Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francisco ameridhia ombi la askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Mkoa wa Kagera, Methodius Kilaini la kustaafu kwake.
Taaarifa za kustaafu kwake zimetolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga katika sherehe ya kuwekwa wakfu kwa Jovitus Mwijage kuwa askofu wa Jimbo la Bukoba, inayofanyikia Uwanja wa Kaitaba, mkoani humo, leo Jumamosi, Januari 27, 2024
“Tumepata taarifa kutoka Roma muda huu saa nane, ombi la Baba Askofu Kilaini la kutaka kustaafu limekubaliwa rasmi,” amesema Askofu Nyaisonga.
Baada ya taarifa hiyo, Askofu Kilaini ameitwa sehemu ya kuzungumzia na kuimba, “nimeumaliza mwendo, nimeumaliza mwendo, nimevipiga vita vilivyo vizuri…” huku wakiitikia wimbo huo.
Kisha Askofu Kilaini amesema, alimualika Rais mstaafu Jakaya Kikwete katika shughuli hiyo lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake ameshindwa kufika.