Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara amewahakikishia wadau wanaotumia Kituo cha Forodha Tunduma kuvusha mizigo kupitia Nakonde upande wa Zambia kuwa kutokana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema kwamba watendaji wahakikishe kuwa changamoto zote zinazowakabili wasafirishaji mizigo kwenda nchi za Zambia, DRC, Zimbabwe na nchi nyingine zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Prof Kahyarara ameyasema hayo kwenye kikao kilichowakutanisha watendaji wa Serikali wanaofanya kazi katika mpaka wa Tunduma.

“Tayari Trade Mark East Afrika pamoja na Benki ya Dunia wako tayari kugharamia mpango kabambe wa maboresho mradi utakao gharimu dola milioni 27 na kutekelezwa kwa mwaka mmoja” amesema Kahyarara.

Pia amesema utakapokamilika utawezesha kituo hicho kuwa na mifumo inayosomana kwa kuwa na ‘scanner’ za kisasa kutumia mifumo ya kisasa ya Tehama hatua itakayoongeza ufanisi na ushindani kwa Bandari ya Dar es Salaam.
Screenshot_20230923_150521_Instagram.jpg
 
Watu tisa wamefariki dunia huku 23 wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana Septemba 22, 2023 katika mteremko wa Iwambi, Wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya ikihusisha magari mawili.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga imeeleza kuwa katika ajali hiyo watu tisa walipoteza maisha na kati ya hao, wanaume ni watano na wanawake wanne.

Amesema watu 23 walijeruhiwa, ambapo wanaume ni 13 huku wanawake wakiwa 10, majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya Ifisi iliyopo mji mdogo wa Mbalizi.

“Miili ya marehemu pia imehifadhiwa kwenye hospitali hiyo na marehemu saba tayari wametambuliwa, huku miili miwili bado haijatambuliwa,” amesema.

“Chanzo cha ajali ni dereva wa lori Mohamed Abilah (47) raia wa Zambia kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuligonga kwa nyuma gari ya abilia. Dereva huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema Kuzaga.

Screenshot_20230923_150626_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Septemba 23, 2023 amemteua Jenerali Paul Kisesa kuwa Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Aidha, aliyekuwa akiongoza katika nafasi hiyo, Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango.
Screenshot_20230923_150732_Instagram.jpg
 
Wakati changamoto ya upatikanaji umeme ikiendelea kushika kasi nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko akimteua Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Kabla ya uteuzi huo Nyamo - Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) ambapo amechukua nafasi ya Maharage Chande aliyehamishiwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Screenshot_20230923_150824_Instagram.jpg
 
Kocha Robertinho amefurahi kumuona Luis Miquissone akicheza kwa dakika zote 90 bila kuchoka.

“Awali alikuwa hawezi kufanya hivi, lakini tumemuona akizidi kuwa bora na kutochoka, hili ndilo tunalotaka kwani tukiwa wote kwenye ubora inatusaidia,” alisema Robertinho ambaye alikuwa anasema mara kwa mara mchezaji huyo hakuwa fiti kwa sababu alichelewa kujiunga na wenzake katika pre season.

“Timu yangu ina makundi mawili, lakini yote yapo sawa kwa kulingana kwa sasa jambo ambalo linanipa nguvu katika kila mchezo unaokuja. Viwango vya wachezaji vinazidi kuimarika, hii inafurahisha.”
Screenshot_20230923_151002_Instagram.jpg
 
Stephen Sey amefanikiwa kujiunga na Klabu ya Al-Suqoor ya Libya [emoji1149] akisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Dodoma Jiji ya hapa nchini.
.
Sey ambaye amewahi kutamba na Namungo ya Lindi amesaini mkataba huo wiki iliopita baada ya kufuzu majaribio ya wiki mbili.
.
Hata hivyo, Sey bado hajatambulishwa rasmi na klabu hiyo akisubiri hali ya nchini humo kutulia kufuatia ligi kusimamishwa kutokana na janga la mafuriko lililoikumba nchi hiyo.
Screenshot_20230923_151136_Instagram.jpg
 
[emoji599] SIMBA HATARI DK 15-20
.
Rudia magoli mawili yaliyopatikana kwenye mchezo wa kwanza baina yao na Mtibwa ambapo walipata bao mbili za haraka haraka kupitia kwa Willy Onana na Baleke, juzi pia walpata bao mbili za haraka kupitia kwa Baleke.
.
Wanachofanya Simba ni kuhama haraka kutoka kwenye mfumo mama wa 4-2-3-1 na kuingia kwenye 3-5-1-1 ambapo Chama huwa karibu zaidi na mchezaji wa juu kumrahisishia ufungaji.
Screenshot_20230923_151231_Instagram.jpg
 
Kocha wa Simba, Robertinho amefunguka juu ya majeraha aliyopata beki Henock Inonga
.
“Ni habari mbaya sana kwetu hasa wakati huu tunatafuta muunganiko wa timu yetu, tupo kwenye wakati wa kuiunganisha timu na mchezaji na beki bora Afrika ameumia vibaya.“
.
“Kwa haraka haraka nadhani tunaweza kumkosa kwa siku 15 au 20, kile ni Kidonda kikubwa kilichohusisha ushonaji wa nyuzi kama 12 au zaidi, itategemea atakuwa na uponaji wa haraka kwa namna ipi, tunamuombea sana apone haraka,” aliongeza.
.
Pia Robertinho alisema tukio lile liliwaumiza wachezaji wake kwa mshtuko na kuwafanya kushindwa kujituma uwanjani mara baada ya kuona jeraha lake. “Kuna mchezaji aliniomba nimtoe, lakini nilikataa ilihitaji kuwajenga kisaikolojia, wenzake.”
Screenshot_20230923_151356_Instagram.jpg
 
SIRI YA TATTOO YA MESSI MGUUNI
.
Staa wa Inter Miami, Lionel Messi amesisitiza tattoo yake aliyochora mguuni ni maalumu kwa ajili ya timu yake ya zamani Barcelona. Messi, 36, alikipiga Barcelona kwa muda wa miaka 21 kabla ya kutimkia PSG kutokana na mataizo ya kiuchumi. Lakini, licha ya kuondoka staa huyo wa Inter Miami bado anaipenda Barcelona kutoka moyoni.
.
Akizungumza kwenye mahojiano na mchekeshaji maarufu kutoka Argentina Migue Granados, Messi alifafanua kuhusu tattoo hiyo.
.
“Nilichora tattoo kuonyesha mapenzi yangu kwa Barcelona. Ilikuwa kila kitu kwangu, ilichorwa vizuri sana, imechorwa mpira, nembo ya Barcelona, na namba 10,” alisema Messi akaeleza alidizaini tattoo hiyo ili kubadilisha tattoo yake ya zamani.
Screenshot_20230923_151512_Instagram.jpg
 
Messi ameulizwa kuhusu mipango yake baada ya kustaafu soka Je anatamani kuwa Kocha ? majibu yake ;

"Sitakuwa Kocha ! Lakini Zidane pia alisema hivi na baadae akawa Kocha na akashinda ubingwa wa UEFA "

“Natamani kuwa Mkurugenzi wa Michezo, lakini sijui nianzie wapi napenda kufundisha kuhusu soka,zaidi napendelea kufundisha watoto wadogo “

[emoji238]
Screenshot_20230923_151620_Instagram.jpg
 
Kocha wa Chelsea amefanya mazungumzo na mshambuliaji wake Nicolas Jackson ambaye ameonekana kutokuwa na makali tangu ajiunge na Chelsea ,hadi sasa amefunga goli moja (1) ,kadi za njano nne (4) uwezo wa kulenga lango 33% na amekosa nafasi sita (6) za wazi kwenye mechi tano (5) za Premier League .

Pochettinho amemshauri kuongeza utulivu zaidi uwanjani hasa akiwa mbele ya lango akilinganisha na hali aliyowahi kupitia Vinicius Jr, ambaye alichukua misimu miwili kutulia na kuonesha makali

“Nimezungumza na Nicolas Jackson nimemsema kwa kuwa mshambuliaji mwenye kadi nne za njano hadi sasa”

"Jackson ana umri wa miaka 22, ni mdogo anahitaji kujifunza, anahitaji kuimarika, anahitaji kutulia mwisho atakuwa mchezaji mzuri”

“Napenda kufanya mfanano na wachezaji wa Klabu zingine , Jackson anahitaji kuwa mtulivu na kutulia mbele ya goli nimemfananisha na Vinicius ambaye alichukua misimu mitatu, au misimu miwili na nusu kucheza Madrid”

Wakati tunampa misimu mitatu ya uvumilivu swipe kuona namba za Jack
Screenshot_20230923_151709_Instagram.jpg
 
Washambuliaji wa Al Nassr Cristiano Ronaldo na Sadio Mané wameanza vizuri msimu wa 2023| 24 [Saudi Pro League ] , hadi sasa mechi saba zimechezwa CR7 yupo juu kama mfungaji bora hii ni baada ya kuweka chuma mbili jana dhidi ya Al Ahli

Ronaldo: [emoji460]️9
4 assists
Mané: [emoji460] 6
1 assist

Screenshot_20230923_151801_Instagram.jpg
 
Mgao maana yake kugawa, imetokana na neno gawa, gawanya, yaani kila mtu apate hata hicho kidogo, huenda ikawa zamu zamu.
Mfano.
KUGAWA URODA.

Upungufu, imetokana na neno, pungua, yani kitu ambacho hakijafikia utimamu wake(kihisabatia tunaita kitu kizima), kama ukihitaji maji lita 1 ukapata ½ lita maana yake hapo ½ ni pungufu
Mfano.
Upungufu wa kinga za mwili.

Tutunge sentensi kutokana na maneno MGAO na upungufu.

UKIGAWA sana uroda, utapata UPUNGUFU wa kinga za mwili.

See you next time class, see you, when you see me.😂
Umetisha Mwalimu mwenzangu

Kwa jinsi ulivyotoa mifano rahisi hivi ikitokea kuna Mwanafunzi hajaelewa basi huyo atatakiwa kurudia darasa 🤪
 
Back
Top Bottom