Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo January 13, 2024.
Screenshot_20240113_060011_Chrome.jpg
 
Abiria 1,200 waliokuwa wakisafiri kwa treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya bara wamekwama katika stesheni ya Morogoro kwa saa 18 baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kuharibu njia ya reli kipande cha Morogoro - Kilosa mkoani hapa.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Januari 12, 2024 katika stesheni ya Morogoro, Kaimu Stesheni Masta Morogoro, Herman Ngonyani amesema kipande cha njia ya reli Morogoro hadi Kilosa kimehabiriwa na mvua zilizonyesha juzi usiku na njia ya Mpwawa na Chamwino imeharibiwa na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo.

Kutokana na mkwamo huo, Ngonyani amesema wameandaa usafiri mwingine wa mabasi 48 yatakayoanza safari jioni ya leo.

Screenshot_20240113_061354_InstaPro%20.jpg
 
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Mlima Ngaile amefariki dunia leo asubuhi Ijumaa Januari 12, 2024 baada ya kudondoka wakati akishiriki mbio zilizoandaliwa na Wiloles Foundation Marathon.

Baada ya kudondoka inaelezwa akiishiwa pumzi akiwa eneo la Matalawe Manispaa ya Songea na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso) kwa matibabu, lakini alifikwa na mauti.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema daktari amethibitisha kifo hicho na mwili wa meneja huyo umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri taratibu za mazishi kuendelea kwa kushirikiana na Tanroads Makao Makuu.

Akisimulia jinsi walivyoshiriki mbio hizo, mkuu huyo wa wilaya (DC), amesema leo asubuhi kulikuwa na mbio za hisani za kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto wachanga katika Hospitali ya Rufaa ya Songea.

Screenshot_20240113_061551_InstaPro%20.jpg
 
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) kupitia vikundi vya Benki ya Hifadhi ya Jamii (Cocoba), imegawa mizinga 300 kwa wilaya tatu za Itilima, Meatu, Busega itakayosaidia kuinua kipato na kupambana na kupambana na tembo waharibifu.

Wilaya hizo tatu ni kati ya wilaya zinazokabiliwa na changamoto ya tembo kwa baadhi ya maeneo yake kuingia shambani na katika makazi ya watu na kufanya uharibifu.

Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo, tembo wamekuwa wakiingia katika mashamba na makazi ya watu kutokana na shughuli za kibinadamu katika njia zao za asili (corridor), huku idadi ya tembo ikiongezeka kwa asilimia 30.

Taarifa kutoka kwa wananchi wa vijiji hivyo na maofisa wa Serikali zinaeleza kuwa sauti ya nyuki huwakimbiza tembo na hawathubutu kusogelea maeneo hayo, hivyo miradi ya ufugaji nyuki inawapa suluhusho la tembo hao.

Screenshot_20240113_061658_InstaPro%20.jpg
 
Kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ametabiriwa makubwa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazoanza rasmi kesho Jumamosi huko Ivory Coast, ikidaiwa zitambeba nyota huyo aliyepo kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
.
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema : “Namuona Fei akifika mbali, hasa akizitumia vyema mechi za Afcon kuna timu zitaanza kumtafuta, kule mataifa mbalimbali yanakutana, hivyo kuna viongozi wengine wa timu wanakwenda kwa lengo la kuangalia wachezaji ambao baadaye watawasajili.”
.
“Fei ana kipaji sio kwamba katengenezwa ukubwani, umri pia unamruhusu, ni kujitambua zaidi na kuwa na ndoto za kucheza timu kubwa zaidi na isiwe hapa Tanzania sasa, uzuri wa Azam hawana choyo pale atakapopata timu nje ya nchi.”
Screenshot_20240113_061953_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom