Kwa hali ilivyo sasa pale nchini Kongo,
Félix Tshisekedi anamuita Joseph Kabila MHAINI, na yuko tayari kumpiga KITANZI na kumnyonga hadharani.
Kwa upande wa Joseph Kabila, na yeye pia anamuita Félix Tshisekedi MHAINI.
Na kwa sasa, analiandaa jeshi lake kuelekea jijini Kinshasa kwa lengo la kumng’oa Tshisekedi madarakani.
Njia ileile ambayo baba yake, Laurent-Désiré Kabila, aliitumia kumpindua Mobutu Sese Seko mwaka 1997,
Na yeye anataka kuitumia dhidi ya dereva TAXI na muuza PIZZA.
Kwa hiyo, TIMU yote ya Tshisekedi inamtambua Joseph Kabila kama MUASI, na kwa upande wa pili,
Kambi ya Kabila nayo inamchukulia Félix Tshisekedi kama MUASI.
Hapo sasa, ndo utata wa kisiasa na utawala wa taifa la Kongo unapozidi kuwa PASUA KICHWA.
Kila upande unamnyooshea kidole mwenzake kwa usaliti na kutaka kumzika FUTI SITA.
Usilolijua ni kwamba, kabla ya Joseph Kabila kuungana na M-23,
Hao jamaa walikuwa wanapiga Mishe zao nyingi katika upande wa Mashariki mwa Kongo.
Lakini baada tu ya Kabila kuwa Kiongozi wao Mkuu, jamaa ameanza kuyaunganisha makundi mbalimbali ya waasi,
Kwa lengo la kuunganisha nguvu ili waanze mashambulizi ya kuelekea Ikulu pale Kinshasa na kumtoa Félix Tshisekedi.
Ndiyo maana, siku chache zilizopita, Corneille Nangaa, Makamu wa Joseph Kabila, alitoka hadharani na kuelezea zaidi mipango yao.
Jamaa alisema kwamba eti, kwasasa wana mpango wa kuvuka mipaka na kuanza safari ya kuelekea Kinshasa kuichukua nchi.
Yaani ukisikia MBOMBO NGAFU, ndiyo hii sasa!
Kila mtu amekuwa kambale katika upande anao-uongoza.
Kama unataka kwenda kwa buriani, jifanye kama unakosea kupita kwenye mitaa ya hao jamaa. Utabaeleza benyewe kwa vitendo.
Suala la Kongo jamani ni zaidi ya MUVI, mambo yako DIPU sana.
Upande wa Kabila kuna Bwana Tolu na Mzee Kaguta, watu ambao wanaijua Kongo kwa vitendo, kwa maana wote ni WAJEDA.
Kwa upande wa Tshisekedi, yeye mtaji wake ni kutoa madini kwa Israel na Marekani ili apewe sapoti ya ulinzi na usalama.
Kwahiyo hapo inakwenda kupigwa ndondo kati ya Watoto wa Mbwa Vs Watoto wa Kishua.
Je, unadhani Felix Tshisekedi “Dereva TAXI” wa zamani, atatoboa kweli mbele ya hao WAJEDA?