Mtoto wa miezi mitano, Leornad Kabilu, mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa wilayani Geita amefariki dunia baada ya kupigwa na baba yake sehemu mbalimbali mwilini kwa kutumia mkanda na kiatu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea jana Alhamisi Januari 11,2024 saa saba usiku wakati wakiwa wamelala na chanzo cha tukio hilo kinadaiwa ni ugomvi wa kifamilia.
Kamanda Jongo amesema mtuhumiwa, Kabilu Mayege (20) baada ya kutenda kosa hilo ametoroka na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
Akizungumza mama wa mtoto huyo, Riziki Leornad amesema siku ya tukio mumewe alitoka kuangalia mpira na akataka amuandalie chakula wakati mtoto amelala na wakati anakula mtoto alianza kulia na mama akabaki akitoa vyombo mezani na mumewe kupanda kitandani alikokuwa amelala mtoto.
View attachment 2869712