Makato kwa utaratibu wa asilimia kwenye mishahara ya watumishi, ni utaratibu usiofaa; Kuwe na utaratibu wa kuomba kibali cha kuongeza makato hayo

Kubali kusahihishwa Mkuu, Makato ya CWT, TUGHE, TALGWU, TUICO nk ni hiari unaweza ukakatwa au ukakataa kukatwa na Endapo unakatwa makato hayo na hujawahi kujaza fomu ya Uanachama kukiri kukwata haya Makato, kesho nenda kwa mwajiri wako Uandike barua ya Ombi la kurejeshewa pesa yako na utaipata na msamaha juu.
Makato ya Lazima ni PAYE, NHIF, HESLB, PSSSF/NHIF baaaaasi. Mengine yooote kukatwa hadi ukubali na utie saini ya kuidhinisha mwajiri akate.
Wabongo huwa mna UJASIRI wa UBISHI.

Kujua HAMJUI lakini MNABISHANA Kama MATAAHIRA.

Nimekuuliza unaijua ADA YA UWAKAL??

======

Walimu 347 Kigoma ruksa kujitoa CWT​

TUME ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), imekubali ombi la walimu 347 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kujitoa kutoka katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ili kuanzisha chama kitakachotetea maslahi yao kutokana na madai kwamba chama hicho cha walimu hakikuwa na msaada kwao katika kutetea maslahi yao.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo mjini Kigoma, mwamuzi wa shauri hilo, L.L Mwakyusa alisema baada ya mlolongo mzima wa uamuzi wa pande zinazohusika, Tume imeamua kuwa walalamikaji si wanachama wa CWT tena na kitabaki kuwa wakala kwa walalamikaji kwa kuwa ni chama pekee kinachotambuliwa na mwajiri.

Aidha, Mwakyusa alisema suala la makato kwa walimu hao linapaswa kuangaliwa upya kwa kuwa pande hizo zimeshaingia kwenye mgogoro na kwamba walimu hao hawatafaidi matunda halisi kama wanachama.

Pamoja na uamuzi wa kujitoa kwa walimu hao na kujiunga na chama kingine, alisema walimu hao wataendelea kukatwa ada ya uwakala ili kufaidi matunda ya masuala ya jumla kama walimu yatakayosimamiwa na CWT kwa mujibu wa kifungu cha 72 (c) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya Mwaka 2004.

Akizungumzia hukumu hiyo, kiongozi wa kundi hilo la walimu, Kalimwabo Sabibi alisema pamoja na Tume hiyo kuridhia kujitoa CWT, wanakusudia kuanzisha chama kingine cha walimu kitakachosimamia maslahi yao.

Sabibi alisema kwa muda mrefu, walimu wamekuwa kama watoto yatima kutokana na CWT ambacho machoni kinaonekana kama kinasimamia maslahi yao, kudai hakifanyi chochote kwa ajili ya maslahi ya walimu.

Alisema walimu wamekuwa kwenye malumbano ya kudai maslahi yao kutoka kwa mwajiri badala ya chama hicho kuwa upande wao, wakati mwingine kimechangia kuwafanya wakose hata kile kidogo wanachodai.

Pamoja na hukumu hiyo, hata hivyo walimu hao wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa Tume kuruhusu kuendelea kukatwa kwa makato kutoka katika mishahara yao kwa ajili ya kuchangia CWT kwa kigezo cha ada ya uwakala wakati wao si wanachama wa chama hicho.
 
Hoja nzito hii mkuu! Makato ya NHIF yakiwa kwa asilimia, kadi za matibabu zitatofautiana?

10% ya 3,000,000 ni tofauti na 10% ya 720,000
 
Mtumishi awe huru kuingia na awe huru kujitoa na ammuue mwenye akatwe kiasi gani na isiwe lazima kuchangia kupitia mshahara.

Makato ya NHIF ni kwa asilimia.
 
PAYE yangu ni TZS 501,992/= yaani laki tano inapotea eti ni kodi.
Screenshot_20220904-134313.jpg
 
Mtumishi awe huru kuingia na awe huru kujitoa na ammuue mwenye akatwe kiasi gani na isiwe lazima kuchangia kupitia mshahara.

Makato ya NHIF ni kwa asilimia.
Sahihi. Waliweka huduma sawa kwa wote ila kiwango cha uchangiaji ni tofauti.

Vyama vya wafanyakazi, zaidi ya posho za vikao na zile bahasha wapewazo wakienda kwenye mabaraza, hawana tofauti na HRs, hawana msaada.

Skills Development Levy, hii si ni tozo tu? Inafanyaje kazi?

WCF, hii kwanini isingekuwa chini au tawi la masuala ya Afya na Usalama kazini?
 
Wabongo huwa mna UJASIRI wa UBISHI.

Kujua HAMJUI lakini MNABISHANA Kama MATAAHIRA.

Nimekuuliza unaijua ADA YA UWAKAL??

======

Walimu 347 Kigoma ruksa kujitoa CWT​

TUME ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), imekubali ombi la walimu 347 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kujitoa kutoka katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ili kuanzisha chama kitakachotetea maslahi yao kutokana na madai kwamba chama hicho cha walimu hakikuwa na msaada kwao katika kutetea maslahi yao.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo mjini Kigoma, mwamuzi wa shauri hilo, L.L Mwakyusa alisema baada ya mlolongo mzima wa uamuzi wa pande zinazohusika, Tume imeamua kuwa walalamikaji si wanachama wa CWT tena na kitabaki kuwa wakala kwa walalamikaji kwa kuwa ni chama pekee kinachotambuliwa na mwajiri.

Aidha, Mwakyusa alisema suala la makato kwa walimu hao linapaswa kuangaliwa upya kwa kuwa pande hizo zimeshaingia kwenye mgogoro na kwamba walimu hao hawatafaidi matunda halisi kama wanachama.

Pamoja na uamuzi wa kujitoa kwa walimu hao na kujiunga na chama kingine, alisema walimu hao wataendelea kukatwa ada ya uwakala ili kufaidi matunda ya masuala ya jumla kama walimu yatakayosimamiwa na CWT kwa mujibu wa kifungu cha 72 (c) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya Mwaka 2004.

Akizungumzia hukumu hiyo, kiongozi wa kundi hilo la walimu, Kalimwabo Sabibi alisema pamoja na Tume hiyo kuridhia kujitoa CWT, wanakusudia kuanzisha chama kingine cha walimu kitakachosimamia maslahi yao.

Sabibi alisema kwa muda mrefu, walimu wamekuwa kama watoto yatima kutokana na CWT ambacho machoni kinaonekana kama kinasimamia maslahi yao, kudai hakifanyi chochote kwa ajili ya maslahi ya walimu.

Alisema walimu wamekuwa kwenye malumbano ya kudai maslahi yao kutoka kwa mwajiri badala ya chama hicho kuwa upande wao, wakati mwingine kimechangia kuwafanya wakose hata kile kidogo wanachodai.

Pamoja na hukumu hiyo, hata hivyo walimu hao wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa Tume kuruhusu kuendelea kukatwa kwa makato kutoka katika mishahara yao kwa ajili ya kuchangia CWT kwa kigezo cha ada ya uwakala wakati wao si wanachama wa chama hicho.
Walimu wa kigoma ni wapambanaji sana mpaka wamefanikiwa kuanzisha chama kipya cha CHAKUHAWATA ambacho kinatakata kiasi cha tsh 5000 kwa kila mwanachama wake pasipo kujali mtu ana mshahara mkubwa kiasi gani ni mwendo wa flat rate .Zimebaki tu propaganda za cwt ooh mwl atakayejiondoa atakatwa mara mbili .Katavi cwt kwishaa
 
Hongera zao. Huu ni mfano wa kuigwa.
 
Serikali ilivyoweka katika sheria ya ajira na mahusiano kazini kwamba mwaajiriwa ana uhuru wa kujiondoa kwenye chama cha wafanyakazi alichojiunga kwa kupenda au kwa kuungwa kwa hila muda wowote ni jambo jema sana yy ni kujaza fomu namba 15 (TUF 15) na kujaza notice ya siku 15 na kupeleka kwa mwajiri wake ambaye anatakiwa kumuondoa kwenye chama asichokitaka ndani ya siku 7 baada ya muda wa notice wa siku 30 kwisha.
 
Kuna kitu ambacho naona mnashindwa kuelewa. Yaani hili suala hata uwaleleze watu vipi kuelewa hawataki.

Issue siyo kujiunga Wala kuijiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi.

Tatizo kubwa ni kwamba UWE MWANACHAMA au USIWE MWANACHAMA. Ujitoe kwenye vyama au usijitoe.

WATAKUKATA TU tena KIWANGO kile kile sawa na wanachama wao.

Sababu kubwa ni kwamba Sheria imewapa LOOPHOLE hiyo.

MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwanachama.

Na Kama wewe siyo MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwakala.
 
Hao cwt hata mh Magu aliwatilia wasiwasi kuhusu namna wanavyotumia kiasi cha bilioni 4 hadi 5 wanazovuna kila mwezi toka kwa walimu wenye mishahara isiyoweza hata kukidhi mahitaji yao.Kukata mshahara 2 asilimia ya mshahara ghafi kwa zaidi ya walimu 285000 ni makusanyo yake ni kufuru ukilinganisha na wakipatacho hao walimu kutoka huko cwt
 
Kuna kitu ambacho naona mnashindwa kuelewa. Yaani hili suala hata uwaleleze watu vipi kuelewa hawataki.

Issue siyo kujiunga Wala kuijiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi.

Tatizo kubwa ni kwamba UWE MWANACHAMA au USIWE MWANACHAMA. Ujitoe kwenye vyama au usijitoe.

WATAKUKATA TU tena KIWANGO kile kile sawa na wanachama wao.

Sababu kubwa ni kwamba Sheria imewapa LOOPHOLE hiyo.

MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwanachama.

Na Kama wewe siyo MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwakala.
Ni kweli lakini mtumishi ambaye ni smart enough hilo anaweza kusave kiasi kikubwa cha fedha kwa kujiondoa chama A na kwenda chama B kwa sababu viwango vya makato ya uanachama sio uniform .kwa maana hiyo mtumishi anachagua yy mwenyew mshahara wake ukatwe kwa asilimia ngapi au kiasi cha shilingi ngapi?
 
Vyama vyote vya wafanyakazi vilivyoko chini ya TUCTA vinakata 2%.

Walimu ndio wamepambana Sana kuanzisha vyama vyao wenyewe kwaajili ya makato madogo.
- CHAKUHAWATA ( Tsh 5000 ) flat rate.

- CHAKAMWATA ( 1% ) Ila hiki kimeshapigwa Vita nadhani kinapumulia mashine Sasa hivi.

Hakuna chama kingine kinachokata pungufu.
 
Kuna kitu ambacho naona mnashindwa kuelewa. Yaani hili suala hata uwaleleze watu vipi kuelewa hawataki.

Issue siyo kujiunga Wala kuijiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi.

Tatizo kubwa ni kwamba UWE MWANACHAMA au USIWE MWANACHAMA. Ujitoe kwenye vyama au usijitoe.

WATAKUKATA TU tena KIWANGO kile kile sawa na wanachama wao.

Sababu kubwa ni kwamba Sheria imewapa LOOPHOLE hiyo.

MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwanachama.

Na Kama wewe siyo MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwakala.
Kwahiyo ukiwa mwanachama unakatwa mara mbili hiyo ya uanachama na hiyo ya uwakala?.Na kazi ya hiyo ya uwakala ni ipi maana siioni kwenye vyama vingine.
 
Wakikuunga kutoka ni ngumu mfano cwt kutoka ni ngumu na walimu wengi wanatamani kutoka
 
Ipo kila chama.

Makato ni yale yale. Ila MWANACHAMA atanufaika zaidi Kama utetezi, uongozi n.k.

Suala la kukatwa au kuachwa linategemeana pia na siasa na ulaji wa waajiri.

Unakuta Afisa Utumishi au DHRO kapewa kinafsi huko kwenye vyama, kwahiyo anawaingiza kwenye makato kibabe maana Sheria inawapa mwanya huo.

Mfano, Walimu ni wachache Sana wamejiunga CWT lakini kama.kuna Walimu hawakatwi basi ni 1% tu.
 
Wakikuunga kutoka ni ngumu mfano cwt kutoka ni ngumu na walimu wengi wanatamani kutoka
Si ngumu ukifuata utaratibu kama sheria inavyotaka ya kujaza fomu namba 15 na ukaandika notice ya siku 30 na nakala yake ukaipeleka kwa katibu wako wa wilaya kwa kuituma posta kwa EMS na derivery note ya posta ukaambatanisha na kuipeleka kwa mwajiri wako mwaajiri wako kwa kumtumia HR wako sheria inamtaka akutoe usikotaka ndani ya siku 7 baada ya muda wa notice
 
Ni makato ya hiari ya lazima. Yaani ukikataa kuwa mwanachama wao wanakata kitu wanaita agency fee. Ni aslimia hiyohiyo.
Hiyo ni kulazimishana haijakaa sawa.

Serikali iangalie upya. Mtu akikataa kuwa mwanachama basi asikatwe hela yake
Uwongo kabisa mimi nilikataa kujaza form mpaka leo sijawahi katwa ni hiari kwani huwa wananibebembeleza sana ila sitaki kabisa kusikia
 
Back
Top Bottom