Makato kwa utaratibu wa asilimia kwenye mishahara ya watumishi, ni utaratibu usiofaa; Kuwe na utaratibu wa kuomba kibali cha kuongeza makato hayo

Makato kwa utaratibu wa asilimia kwenye mishahara ya watumishi, ni utaratibu usiofaa; Kuwe na utaratibu wa kuomba kibali cha kuongeza makato hayo

Kuna kitu ambacho naona mnashindwa kuelewa. Yaani hili suala hata uwaleleze watu vipi kuelewa hawataki.

Issue siyo kujiunga Wala kuijiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi.

Tatizo kubwa ni kwamba UWE MWANACHAMA au USIWE MWANACHAMA. Ujitoe kwenye vyama au usijitoe.

WATAKUKATA TU tena KIWANGO kile kile sawa na wanachama wao.

Sababu kubwa ni kwamba Sheria imewapa LOOPHOLE hiyo.

MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwanachama.

Na Kama wewe siyo MWANACHAMA atakatwa Ada ya uwakala.
Uwongo mkubwa huu mbona mimi sikatwi? Huo uwakala?
 
Tughe ,taasisi ya serikali
Taasisis zina unafuu. Huku halmashauri waajiri ( Maafisa Utumishi na Maafisa Raslimali watu Wilaya wako wanavyeo huko kwenye vyama. Kwahiyo wanakula nao, hakuna namna mtumishi atakwepa, unless Kama Sheria itakuja kubadikika.
 
Sahihi. Waliweka huduma sawa kwa wote ila kiwango cha uchangiaji ni tofauti.

Vyama vya wafanyakazi, zaidi ya posho za vikao na zile bahasha wapewazo wakienda kwenye mabaraza, hawana tofauti na HRs, hawana msaada.

Skills Development Levy, hii si ni tozo tu? Inafanyaje kazi?

WCF, hii kwanini isingekuwa chini au tawi la masuala ya Afya na Usalama kazini?
Wizi mtupu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kubali kusahihishwa Mkuu, Makato ya CWT, TUGHE, TALGWU, TUICO nk ni hiari unaweza ukakatwa au ukakataa kukatwa na Endapo unakatwa makato hayo na hujawahi kujaza fomu ya Uanachama kukiri kukwata haya Makato, kesho nenda kwa mwajiri wako Uandike barua ya Ombi la kurejeshewa pesa yako na utaipata na msamaha juu.
Makato ya Lazima ni PAYE, NHIF, HESLB, PSSSF/NHIF baaaaasi. Mengine yooote kukatwa hadi ukubali na utie saini ya kuidhinisha mwajiri akate.
Ms3ng3 wewe
 
Basic Salary ya Tsh 2,442,000 unawezaje kuishi ndugu? Huna mke na watoto? Wanaishije? Watoto wanasoma KAYUMBA?
Hivyo basic serikalini ni kubwa mno hivyo huyu ana nafuu sana.

Najua umefanya hesabu kupata hiyo basic kwasababu inajulikana PSSSF ni asilimia 5 ya basic hivyo utakuwa umetafuta x na uko sahihi kabisa.
 
Hili ni wazo la Msingi sana
Inatakiwa walau makato kwa watumishi yaangaliwe
Badala kukata kwa asilimia yaanze kukata kwa amount fulani
NIimepata taarifa kuwa kuna chama kipya cha walimu kimeanzishwa kinakata flat rate shilingi 5000 tu na walimu wengi wanajitoa CWT na kujiunga na hicho chama kipya cha walimu.
 
Back
Top Bottom