Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20240229_124810_InstaPro%20.jpg
 
Siku moja baada ya Polisi wa South Africa kuthibitisha kuwa wamewamakata Washukiwa sita wa mauaji ya Rapper Kiernan Forbes maarufu AKA yaliyotokea February 2022, leo Washukiwa watano kati ya sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Durban.

Mshtakiwa mwenye umri mkubwa kati yao ni Mziwethemba Myeza mwenye umri wa miaka 36, wengine ni Lindani Ndimande (35), Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Thabani (30) na Lindokuhle Ndimande (29).

Mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo hiyo ni Muandaaji Mkuu ‘Mastermind’, pia wamo Watumia bunduki wawili, watoa taarifa wawili na mmoja wa mwisho ni aliyehusika kutafuta silaha na magari.

Waziri anayehusika na Idara ya Polisi Bheki Cele jana alisema miongoni mwa waliokamatwa wamewahi kuhusishwa na mauaji ya kutisha ambapo walikimbilia Nchi jirani ya Eswatini ( zamani Swaziland) kujificha lakini tayari wamekamatwa.
Screenshot_20240229_134045_InstaPro%20.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi amesema yuko tayari kuzungumza na mwenzie wa Rwanda Paul Kagame ili kukomesha machafuko mashariki mwa Kongo.

Kauli imekuja baada ya mkutano wa ana kwa ana wa dakika 180 uliofanyika Luanda, Angola na kuwahusisha Rais Felix Tshisekedi na mwenyeji wake Joao Lourenco ambao hata hivyo hawakutoa kauli yoyote mbele ya Waandishi lakini Waziri wa mambo ya nje wa Angola, Tete Antonio baadae ndio alitoa kauli hii kwamba Tshisekedi amekubali kuzungumza na Paul Kagame, @dw_kiswahili wameripoti.

‘’Matokeo ya mkutano huu ni kwamba Rais Tshisekedi amekubali kimsingi kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Angola kama Mpatanishi sasa ina jukumu la kufanya kazi ili kufanikisha mkutano huo” — Tete.

Hatua ya Tshisekedi kukubali mazungumzo na Kagame imekuja miezi mitatu baada ya Kiongozi huyo kuapa kwamba hawezi tena kukutana na jirani yake huyo hadi mbele ya Mungu ambapo Ikulu ya Congo ilitoa masharti na kusema kabla ya mkutano wowote kufanyika kati ya Tshisekedi na Kagame ni lazima kwanza Wanajeshi wa Rwanda waondolewe katika eneo la Congo lakini pia Kundi la M23 lipokonywe silaha.
Screenshot_20240229_134212_InstaPro%20.jpg
 
Mzee mwenye umri wa miaka 72, Amos Mohamed amedaiwa kujipiga risasi na kujiua alipokuwa akisubiri matibabu katika hospitali moja eneo la Kusini B, Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Star ya nchini humo, mzee huyo alimtembelea wakili wake kabla ya kuagiza teksi ya kumpeleka hospitali.

Polisi wa eneo hilo wameanzisha uchunguzi baada ya mzee huyo kujifyatulia risasi na kujiua papo hapo katika mazingira ya kutatanisha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha Mohamed alijipiga risasi akiwa kwenye kiti cha nyuma cha gari lililompeleka hospitali.

Mwanamume huyo inadaiwa alikuwa akisubiri matibabu ya ugonjwa ambao haujajulikana.
Screenshot_20240229_134402_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom