Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio ya mbwa wa kufungwa majumbani kuwashambulia wamiliki wake huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwemo kichaa.
Akizungumza na Mwananchi Digital, mtaalamu wa mifugo, Joseph Ndalu amesema sababu za mbwa kuwashambulia wamiliki wake zinatofautiana kulingana na mazingira.
Amesema utamaduni wa kufuga wanyama hao kiholela na kwa mazoea ni sababu kuu.
Ndalu ametaja sababu nyingine kuwa ni ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kutopewa chanjo na dawa za kuua vimelea wa nje na ndani ikiwamo minyoo, kutopewa chakula kwa wakati na kwa ujazo unaohitajika, kufanyishwa michezo wasiyoipenda na kuanzisha mazingira hatarishi kwa kiumbe huyo.
View attachment 2869714