Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230925_071548_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230925_071607_Opera%20Mini.jpg
 
Mwanariadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Berlin Marathon akifanikiwa kumaliza nafasi ya kwanza kwa muda wa 2:02:42 ikiwa ni ushindi wa tano katika mbio hizo za ujerumani kuanzia mwaka 2015.

Kipchoge ameshinda mbio hizo zilizofanyika nchini Ujerumani asubuhi ya leo Jumapili Septemba 24, 2023 huku akipokea pongezi kutoka kwa watu mashuhuri akiwemo Rais wa Kenya William Ruto pamoja na makamu wake.

“Nilitarajia kuvunja rekodi ya dunia lakini malengo yangu hayakutimia, nilikua vizuri kimwili lakini nilipata kidogo changamoto ya kwikwi ila ni kawaida. Ni mwendelezo wa kujifunza na hili nitaenda kulifanyia kazi kwa ajili ya mwakani katika mbio za Paris Olympic,” amesema.

Mshindi huyo mara tano wa Berlin Marathon ameshinda mbio hizo mwaka; 2015, 2017, 2018, 2022 na 2023.

Screenshot_20230925_073252_Instagram.jpg
 
Vuguvugu la mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Malindi baada ya kukabidhiwa kwa mwekezaji bado halijapoa, sasa wamiliki wa meli wameibuka wakilalamikia gharama za kulipia meli kutia nanga.

Wamesema hali hiyo huenda ikasababisha kuongezeka kwa gharama za bidhaa.

Tangu Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) lilipokabidhi uendeshaji wa bandari hiyo kwa mwekezaji Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) ya Ufaransa, Septemba 18, mwaka huu kumeibuka malalamiko ya kuongezeka kwa ushuru na kusababisha baadhi ya shughuli kusimama.

Wadau wa bandari, hususani wa majahazi wanalalamikia kupandishiwa ushuru mara mbili ya bei iliyokuwapo awali.

Hata hivyo, bei hizo zimeelezwa kuwa ndizo halali kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2018, lakini zilikuwa hazifuatwi.

Wakizungumza na Mwananchi, wamiliki wa meli walisema iwapo yasipofanyika mabadiliko ya haraka, athari zitajitokeza, hususan kwa wananchi wa kawaida kwa sababu bidhaa zitapanda bei.

Mansour Said, mmiliki wa meli alisema mpaka sasa kuna meli tatu zimezuiwa kutia nanga kwa sababu hazijalipiwa. "Huu utaratibu wa kuanza kulipia meli kabla ya kufika bandarini unaibua changamoto mpya, kwa kawaida meli inatia nanga ndipo unalipa, maana kwanza wahusika washushe mzigo.

"Pia gharama za kulipia zipo juu ikilinganishwa na bandari nyingine, tunalipa Dola tatu za Marekani (Sh7,500) kwa tani moja, wakati Bandari za Dar es Salaam na Mombasa tunalipa Dola mbili (Sh5,000)" amesema.

Mmiliki mwingine wa meli, Hamad Khamis, maarufu kama Kisu, alisema hatua hiyo inasababisha hata makasha yasishushwe kwa wakati kutokana na ongezeko la gharama.
Alisema kwa sasa bei ya saruji mfuko mmoja ni Sh17,000, lakini hali hiyo ikiendelea utauzwa hadi Sh20,000 kwa sababu hakuna mfanyabiashara atakubali kuuza bidhaa kwa hasara.

Akizungumzia hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alisema baadhi ya wafanyabiashara wameanza kutumia mwanya huo kwa kisingizio cha bandari kupandisha bei za bidhaa, akionya hawatakubali jambo hilo litokee.
Screenshot_20230925_073442_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom