Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wafuasi wa mgombea urais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu, Dakar, kusherehekea matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika jana, Machi 24, 2024, yakionyesha mgombea huyo wa upinzani anaongoza.

Sherehe hizo zilifanyika huku wagombea wasiopungua watano kati ya 19 katika kinyang’anyiro hicho wakitoa taarifa za kumpongeza Faye kwa kile walichokiita ushindi wake.

Hata hivyo, mpinzani wake mkuu kutoka muungano unaotawala, Waziri Mkuu wa zamani, Amadou Ba, amesema sherehe hizo zilikuwa kabla ya wakati wake.
“Kwa upande wetu, na kwa kuzingatia mrejesho wa matokeo kutoka kwenye timu yetu ya wataalamu, tuna uhakika kwamba, katika hali mbaya zaidi, tutaenda kwenye duru ya pili,” timu ya kampeni ya Ba imesema katika taarifa yake.

Hakukuwa na maoni ya moja kwa moja kutoka kwa Faye mwenyewe.

Mamilioni ya wananchi wa Senegal walipiga kura Jumapili kumchagua Rais wa tano wa nchi hiyo.

Hatua hiyo ilifuatia baada ya miaka mitatu ya msukosuko wa kisiasa ambayo haijawahi kushuhudiwa ikiwamo maandamano dhidi ya Serikali na kuungwa mkono kwa upinzani.

Kuna uwezekano wa kumalizika kwa utawala wa Rais anayemaliza muda wake, Macky Sall ambaye anaondoka madarakani baada ya muhula wa pili uliokumbwa na machafuko kutokana na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko.

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 

Attachments

  • Screenshot_20240325_144227_InstaPro .jpg
    Screenshot_20240325_144227_InstaPro .jpg
    279.2 KB · Views: 2
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umetangaza kuwa April 12, 2024, utaanza zoezi la ubomoaji nyumba katika Bonde la Msimbazi, Jijini Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa daraja jipya , ukarabati wa kingo za Mto, City Park na ujenzi maeneo ambayo ni korofi ambapo mradi huo utagharimu USD milioni 260.

Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia (TARURA), Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema “Tunataka kuanza zoezi la kubomoa pale Msimbazi kwa ambao tumeshawalipa wale 2155, tumepanga kuanzia rasmi Aprol 12,2024, wakati wa kulipa fidia tulikubaliana wataondoka ndani ya wiki 6, kwa wale ambao wameshindwa kufanya hivyo sisi tuanza hili zoezi tarehe 12”
Screenshot_20240325_220449_InstaPro%20.jpg
 
Mtu mmoja amesombwa na maji huku nyumba zaidi ya 100 zilizopo Tarafa ya Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro zikizingirwa na maji baada ya Mto Lumemo kujaa maji kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kilombero, Haji Muduluka amesema hadi sasa Wananchi zaidi ya 40 wameokolewa huku juhudi za kuokoa wengine zikiendelea .

Maduluka anasema hadi sasa Mtu mmoja anahofiwa kufariki baada ya kusombwa na maji akijaribu kuvuka ambapo jitihada za kumtafuta zinaendelea.

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo wamesema wapo waliopoteza chakula na makazi yao kusombwa na maji na kuomba juhudi zaidi za kunusuru uhai wao kufuatia mvua hizo kuendelea kunyesha.
Screenshot_20240325_220644_InstaPro%20.jpg
 
Beki wa zamani wa Simba na Yanga Ramadhani Waso amefariki Dunia leo March 25 2024 nchini kwao Burundi.

Taarifa ya kifo chake haijaeleza zaidi kuhusu chanzo cha kifo cha Mkali huyo wa soka lakini amefia kwa Burundi leo.

Waso alijiunga na Simba SC mwaka 2000 na alikuwa sehemu ya Kikosi cha Simba SC kilichoitoa Zamalek ya Misri mwaka 2003 katika michuano ya CAF.
Screenshot_20240325_220754_InstaPro%20.jpg
 
Baada ya Dereva Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma kukamatwa akiwa amebeba Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia katika gari aina ya Land Cruiser V8 likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM katika eneo la Minjingu mkononi Manyara, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoani Manyara Philon Kyetema leo amesema gari hilo, bendera pamoja na Dereva havina uhusiano wowote na Chama cha Mapinduzi.

“Gari lilikuwa na mlingoti na baada ya kufunuliwa ikakutwa bendera inayofanana na bendera ya Chama cha Mapinduzi maana yake ni kwamba huyu bwana Edward alijiandaa kuhadaa Vyombo vya ulinzi na usalama ili visimtie nguvuni lakini tunashukuru Askari Polisi wa Minjingu waliweza kumtilia shaka na kuzuia gari na ndani kukuta Wahamiaji hao 20, kesho tutawafikisha Mahakamani”

“Naomba kufafanua kwa Watanzania ninaomba wasihusishe gari hilo na bendera inayoonekana kwenye gari hilo haina uhusiano na Chama Tawala cha CCM, hilo gari lenyewe, bendera yenyewe pamoja na Dereva hawana uhusiano na Chama cha Mapinduzi” ——— Kyetema.
Screenshot_20240325_220904_InstaPro%20.jpg
 
FT: Tanzania 3-0 Mongolia (Kelvin 49’ Sopu 63’ Novatus 76’) #FIFASeries

Taifa Stars imepata ushindi wake wa kwanza wa michezo ya FIFA Series baada ya awali kupoteza 1-0 dhidi ya Bulgaria.
Screenshot_20240325_221020_InstaPro%20.jpg
 
Saa chache toka Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuagiza Mamlaka husika kutengeneza sehemu ya daraja la somanga iliyokatika na kukwamisha magari kusafiri kati ya Dar es salaam na mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, ukarabati wa muda mfupi wa kuokoa jahazi tayari umefanyika na sasa magari yameanza kupita.

Daraja hilo lilikatika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua zinaoendelea kunyesha na kusababisha magari ya abiria na mizigo kukwama njiani kwa saa kadhaa kitendo kilichopelekea Waziri Bashungwa kuagiza kazi ya ujenzi ifanywe usiku kucha ili mawasiliano yarejee kama kawaida.

Akiongea na @AyoTV_ kwa njia ya simu, Waziri Bashungwa ameishukuru Timu ya TANROADs ikiongozwa na Dkt.Kayoza na amempongeza pia Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohamed Nyundo na Timu yake kwa kazi nzuri ya kuhakikisha panapitika.
Screenshot_20240325_221126_InstaPro%20.jpg
 
Watoto wawili wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji walipokuwa wanavuka mto katika daraja la miti na mbao katika Mto Mzinga Kitongoji cha Churwi wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi leo Jumatatu Machi 25, 2924 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Protas Mutayoba amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 24 mwaka huu.

"Ni kweli tukio hilo limetokea Machi 24, 2024 saa kumi jioni na watoto hao walikuwa wanavuka mto wakiwa na mama yao Fadhila Alawi, mkazi wa Tandika Dar es Salaam."
Amewataja watoto waliopoteza maisha kuwa ni Habiru Stephano (1) na Ashfati Lishera(4).

Amesema juhudi za kutafuta miili ya watoto hao imepatikana na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Screenshot_20240325_221420_InstaPro%20.jpg
 
Rais wa Senegal anayemaliza muda wake, Macky Sall amempongeza mgombea wa upinzani, Bassirou Diomaye Faye kwa ushindi alioupata huku mshindani wake wa karibu, Amadou Ba akikubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Baada ya mgombea huyo wa chama tawala, Amadou Ba kutambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza na kutoa pongezi zake, Sall, ambaye alishinda chaguzi za mwaka 2012 na 2019, amesema “napongeza maandalizi mazuri ya uchaguzi na nampongeza mshindi, Bassirou Diomaye Faye ambaye mwenendo wa kura unaonyesha kwamba ameshinda.”

Mgombea huyo wa upinzani aliyeshinda hajawahi kushika nafasi ya kuchaguliwa ya kitaifa na bado hajazungumza hadharani tangu uchaguzi wa Jumapili Machi 24, 2024, uliofuatia miaka mitatu ya machafuko na mgogoro wa kisiasa.

Mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa chama tawala, Amadou Ba ametambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo na akatoa pongezi zake, ilisema taarifa.
Screenshot_20240325_221532_InstaPro%20.jpg
 
Fisi wanne wanaosadikiwa kushambulia na kuua watu katika Kata ya Kasenyi, wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wameuawa na wawindaji wa jadi kutoka wilayani Misungwi.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kasenyi, Juma Bupamba amethibisha kuuawa fisi hao.
Amesema wameuawa leo Machi 25, 2024 saa 11.00 jioni.

Ameeleza wawindaji hao wametumia takribani dakika 90 kuwaua wanyama hao.
Ofisa mtendaji huyo amesema baada ya kuona matukio ya watu kushambuliwa na fisi yamekithiri; na wananchi walichanga fedha kuwaita wawinda hao kutoka Kata ya Mbalika wilayani Misungwi.

Mkazi wa Kijiji cha Kasenyi, Amon Jonathan amesema fisi hao walikuwa tishio kwao, hivyo wanaamini watapa ahuweni.

Matukio ya fisi kushambulia na kuua watu yameripotiwa kwenye kata za Kasenyi, Chifunfu, Katunguru na Buyagu.

Watu watatu wamefariki dunia kwa kushambuliwa na fisi katika matukio tofauti wilayani Sengerema kati ya Januari hadi Febaruari 24, mwaka huu.

Tukio la kwanza lilitokea Januari 15, 2024, saa 12.30 jioni, kwa mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Nyakahako, Kata ya Chifunfu wilayani Sengerema, Sadiki Mashaka (16) kushambuliwa na fisi alipokuwa akichanja kuni mlimani.

Mwingine ni Mkazi wa Kijiji cha Lukumbi, Kata ya Chifunfu wilayani humo, Mkabagobi Sibanga (70), aliyefariki dunia Januari 29, 2024, saa 11.30 alfajiri, baada ya kushambuliwa na fisi akielekea shambani kuvuna mahindi.

Katika tukio lingine, mtoto wa miaka sita, Adela Shimba, mkazi wa Kijiji cha Kafundokile, Kata ya Kasenyi wilayani humo aliuawa na fisi Februari 16, 2024 alipokuwa ameambatana na bibi yake kwenda kuchota maji mtoni.

Taarifa za matukio hayo zimethibitishwa na Mkuu wa Idara ya Wanyamapori katika Halmashauri ya Sengerema, Paul Ponsian alipozungumza na Mwananchi Digital hivi karibuni.
Screenshot_20240325_221644_InstaPro%20.jpg
 
Kituo maalum cha kupima na kuthibitisha madini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimeanzishwa Bandari ya Dar es Salaam ili kuthibiti utoroshaji wa madini ya shaba.

Hatua hiyo ya ushirikiano baina ya Tanzania na DRC kinakwenda kumaliza tatizo la wizi wa madini hayo ambayo umekuwa ukitokea na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara na Serikali za nchi hizo mbili.

Kituo hicho kidogo cha biashara za madini, kipo chini ya ofisi ya Mamlaka ya Tathmini na Uthibitishaji wa Utaalamu (CEEC) ya nchi hiyo, kitathibitisha madini yote kutoka DRC yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam. Hatua hiyo itasadia kuongeza imani kwa wawekezaji na hatimaye kuzinufaisha nchi zote mbili.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa kituo hicho cha biashara leo Jumatatu, Machi 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Mwambata wa Kibiashara kutoka Ubalozi DRC nchini Tanzania, Kasongo Yampanya amesema kwa muda mrefu nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya wizi wa bidhaa za madini hasa shaba.

“Tunashukuru Serikali za nchi zote mbili kwa kuungana na kukubali kuanzisha kituo hiki. Itahakikisha bidhaa zote za madini zinafika kwenye nchi husika bila vizuizi,” amesema.

Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa TPA, Dk George Fasha amesisitiza umuhimu wa DRC kuwa moja ya masoko sita muhimu kutokana na ongezeko la mizigo inayopita katika bandari ya Dar es Salaam tangu 2018.

"Kuanzishwa kwa ofisi katika nchi yetu kunatoa ujumbe wa wazi kwamba wako tayari kufanya biashara na sisi, kwa hiyo, natao wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hizi ili kuvutia wawekezaji zaidi,” amesema.

Screenshot_20240325_221813_InstaPro%20.jpg
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko amezindua namba ya simu 115 ya dharura itakayokuwa suluhisho la vifo vya wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga.

Namba hiyo ya bure imezinduliwa leo Jumatatu, Machi 25, 2024 jijini Dodoma kwenye mkutano wa siku tatu kimataifa wa Afya ya Msingi unawakutanisha wataalamu wa afya kutoka Afrika na ulimwenguni.

Dk Biteko amesema itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama mtoto vilivyotokana na ukosefu wa msaada paleikiwamo usafiri wanapopata dharura.

“Ninawagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha namba hii inapatikana kwenye huduma zote za afya,” amesema Dk Biteko ambaye amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan Kwenye mkutano huo.

Amsema m-mama inaratibiwa katika hospitali za mikoa kupitia waratibu waliopewa mafunzo. Kwa kupiga namba 115, waratibu wa m-mama katika kila mkoa wanaweza kutoa huduma hizo.

Screenshot_20240325_221924_InstaPro%20.jpg
 
Simba inakamilisha mazungumzo na beki wa kushoto mmwaga maji wa Al Hilal, Ibrahim Imoro anayesifika kwa kukaba na kupandisha timu na kupiga krosi za maana kwa washambuliaji.
.
Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kinasema beki huyo Mghana [emoji1110] anatakiwa kutua Msimbazi ili kuja kusaidiana na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye kwa muda mrefu hana mbadala kikosini katika eneo hilo la kushoto.
.
Imoro anayemudu pia kucheza kama winga wa kushoto, kwa sasa yupo huru baada ya kuvunja mkataba na Al Hilal iliyomsajili Agosti 5, 2022 kutoka Asante Kotoko ya Ghana tangu Julai mwaka jana na tayari ameshaanza mazungumzo na mabosi wa Msimbazi ili aje kuitumikia msimu ujao.
.
Mghana huyo mwenye umri wa miaka 24 amewahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji aliyeasisti mabao mengi katika Ligi ya Ghana msimu wa 2021-2022 akitoa pasi tisa, pia ametwaa mataji zaidi ya manne ikiwamo la Ligi Kuu Ghana akiwa na Asante Kotoko msimu wa 2021-2022 na Kombe la Rais (Ghana) 2019 na taji la Sudan Super Cup 2022 akiwa na Al Hilal.
Screenshot_20240325_222049_InstaPro%20.jpg
 
[emoji599] Habari kutoka chanzo cha ndani ya Yanga kimesema nyota wanne, Pacome Zouzoua (Ivory Coast), Stephane Aziz KI (Burkina Faso), Kennedy Musonda (Zambia) na Djigui Diara (Mali) wanatarajiwa kuingia nchini Jumatano kujiunga na wenzao kwa ajili ya mechi na Mamelodi.
Screenshot_20240325_222151_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom