito katika hatari ya kupasuka kizazi na hata kusababisha vifo vya mama na mtoto.

Watumiaji hao huamini dawa hizo zitawasaidia kutokaa muda mrefu hospitali kwa kuwa watajifungua mapema.

Pia, wapo wanaoamini kwenda hospitali pasipo kutumia dawa hizo watakaa muda mrefu, watatundikiwa dripu kuongeza uchungu au kuzaa kwa upasuaji.

Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi
(Imeandikwa na Devotha Kihwelo)
Screenshot_20240111_152720_InstaPro%20.jpg
 
Wakazi wa Mtaa wa Mbutu Mkwajuni, Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam wamejikuta wakitumia Sh4,000 kufuata sokoni fungu la dagaa la Sh1,000 kutokana na ubovu wa barabara.

Mkazi wa eneo hilo, Frank Ngunda amesema hayo leo Januari 11, 2024 alipokuwa akitoa malalamiko yao kuhusu ubovu wa barabara katika eneo lao.

Ngunda amesema kutokana na ubovu huo wa barabara, gharama za maisha zimeongezeka huku akitolea mfano wanavyolazimika kukodi bodaboda kwa Sh3,000 kwa ajili ya kufuata dagaa wa Sh1,000, hivyo wanajikuta wakitumia Sh4,000.

“Tunaiomba Serikali katika hili, ituangalie kwa jicho la huruma kututengenezea barabara kwa kuwa tumekuwa tukiteseka kwa muda mrefu,” amesema Mbunda.

Kwa upande wa Ipuli Sagula pia mkazi wa mtaa huo, amesema ubovu huo wa barabara umechangiwa pia na malori ya kubeba mchanga yanayopita hapo, hali iliyosababisha waifunge ili yasipite.

Screenshot_20240111_152824_InstaPro%20.jpg
 
Mgambo wa Al-Shabaab Somalia, wamemuua mtu mmoja na kuwashikilia wengine sita baada ya helikopta ya Umoja wa Mataifa (UN), kutua kwa dharura eneo linalodhibitiwa na kundi hilo.

Shirika la Habari la DW, limeripoti kuwa maofisa wa Somalia wamesema, helikopta hiyo ililazimika kutua kwa dharura baada ya kupata hitilafu.

Waziri wa masuala ya ndani Jimbo la Galmudug, Mohamed Abdi Aden Gaboobe amesema helkopita hiyo ilipata hitilafu ya injini na kutua karibu na Kijiji cha Xindheere.
Watu tisa wanaripotiwa walikuwa ndani ya helikopta wakati wa tukio hilo, wanane kati yao ni raia wa kigeni.

Abiria wawili walifanikiwa kutoroka na mmoja aliuawa kwa risasi wakati akijaribu

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, taarifa ya ndani ya UN imesema helikopta hiyo ilianguka takriban kilomita 70 Kusini Mashariki mwa Dhusamareb.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, waliokuwamo ndani ya helikopta ni maofisa wa kukodishwa na sio wafanyakazi wa UN.

Screenshot_20240111_152928_InstaPro%20.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Palestina, Mahmud Abbas.

Shirika la Habari la DW limeripoti kuwa katika mazungumzo hayo, Rais huyo amemueleza Manadiplomasia huyo wa Marekani, kuwa anakusudia kufanya mageuzi katika uongozi ili kuunganisha tena Gaza iliyokumbwa na vita na Ukingo wa Magharibi.

Blinken ameasema hayo baada ya kukutana na kiongozi huyo, katika ziara yake ya nne ya Mashariki ya Kati yenye lengo la kuzuia vita vya Israel na Hamas kusambaa zaidi.

Shirika la Habari la Palestina la Wafa, limeripoti kwamba, Rais Abbas alimweleza Blinken haja ya kuzuia "uchokozi" wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na Ukingo wa Magharibi.

Blinken amesisistiza kuwa Washington inaunga mkono hatua za wazi kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina, ambalo ni lengo la muda mrefu linalopingwa na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Blinken ameendelea na ziara yake huko Bahrain.

Screenshot_20240111_153109_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom