Makapuku Forum

Makapuku Forum

Zaidi ya Watanzania 7,200,000, sawa na asilimia 12, wanaugua ugonjwa wa pumu unaoathiri mfumo wa upumuaji, huku wengi wao wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka 16, Wizara ya Afya imebainisha.

Pumu unakuwa ugonjwa wa pili kuwaathiri zaidi Watanzania baada ya shinikizo la juu la damu linaloathiri asilimia 26 ya watu wazima.

Akizungumza Februari mwaka huu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema pumu ni miongoni mwa magonjwa ya mfumo wa upumuaji, ambayo kwa takwimu za mwaka 2013, maambukizi yaliongoza kuwaathiri Watanzania 4,901,844, sawa na asilimia 18.9.

Screenshot_20240507_221200_InstaPro%20.jpg
 
Refa Beida Dahane ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika kusimamia teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR) katika mechi ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Esperance na Al Ahly itakayochezwa Tunis, Tunisia, Mei 18.

Jina la Dahane limekuwa maarufu nchini tangu alipochezesha mechi ya marudiano baina ya Mamelodi Sundowns na Yanga iliyochezwa Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 5.

Katika mechi hiyo, Dahane alitoa uamuzi uliozua mjadala baada ya kutoamuru mpira uliopigwa na Stephane Aziz Ki kuwa bao licha ya kuonekana ulivuka mstari na kuingia golini.

Katika mechi hiyo ya kwanza ya fainali, refa wa kati atakuwa ni Mustapha Ghobal kutoka Algeria.

Katika uteuzi huo wa Caf, mechi ya marudiano ambayo imepangwa kuchezwa jijini, Cairo, Mei 25, refa wa kati atakuwa ni Jean Jacques Ndala kutoka DR Congo.
Screenshot_20240507_221301_InstaPro%20.jpg
 
Serikali imetenga kiasi cha Tsh. bilioni 18.5 kwa ajili ya kuwawezesha Wajasiriamali Nchini zitakazotolewa kama mikopo yenye masharti nafuu kupitia Benki ya NMB (@nmbtanzania ).

Makubaliano ya utaratibu wa ufadhili huo yametiwa saini leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe kwa niaba ya Serikali na kushuhudiwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima.

Akiongea kabla ya utiaji saini ya mkataba huo wa miaka miwili, Waziri Gwajima amesema Wafanyabiashara wadogo na wa kati watakopeshwa fedha hizo kwa riba ya 7% “Tsh. bilioni 18.5 ni hela nyingi za kuanzia lakini kiasi hiki kitaongezeka kwani lengo la Serikali ni kuifanya mikopo hii kuwa endelevu ili iwafikide Watu wengi”

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema mkataba wa kutoa mikopo hiyo ni kielelezo cha jitihada kubwa zinazofanywa na benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya biashara kwa Wafanyabiashara wote Nchini wakiwemo wadogo.
Screenshot_20240507_221414_InstaPro%20.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela, Paulo John (23) Mkazi wa Mapea Magugu na Athumani Misanya (31) Mkazi wa Mamire baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kukutwa na nyara za Serikali ikiwemo kichwa cha Twiga.

Hukumu hiyo imetolewa leo May 07,2024 na Hakimu wa Mahakama hiyo, Victor Kimario baada ya kusikiliza hoja za pande zote.

Katika hukumu hiyo amesema amejiridhisha pasina kuacha shaka juu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri, hivyo kwa kuzingatia kuwa Wakosaji ni wa mara ya kwanza licha ya kuwa Vijana wadogo lakini wametumia nguvu zao vibaya kuihujumu Serikali hivyo amewahukumu kwenda Jela miaka 20 kila mmoja huku vifaa vilivyotumika kubebea nyara hizo(ndoo na pikipiki) vikitaifishwa huku haki ya kukata rufaa ikiwa wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Awali waendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Getrude Kariongi na Shaidu Kajwangya wakishirikiana na Wakili Mwanaidi Chuma wamesema washtakiwa hao wanadaiwa kutenda Kosa hilo 02/02/2024 katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge ambako walikutwa na kichwa cha Twiga, mkia, ngozi pamoja na nyama vikiwa kwenye ndoo huku wakitumia usafiri wa pikipiki ambapo thamani ya Twiga huyo ni zaidi ya shilingi Milioni 50, na hivyo wakaiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu ili kufikisha ujumbe kwa Jamii na watu wenye kufanya makosa ya ujangili ili kukomesha vitendo hivyo kwani Mnyama Twiga ni nembo ya Taifa lakini pia ni kivutio cha Utalii na kuiwezesha Nchi kupata Mapato.
Screenshot_20240507_221505_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom