Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Goodluck Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati.

Kabla ya uteuzi huo, Shirima alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria na uhusiano wa kampuni ya Puma.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Ijumaa Aprili 12, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Screenshot_20240412_233130_InstaPro%20.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, imelitaifisha gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 iliyotumika kuwasafisha wahamiaji haramu 16 na kuwa mali ya Serikali, baada ya washtakiwa hao kukiri kosa hilo.

Pia imewahukumu washtakiwa hao 16, raia wa Ethiopia adhabu ya kulipa faini ya Sh500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Washtakiwa hao wameshindwa kulipa faini hiyo, hivyo wamepelekwa gerezani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa April 12, 2024 na Hakimu Mkazi wa Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo, baada ya kukiri kutenda kosa hilo.

Waethiopia hao walitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Idara ya Uhamiaji, Aprili 6, 2024 wakati wanapita Tanzania, huku wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8.

Screenshot_20240412_233306_InstaPro%20.jpg
 
Kuanzia leo saa 3:00 usiku, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mikoa nane itashuhudia mvua kubwa.

Mikoa hiyo ambayo maeneo machache yatashuhudia mvua kubwa ni Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa hiyo ya TMA imetolewa leo Aprili 12, 2024 na tayari mamlaka hiyo imeshatabiri uwepo wa mvua kubwa kwa mikoa 14 kwa siku tano kuanzia jana.

“Upepo mkali unaozidi kasi ya km 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili vinatarajiwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi Mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba,” imeeleza taarifa hiyo.
Screenshot_20240412_233357_InstaPro%20.jpg
 
Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60, mkazi wa Kitongoji cha Ipapa kilichopo Kijiji Cha Isongole, Wilaya ya Ileje mkoani Songwe amefukuzwa kijijini hapo na wananchi akituhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina.

Wananchi hao wamefikia hatua hiyo baada ya kumkuta mwanamke huyo kwenye nyumba ya jirani yake akiwa hajavaa nguo, jambo lililoibua hisia kwamba alikuwa akifanya imani za kishirikina.

Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Aprili 12, 2024 kuhusu tukio hilo lililotokea saa nane usiku, baadhi ya wananchi wamesema mwanamke huyo amekuwa akituhumiwa kwa imani za kishirikina kwa kuwaroga majirani na kuharibu vitu vyao kishirikina kama vile mazao na mifugo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Nelbati Kasekwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewapongeza wananchi kwa kutojichukulia sheria mkononi, hivyo mtuhumiwa yuko salama chini ya ulinzi wa balozi wa eneo husika.

Baada ya Jeshi la Polisi, kituo cha Itumba kupata taarifa hizo, limefika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa kwenda naye kituo cha polisi kwa usalama zaidi.

Screenshot_20240412_233457_InstaPro%20.jpg
 
Pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu za kusaka uongozi katika kanda nne za kiuongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), linafunguliwa rasmi leo Ijumaa Aprili 12 hadi 22, saa 10 alasiri.

Nafasi zinazowaniwa ni mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kanda, mweka hazina na katibu wa kanda. Kanda hizo ni Victoria, Magharibi, Nyasa na Serengeti zinazounda mikoa ya Mwanza, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Njombe, Mara, Rukwa, Katavi, Tabora, Songwe na Kigoma.

Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi lililotolewa leo Ijumaa Aprili 12, 2024 na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Benson Kigaila limeeleza kuwa fomu za kuwania nafasi hizo zitapatikana kwa makatibu wa mikoa na tovuti ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Miongoni wa vigogo wanaotajwa kuchukua fomu ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' atakayechuana na Mchungaji Peter Msigwa anayetetea uenyekiti wa kanda ya Nyasa. Wengine ni mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu atakayekabiliana na Ezekiah Wenje katika Kanda ya Victoria.

Screenshot_20240412_233548_InstaPro%20.jpg
 
Miili sita ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ghati Memorial iliyopo Murieti jijini Arusha kati ya saba wanaohofiwa kufa maji imepatikana katika maeneo tofauti.

Miii hiyo imepatikana kwa msaada wa uokozi unaofanywa na Jeshi la Zimamoto, Polisi kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya pamoja na wananchi.

Wanafunzi hao wamefariki dunia leo Aprili 12, 2024 baada ya gari la shule waliokuwemo kuangukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo mkoani Arusha, saa 12 asubuhi ya leo.
Screenshot_20240412_233636_InstaPro%20.jpg
 
Baadhi ya wenza wa viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada ya misa maalumu ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Sokoine.

Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa hayati Sokoine, Monduli Juu mkoani Arusha, leo Ijumaa, Aprili 12, 2024.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Screenshot_20240412_233733_InstaPro%20.jpg
 
“Upungufu wa nguvu za kiume au za kike sio ugonjwa, bali ni dalili kuwa kuna kasoro katika mfumo wako wa mwili pamoja na ubongo,” ndivyo anavyoanza kusema mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dk Ali Mzige.

Anasema changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume huwakumba wanaume wengi, hali inayowafanya wasake matibabu kila kona, wakiamini matumizi ya dawa za viwandani, mitishamba na ulaji wa baadhi ya vyakula kama supu ya pweza, vumbi la Congo, alkasusu ni suluhisho.

Daktari huyo ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na kustaafu mwaka 2005 amesema chanzo kingine ni ‘michepuko’, lishe duni, kutokufanya mazoezi ya mwili na viungo kubweteka.

Screenshot_20240412_233837_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom