Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mtoto wa mwaka mmoja na miezi nane amefariki dunia kwa kuungua na moto baada ya mama yake mzazi kumuacha ndani kukiwa na jiko la mkaa lenyewe moto.

Tukio hilo limetokea Machi 25, 2024 katika mtaa wa Igangidung'u uliopo Kata ya Kivavi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 26, 2024 mama wa mtoto huyo Anna Mabiki (28) amesema alimuacha ndani akiwa amelala kwenye kochi na kwenda kupokea mafuta ya kupikia barabarani kwa dereva bodaboda ambaye hakupafahamu nyumbani kwake.

Amesema baada ya kuchukua hayo mafuta na kurudi nyumbani, ndipo alikutana na janga hilo la moto ambao uliondoa maisha ya mtoto wake huyo.

"Niliagiza mtu aniletee mafuta kule chini hapa kwangu hapafahamu akataka tukutane barabarani, lakini wakati ananikabidhi mafuta nageuka nyuma nyumbani kuna moto tukaanza kukimbia na yule kaka kuja kumuokoa mwanangu" amesema Anna.

Screenshot_20240326_225150_InstaPro%20.jpg
 
Mohamed Omary, mkazi wa Kimamba A wilayani Kilosa amefikishwa mahakamani katika mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro na kusomewa mshtaka manne likiwemo mauaji na ubakaji.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Renatus Barabara, mwendesha mashtaka wa Serikali, Elizabeth Malya, amesema kesi namba 8108/2024 inahusu mtuhumiwa kumuua mpenzi wake, Beatrice Ngongolwa.

Katika kesi namba 8101/2024 mshatakiwa kwa nyakati tofauti anadaiwa kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto wa marehemu mwenye miaka 9 kuanzia Aprili 2023 hadi Machi 2024, ambapo alimjeruhi kwa kumng’oa meno mawili, kumchoma kwa kutumia kifaa chenye moto mapajani, kumchoma kwa misumari pamoja na kumpiga rungu kichwani.

Kesi ya mauaji namba 8108/2024, Elizabeth amesema mshtakiwa anadaiwa kumuua mke wake Beatrice Ngongolwa Januari Mosi mwaka 2024 na kumfukia ndani ya chumba chake.

Kwenye shtaka hilo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Shtaka la ubakaji namba 1112/2024 Mstakiwa anadaiwa kumbaka mtoto wa kike wa marehemu mwenye miaka 12 kinyume cha sheria.

Shauri namba 8113/2024 mshtakiwa anadaiwa kumfanyia ukatili mtoto wa kiume wa marehemu mwenye miaka tisa ambapo alimng’oa meno, kumchoma mdomo na makalio na kumtengua kiwiko na kumtoboa kwa misumari sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa huyo amekana mashtaka mawili ya ukatili na ubakaji. Amerudishwa rumande mpaka Machi 28, ambapo shtaka la ukatili na ubakaji litakapotajwa tena, huku lile la mauaji likipangwa kutajwa tena Aprili 9 mwaka huu.
Screenshot_20240326_225307_InstaPro%20.jpg
 
Aliyewahi kuwa beki wa Barcelona ya Hispania, Dani Alves ameachiwa huru baada ya kukaa gerezani kwa siku chache.
Alves alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu lakini leo ameachiwa baada ya kulipa dhamana aliyotakiwa ya Pauni 850,000 zaidi ya Sh2.7 bilioni za Kitanzania.

Awali beki huyo wa zamani wa Brazil alitakiwa kutoka jana, lakini baba mzazi wa Neymar ambaye alikuwa akitajwa kuwa anakwenda kumlipia fedha hizo, hakutokea.

Pamoja na waandishi wengi kujaa nje ya gereza hilo, Alves alitoka akitembea haraka akiwa ameandamana na mwanasheria wake, Ines Guardiola na kwenda kupanda gari lililoandaliwa kwa ajili yake na kuondoka eneo hilo.

Hata hivyo, Alves ni kama atakuwa kwenye kifungo cha nje, baada ya kutakiwa kuwasilisha hati zake zote za kusafiria ya Brazil na Hispania na hataruhusiwa kutoka nje ya Hispania kwa kipindi chote atakachokuwa nje.

Staa huyo aliambiwa anaweza kutoka kwenye gereza la Brians 2 lililopo karibu ya Barcelona, Jumatano iliyopita baada ya kushinda rufani yake kwamba kifungo hicho cha miaka minne anaweza kwenda kukitumikia nyumbani badala ya ndani ya gereza.

Hata hivyo, alitakiwa kulipa dhamana, ambayo aliikosa na kulazimika kubaki gerezani hadi alipotoka leo.
Screenshot_20240326_225448_InstaPro%20.jpg
 
Maduka muhimu ya dawa 78 katika mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera yamebainika kuwa na dawa na vifaatiba visivyoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka hayo.

Maduka hayo pia yamekutwa yakiuza dawa za Serikali kinyume na sheria zote zikiwa na thamani ya Sh12.7 milioni.

Kukamatwa kwa dawa hizo kumetokana na ukaguzi uliofanywa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya ziwa magharibi kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Februari 2024 ambapo maduka 600 yalikaguliwa na 78 kati yake yalibainika kuwa na dawa zisizostahili kuuzwa kwenye maduka muhimu ya dawa.

Meneja wa TMDA kanda ya Ziwa Magharibi, Edga Mahundi ameyasema hayo leo Jumanne Machi 24, 2024 wakati alipokuwa akikabidhi dawa hizo kwenye Magereza ya wafungwa na mahabusu ya Wilaya ya Chato.

“Ukaguzi tuliofanya tumebaini uwepo wa dawa na vifaa tiba vilivyopo madukani kinyume na sheria ya dawa na vifaa tiba sura namba 219 na tumezipima bado zinafaa kwa matumizi ya binadamu lakini pia tulibaini dawa za Serikali zikiwa kwenye maduka binafsi.

“Kwa mujibu wa sheria tulitakiwa kuzitoa na kuzimiliki sisi sio watumiaji na ndio maana tumezileta Magereza ziwasaidie wafungwa na mahabusu na wagonjwa wanaohudumiwa kwenye zahanati hii, ”amesema Mahundi.
Screenshot_20240326_225558_InstaPro%20.jpg
 
According to reports, #Diddy’s electronic devices have been seized by federal agents after the Department of Homeland Security raided his homes in Los Angeles and Miami.
______________________________________

Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali, Vifaa Vya Mawasiliano Vya #Diddy Ikiwemo (Simu, Laptop, Tablet N.k) Vilivyokutwa Nyumbani Kwake Vimekamatwa Na Maafisa Usalama Kwa Ajili Ya Uchunguzi. Hii Ni Baada Ya Polisi Kuvamia Nyumba Zake Za L.A & Miami Wakimsaka Rapa Huyo Anayekabiliwa Na Kesi Za Unyanyasaji Wa Kingono

Awali ripoti zilisema kwamba Diddy Amekimbilia Visiwa vya Caribbean Na Ndege Yake Binafsi, Lakini Baadae Tovuti Ya TMZ Ilithibitisha Kwamba Rapa Huyo Hakuwepo Katika Ndege Hiyo Ikiwa Ni Baada Ya Diddy Kuonekana Uwanja Wa Ndege Wa Miami "Opa-Locka Executive"
Screenshot_20240326_230934_InstaPro%20.jpg
 
Nyumbani Kwa Diddy Hapakaliki Tena, Watoto Wamekimbia !!

Watoto Wa #Diddy ‘King Na Justin’ Ambao Walifungwa Pingu Na Maafisa Usalama Wakati Polisi Walipovamia Nyumba Yao Ya Los Angeles Jana Wameachiwa Huru

Chakushangaza Ni Kwamba Watoto Hao Walinaswa Na Paparazzi Waliporudi Nyumbani, Ambapo Walionekana Wakifungasha Virago Vyao Kwa Haraka Na Kuondoka Nyumbani Kwao !!!

Kumbuka Tu Kwamba Jana Nyumba Za Diddy Zilivamiwa Na Polisi Kwa Kile Kilichotajwa Kuwa Ni Zoezi La upelelezi dhidi ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono ambayo yanamkabili Rapa Huyo Tangu mwaka jana.
Screenshot_20240327_015135_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom