Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Endapo Wakristo watalalamikia tume ya ukusanyaji maoni na kusema yanachakachuliwa kwa kuwa waislam ni wengi nitawaona wapuuzi.Mbona hawakuikataa wala kuweka shaka kwenye tume baada ya Rais Kikwete kuteua wajumbe? Mbona Mzee Mtei alipotilia shaka uwiano wa kidini kwa wajumbe wa tume hamkumuunga mkono? Hii inamaanisha kwamba malalamiko kama hayo yakitolewa ni ujinga na hata tume ikitathmini na kuona wananchi wengi waliitaka mahakama ya kadhi huo ndiyo utakuwa ukweli mtupu. Kama ni lawama tujibebeshe Wakristo wenyewe na siyo kuwatuhumu ndugu zetu Waislamu walioko kwenye tume kitu ambacho ni kujengeana chuki zisizo na maana. Tumsifu Yesu Kristo...Milele Amina.