Makapuku Forum

Makapuku Forum

Pengine hukulishuhudia hilo katika shughuli zako za kila siku, lakini takwimu zinaonyesha mzunguko wa fedha ulikuwa mkubwa mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Kati ya Januari hadi Novemba 2023 kulikuwa na mwenendo chanya wa mzunguko wa fedha na wastani kulikuwa na ongezeko la asilimia 13.8.

Hii maana yake ni kuwa vyuma vililegea zaidi mwaka 2023, kwani ripoti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT) inaonyesha Novemba 2023, jumla ya fedha zilizokuwa kwenye mzunguko wa uchumi ndani ya nje (M3) zilikuwa na thamani ya Sh43.58 trilioni ikilinganishwa na Sh38.33 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2022.

Screenshot_20240112_150035_InstaPro%20.jpg
 
Mtoto wa miezi mitano, Leornad Kabilu, mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa wilayani Geita amefariki dunia baada ya kupigwa na baba yake sehemu mbalimbali mwilini kwa kutumia mkanda na kiatu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea jana Alhamisi Januari 11,2024 saa saba usiku wakati wakiwa wamelala na chanzo cha tukio hilo kinadaiwa ni ugomvi wa kifamilia.

Kamanda Jongo amesema mtuhumiwa, Kabilu Mayege (20) baada ya kutenda kosa hilo ametoroka na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.

Akizungumza mama wa mtoto huyo, Riziki Leornad amesema siku ya tukio mumewe alitoka kuangalia mpira na akataka amuandalie chakula wakati mtoto amelala na wakati anakula mtoto alianza kulia na mama akabaki akitoa vyombo mezani na mumewe kupanda kitandani alikokuwa amelala mtoto.

Screenshot_20240112_150159_InstaPro%20.jpg
 
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio ya mbwa wa kufungwa majumbani kuwashambulia wamiliki wake huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwemo kichaa.

Akizungumza na Mwananchi Digital, mtaalamu wa mifugo, Joseph Ndalu amesema sababu za mbwa kuwashambulia wamiliki wake zinatofautiana kulingana na mazingira.

Amesema utamaduni wa kufuga wanyama hao kiholela na kwa mazoea ni sababu kuu.

Ndalu ametaja sababu nyingine kuwa ni ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kutopewa chanjo na dawa za kuua vimelea wa nje na ndani ikiwamo minyoo, kutopewa chakula kwa wakati na kwa ujazo unaohitajika, kufanyishwa michezo wasiyoipenda na kuanzisha mazingira hatarishi kwa kiumbe huyo.

Screenshot_20240112_150339_InstaPro%20.jpg
 
Ukishamaliza matibabu, dawa unazopewa na wataalamu wa afya umewahi kuhoji au kujiuliza ni za aina gani, zitasaidia nini na zinaweza kukupa athari gani baada ya kuzitumia?

Watafiti wamechambua hilo na kubaini wataalamu wa afya wamekuwa wakitoa dawa nyingi za antibaotiki kwa wagonjwa tofauti na kiwango kinachotakiwa kimataifa, huku zile za mstari wa tatu na nne ambazo hazishauriwi zikitumika.

Hali hiyo imetajwa kusababisha ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa za antibaotiki mwilini ‘Antimicrobial resistance AMR’.

Hiyo ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas) zilizoonyesha Tanzania imefikia matumizi ya asilimia 88.0 kwa dawa za antibaotiki kinyume na mwongozo uliowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unaoelekeza nchi zitumie asilimia 20.0 hadi 26.8.

Screenshot_20240112_150651_InstaPro%20.jpg
 
Pengine hukulishuhudia hilo katika shughuli zako za kila siku, lakini takwimu zinaonyesha mzunguko wa fedha ulikuwa mkubwa mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Kati ya Januari hadi Novemba 2023 kulikuwa na mwenendo chanya wa mzunguko wa fedha na wastani kulikuwa na ongezeko la asilimia 13.8.

Hii maana yake ni kuwa vyuma vililegea zaidi mwaka 2023, kwani ripoti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT) inaonyesha Novemba 2023, jumla ya fedha zilizokuwa kwenye mzunguko wa uchumi ndani ya nje (M3) zilikuwa na thamani ya Sh43.58 trilioni ikilinganishwa na Sh38.33 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2022.

View attachment 2869710
Uliongezeka wapi huko?
 
Huu ni muhtasari wa mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza yaliyoanzishwa dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen mapema Ijumaa.
Rais wa Marekani, Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak wamethibitisha kuanzisha mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen.

Mashambulizi hayo yameanza mapema leo Ijumaa Januari 12, 2024 wakisema ni jibu la mashambulizi ya mara kwa mara ya Wahouthi dhidi ya meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu.

Makombora ya kivita ya Tomahawk na ndege za Marekani yalishambulia maeneo 12, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu, Sanaa, na Hudaydah, ngome ya bandari ya Houthi.

Ndege nne RAF Typhoon zilishambulia maeneo mawili ya Wahouthi, zikiruka kutoka kambi ya Akrotiri huko Cyprus huku wakipata usaidizi kutoka nchi za Australia, Bahrain, Canada na Uholanzi kwa mujibu wa viongozi hao.

Ofisa wa Houthi ameionya Marekani na Uingereza kuwa "zitalipa gharama kubwa" kwa "uchokozi huo wa wazi" waliouanzisha.

Screenshot_20240112_150758_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom