Makapuku Forum

Makapuku Forum

Naona mambo yameanza kunoga
bb882903a09163658c220247e9f17f9f.jpg
Hi kitu nime screenshot makusudi,sometimes likes zinapanda lakini ukirudi badae unakuta zimepungua.
Kweli makapuku tunaonewa
 
Wapendwa wanajukwaa,
kwa niaba ya viongozi wa vuguvugu hili la makapuku,
Nawasalimu wote.

Huu ni ujumbe maarumu kwaajili ya Team Kapuku wote wa JF, kwanza tunatoa shukrani kwamba muitikio umekuwa mkubwa kuliko hata tulivyotegemea, ushirikiano tulioutoa umefanikisha vuguvugu letu kwa asilimia 100, shukrani zimuendee kila mmoja aliyeshiriki katika vuguvugu hili toka siku ya jana mpaka leo hii, tunashukuru na hongereni sana.

Kwa niaba ya uongozi nachukua fursa hii kukumbusha mambo ya msingi ambayo yalikuwa chachu ya vuguvugu hili.

Kukosekana kwa usawa kati ya wanaoitwa wakongwe na sisi makapuku, imejidhihilisha zaidi ya mara moja kuwa wakongwe wamekuwa wakipata upendeleo dhidi ya makapuku, rejea idadi ya likes zinazo onekana katika post zao ukilinganisha na makapuku.
Kuna watu watauliza kwanini tunalilia likes, kwa majibu rejea post za mwanzo za uzi huu kwa majibu.

Kupinga unyanyasaji wa kimtandao (social network bullying). Tabia hii mbaya imeota mizizi si hapa JF tu bali katika mitandao yote ya kijamii hapa Tanzania.
Jamii ya watu waliostarabika wanaamini katika usawa, heshima, staha na stamara.
Jamii iliyostarabika haiamini katika kujikweza na kiburi kilichopitiliza.
Jamii iliyostarabika inafundishana na kukosoana kistaarabu na si kubezana na kuzodoana.
Ni matamanio ya makapuku JF iwe ni jamii iliyostarabika.

Asiyejua afunzwe
Aliyekosea arekebishwe.
Na si tofauti na hayo!

Makapuku wana mengi ya kujifunza kutoka kwa wakongwe, na wakongwe wana mengi zaidi ya kujifunza kutoka kwa makapuku, sisi sote tunategemeana na hayupo ambaye ni bora zaidi kuliko mwingine, sote tuko sawa!

Ni tumaini la waasisi kuona JF inakuwa sehemu pendwa kwa wote, wakongwe na wenyeji na kuwa hakuna hata mmoja atakayenyanyaswa kwa ugeni wake.

Kwa niaba ya viongozi wa vuguvugu hili naomba makapuku tupunguze munkari na turudie maisha yetu ya kawaida.

Kama tulivyofanikiwa katika vuguvugu hili, nguvu hiyo hiyo tuipeleke katika kuwa mabalozi wema wa makapuku kokote ndani ya JF.

Uzi huu utabaki kuwa ni chachu katika harakati hizi.
Noted
 
Kuna mtu anaweza kujiuliza makapuku wa Jf ni nani?
Kama una kati ya sifa hizi basi knowingly or unknowingly wewe ni kapuku :

1)Kama uki comment watu wanakurukia kwa kebehi kama wewe wa juzi, poor thinking, Jf imevamiwa, siku hizi hamna great thinkers, eti na huyu gt, n.k basi jua wewe ni kapuku.

2) kama ukianzisha uzi comments hazifiki page mbili wkt mwenzako hata akipost Namkubali sana member fulani zinamiminika comments page 20. Basi usingoje tukutaje, we ni kapuku.

3)Kama ukichangia hupati likes wakati mwenzako ana comment "duh" anakula likes nane. Basi karibu sana kwenye jukwaa wewe ni kapuku mwenzetu.

4) kama post zako hazimalizi saa 24 bila kufutwa au kuunganishwa na nyingine. Basi jina letu ni lile lile kapuku

5)Kama ukiingiza masihara kidogo kwenye post za wakubwa unajikuta umekula ban. Basi ndio ukapuku wenyewe tunaousema.

Na mambo mengine kama hayo
Daaaaaah, kapuku umetishaaaaaa
 
Back
Top Bottom