Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waafrika hawavumilii vitendo vya ushoga - Papa Francis

Papa Francis amekaririwa na gazeti moja la nchini Italia akisema kwamba kwa Waafrika ushoga ni kitu kibaya sana na hawavumilii jambo hilo. Papa Francis ameyasema hayo kufuatia waraka ulitolewa na idara ya elimu ya waamini huko Vatican kuruhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kupewa baraka.

Waraka huo umezua gumzo miongoni mwa waumini wa Kanisa Katoliki na hata maaskofu wa kanisa katoliki Afrika wamekataa kwamba hawawezi kuwabariki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Katika mahubiri yake, Askofu Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita alisema, "kubariki mashoga bora nibariki jiwe ujengee nyumba."

Katika mahojiano yake na gazeti hilo Papa Francis amesema anaamini kwamba ipo siku watu wataelewa msimamo wake na kuacha kuwatenga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja hata hivyo Papa amekiri kwamba kwa Waafrika ni kinyume na wanapinga jambo hilo, Papa amesema, "Kwa Waafrika, kwao ushoga ni jambo mbaya na hawavumilii".

Licha ya waraka huo uliozua gumzo bado msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu ndoa ni ule ule kwamba ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke na si vinginevyo..!
Screenshot_20240131_075806_InstaPro%20.jpg
 
LiTitanic la kizazi chetu limeanza kazi....hii ndio meli ya abiria kubwa kwa sasa hapa duniani.... inaitwa The Icons of the Seas...urefu wa meli hii ni zaidi ya viwanja vitatu vya mpira wa miguu...ina swimming pools 7, ina eneo maalum kwa ajili ya michezo ya kwenye mabarafu, idadi ya bar sasa...

Meli hii iliyotengenezwa kwa siku 900 huko Finland ni mali ya kampuni ya Royal Caribbean ya Marekani. Meli hii imeanza safari yake ya kwanza tarehe 27 January huko PortMiami, Florida Marekani... ina uwezo wa kubeba abiria 7,600 na wafanyakazi 2,350...mnapitajwe sasa wakati mimi nipo...!!!
Screenshot_20240131_080012_InstaPro%20.jpg
 
Sasa angalia kwenye kitako cha chupa za maji ya kunywa au juice...kama chombo kina alama hii hicho chombo kinatumika mara moja tu...

Ukiimaliza tupa usikutumie tena kwa kujaza maji au kuweka mafuta ya kula...pia chupa yenye alama hiyo isiwekwe nje kwenye jua au karibu na moto na kama ulikuwa umeyaacha maji yake kwenye gari ni bora kutupa..

Plastiki yenye alama hiyo ikitumika mara kwa mara au kukaa kwenye joto mfano nje kwenye jua au ndani ya gari kemikali za Antimony na Phthalates huwa zinayeyuka na kuingia kwenye maji.

Kemikali zinaweza kusababisha madhara kwa mtumiaji ikiwemo kuvuruga homoni za uzazi...halafu ukienda dukani usichukue maji ambayo yamepigwa na jua....haya share au mtag umpendae na yeye ajifunze na kama una makopo ya hivyo kwenye friji tupa kuanzia leo....!!!View attachment 2889327
Hapa nimejifunza kitu .Merci beacoup 🙏🙏
 
Timu ya Taifa la Afrika Kusini imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) wakiiondosha Morocco kwa kichapo cha mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Laurent Pokou nchini Ivory Coast.

Mabao ya mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji anayekipiga Orlando Pirates, Evidence Makgopa dakika ya 57 huku kiungo, Teboho Mokoena akipigilia msumari wa mwisho 90+ kwa mpira wa faulo nje kidogo ya eneo la 18.

Beki Achraf Hakimi anayecheza PSG ya Ufaransa amepoteza mkwaju wa penalti dakika ya 85 baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba na kwenda nje.

Morocco walilazimika kumaliza mchezo pungufu baada ya kiungo wake anayesakata soka la kulipwa kwenye klabu ya Manchester United, Sofyan Amrabat kupewa kadi nyekundu dakika ya 90 baada kumchezea madhambi Mokoena wa Afrika Kusini.

Timu zote zenye asili ya kiarabu zilizoshiriki fainali hizo zimeondoshwa kwenye ambapo zilikuwa ni Misri, Algeria, Tunisia na Morocco waliokuwepo kati mataifa 16 yaliyoshiriki.

Afrika Kusini itamenyana na Cape Verde Februari 3, mwaka huu katika hatua ya robo fainali.

Screenshot_20240131_082018_InstaPro%20.jpg
 
Mkazi wa Mtaa wa Kapalangao Manispaa ya Mpanda, Fransis Nilanga amedaiwa kufukua kaburi la mwanaye kisha kubeba jeneza lenye mwili huo kwenda nalo nyumbani kufanya maombi ili afufuke.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumanne Januari 30, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema tukio hilo limetokea Januari 28 saa saba usiku.

"Mtoto wake alifariki na kuzikwa Julai mwaka jana katika makaburi ya Kazima akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu. Sisi tulipata taarifa kutoka kwa dereva wa bajaji aliyejitambulisha kwa jina la Alex, akisema wakati anapita eneo hilo alimuona amebeba jeneza alimuomba amsaidie kubeba kwenda nyumbani," amesema Kamanda Ngonyani.

Pia, amesema baada ya kupata taarifa walimkamata na alipofikishwa Kituo cha Polisi Mpanda kufanyiwa uchunguzi, walibaini mtuhumiwa huyo ana ugonjwa wa afya ya akili.
Screenshot_20240131_082122_InstaPro%20.jpg
 
Timu ya taifa ya Mali imetinga robo fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuichapa Burkina Faso mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly nchini Ivory Coast.

Mabao ya mchezo huo kwa upande wa Mali yamefungwa na beki Edmond Tapsoba aliyejifunga dakika ya tatu na Lassine Sinayoko 47’ huku la Burkina Faso likifungwa na Betrand Traore 57’ kwa mkwaju wa penalti.

Mali itashuka dimbani Februari 3, mwaka kuchuana na Ivory Coast kusaka tiketi ya kucheza nusu fainali.
Screenshot_20240131_082254_InstaPro%20.jpg
 
Timu ya watalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji nchini, (Ewura) imefika katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kufuatilia na kufanya tathmini ya kina juu bili za maji.

Wataalamu hao wamewasili leo Januari 30, 2024 kufanyia kazi malalamiko ya wananchi wa Maswa waliyoyatoa kwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda wakidai kwa Mamlaka ya Maji ya Maswa inawatoza bili kubwa ya maji.

Baada ya malalamiko hayo yaliyotolewa jana, Makonda aliwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye alitoa ahadi kwamba ndani ya siku moja angewaelekeza mamlaka husika (Ewura) kufika na kufanya tathmini upya na kuja na ushauri juu ya kiwango sahihi cha wananchi kuchangia huduma hiyo.

Screenshot_20240131_082354_InstaPro%20.jpg
 
Wataalamu wa afya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, wameagizwa kuanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike ili kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Agizo hilo limetolewa leo Januari 30, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili katika Halmashauri ya Ileje baada ya kuibuka kwa hoja ya wanawake wilayani humo, kuogopa kutumia kondomu kutokana na ukubwa wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Ukimwi ambaye ni Diwani wa Kata ya Itale, Fahari Mwampashi amesema hofu ya watumiaji wa kondomu hizo, wamesema kubwa ukilinganisha na maumbile yao wakitaka zipunguzwe.

Screenshot_20240131_083206_InstaPro%20.jpg
 
Baada ya bodi ya wakurugenzi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kumteua Raphael Maganga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo kuanzia Februari mosi, 2024 ameahidi kujenga sekta binafsi shindani na himilivu.

Maganga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na John Ulanga, ambaye aliteuliwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Septemba 26, 2023.

Taarifa ya TPSF iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Angelina Ngalula imeeleza Maganga alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu ulipofanyika uteuzi wa Balozi Ulanga.

Akizungumzia uteuzi huo, Maganga amesema sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi wa Taifa, hivyo anatambua kuwa ana jukumu la kuhakikisha inaendelea kuwa shindani na himilivu.

“Ninalo jukumu kubwa la kuhakikisha sekta binafsi inaendelea kuwa shindani na himilivu, na Tanzania iongoze katika kuwapo kwa mazingira ya biashara kupitia sera bora,” amesema.
Screenshot_20240131_083306_InstaPro%20.jpg
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Geita inaendelea kuchunguza safari ya China aliyokwenda aliyekuwa Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Zahara Michuzi ambaye Desemba mwaka jana alihamishiwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Uchunguzi huo ulioanza mwanzoni mwa Novemba 2023 ulitokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe aliyelitoa mwishoni mwa Oktoba, 2023 la kuitaka taasisi hiyo kuchunguza safari ya Mkurugenzi aliyekwenda nchini China kama ilikuwa kwa masilahi ya halmashauri au binafsi.

Pia aliitaka taasisi hiyo kubaini kama matumizi ya safari hiyo yalitokana na fedha za halmashauri au binafsi na endapo watabaini alitumia fedha za Halmashauri zirejeshwe na zielekezwe kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza jana Januari 30, 2024 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, Azza Mtaita amesema uchunguzi huo umechukua muda mrefu kwa kuwa ni wa mtu mkubwa kwenye taasisi, lakini pia fedha zilizochukuliwa ni nyingi.

Kuhusu uhamisho wake kama unaathiri uchunguzi Mtaita amesema kuhamishwa kwake ni faida kwa timu ya uchunguzi kwa kuwa imewapa uhuru watumishi wanaopaswa kutoa ushahidi, na kuifanya Takukuru kufanya kazi kwa kina zaidi.

“Ni kweli uchunguzi umechukua muda mrefu kwa kuwa naye ni mkubwa na fedha alizochukua ni nyingi na kuna mambo ambayo tunatakiwa tuyahakikishe, ni bora kuchukua muda mrefu kupata matokeo chanya.

“Hata chakula kilichopikwa muda mrefu ladha yake ni tofauti na ile ya haraka unapoandaa kitu muda mrefu kinakuwa na matokeo mazuri,” amesema Mtaita.

Hata hivyo, amesema uchunguzi utakapokamilika utatolewa kama wanavyotoa taarifa nyingine walizozifanyia kazi.
Screenshot_20240131_090917_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom