Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230922_083326_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230922_083341_Opera%20Mini.jpg
 
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamekufa huku mwanamke akiwa amechinjwa na mwanaume ambaye hajafahamika jina akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 katika Mtaa wa Oysterbay, Kata ya Dodoma Makulu kwenye chumba ambacho mwanamke aliyeuawa Samira Mathias alikuwa amepanga.

Akizungumza na Mwananchi katika eneo la tukio mwenye nyumba hiyo, Donald Nhembelo amesema alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye chumba cha mpangaji wake (Samira) saa 7.00 usiku.

Amesema baada ya kufika kwenye chumba hicho alisikia sauti ya mwanaume akiomba msaada ndipo alipouliza Samira yuko wapi na kujibiwa kuwa hawezi kuongea na yeye hawezi kusimama.

“Aliniomba nivunje mlango ili nimsaidie. Nilivunja ubao uliopo juu ya mlango (Venti) na kuingiza mkono kwa ndani na kufungua mlango na nilipowasha taa ndipo nilikuta Samira yuko juu ya kitanda amenyamaza,”amesema.

Amesema damu zilikuwa zimetapakaa kitandani na sakafuni huku mwanaume aliomba msaada ambaye hamfahamu akiwa amelala chini huku utumbo wake ukiwa nje.

Amesema baada ya kuona hali hiyo, aliripoti polisi ambao walifika kwenye eneo hilo ambao baadaye waliondoka na miili ya watu hao.

Balozi wa mtaa wa Oysterbay, Isaya Mabigiri amesema amepata taarifa za uwepo wa tukio kutoka kwa mwenye nyumba hiyo na alipokwenda alikuta miili ya watu.

View attachment 2754130
Duh
 
..binafsi sijambo sana mdau, asante kwa kunijulia hali. Sio veterani mwenzangu makaveli10 anasingizia mgao wa umeme wakati viongozi wanasema sio mgao ni upungufu
Mgao maana yake kugawa, imetokana na neno gawa, gawanya, yaani kila mtu apate hata hicho kidogo, huenda ikawa zamu zamu.
Mfano.
KUGAWA URODA.

Upungufu, imetokana na neno, pungua, yani kitu ambacho hakijafikia utimamu wake(kihisabatia tunaita kitu kizima), kama ukihitaji maji lita 1 ukapata ½ lita maana yake hapo ½ ni pungufu
Mfano.
Upungufu wa kinga za mwili.

Tutunge sentensi kutokana na maneno MGAO na upungufu.

UKIGAWA sana uroda, utapata UPUNGUFU wa kinga za mwili.

See you next time class, see you, when you see me.😂
 
Mgao maana yake kugawa, imetokana na neno gawa, gawanya, yaani kila mtu apate hata hicho kidogo, huenda ikawa zamu zamu.
Mfano.
KUGAWA URODA.

Upungufu, imetokana na neno, pungua, yani kitu ambacho hakijafikia utimamu wake(kihisabatia tunaita kitu kizima), kama ukihitaji maji lita 1 ukapata ½ lita maana yake hapo ½ ni pungufu
Mfano.
Upungufu wa kinga za mwili.

Tutunge sentensi kutokana na maneno MGAO na upungufu.

UKIGAWA sana uroda, utapata UPUNGUFU wa kinga za mwili.

See you next time class, see you, when you see me.😂
....hii imekaa kikubwa sana. Kwa hiyo wale ambao hatujakamilisha ada tusikopi notice!?
 
....hii imekaa kikubwa sana. Kwa hiyo wale ambao hatujakamilisha ada tusikopi notice!?
Kopini, ila waambieni wazee wenu wapunguze kunywa bia, walipe ada...
Bia moja 3500, mbagala chapati 2 jero.. maana yake kwa hela hiyo unapata chapati 14 ye anakunywa bia moja, akinywa 10 je? Unaoata chapati 140. 🤣😂
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesitisha utoaji wa posho kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani isipokuwa madiwani na kutaka zikatumike kukamilisha ujenzi wa shule tano za msingi ambazo miradi yake imeonyesha kusuasua.

Homera ametoa agizo hilo jana Septemba 22, 2023 baada ya kutorishiwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ilipokea fedha kutoka Serikali hali iliyosababisha kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi watumishi wanane wakiwemo walimu wakuu watano, wahandisi wawili na ofisa manunuzi.

“Ile asilimia 40 inayokwenda kwenye maendeleo na ile nyingine 60 za posho kuanzia sasa hazitatolewa kwa watumishi na badala yake zitaelekezwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya elimu isipokuwa madiwani pekee walipwe posho zao,”amesema.

Amesema katika asilimia hizo zinazotolewa na halmashauri kwa sasa watakaopata ni madiwani pekee lakini kwa upande wa watumishi zimesitishwa mpaka hapo miradi ya elimu itakapokamilika na wanafunzi kuanza kupata huduma.

Aidha ameagiza watumishi wote ambao wako kwenye kamati za ujenzi kutokusafiri kwenda nje ya mkoa mpaka hapo miradi hiyo itakapokamilika katika Shule za Kasumuru, Mapinduzi, Luteba, Uhuru na Mababu Wilaya ya Kyela.
Screenshot_20230923_150328_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom