Makato kwenye mshahara

Makato kwenye mshahara

Nyamanoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
651
Reaction score
518
Nauliza wajuzi wa sheria ili nipate ufafanuzi juu ya kifungu namba 28 kifungu kidogo cha 1 na cha 2 cha sheria ya Ajira na Uhusianao kazini namba 6 ya 2004 kinachozungumzia suala la makato kwenye mshahara wa mfanyakazi.

Je ni sahihi mfanyakazi anayelipwa mshahara kwa mwezi (ambaye si kibarua) anapokosa kufika kazini kwa siku moja au mbili mfano kukatwa fedha siku hizo ambazo hakufika kazini?

Nimejaribu kusoma kifungu hicho lakini sikupata jibu au suala hilo linashughulikiwa na sheria nyingine?

Asante.
 
Mkataba wa ajira unasema ajira ni ya kudumu, malipo ya mshahara ni kwa mwezi pamoja na michango ya hifadhi ya jamii inakatwa.

We achana nao, japo inauma lakini wala usivutane nao! Waachie kazi yao!
 
Unatakiwa kupewa onyo kama tabia ikiendelea mwajiri anaweza kukulipa nusu mshajara wakati kesi ya msingi ikiendelea lkn haya yote lazima uwe na onyo la kawaida,kalipip kali tena kwa barua.Kukatwa mshahara mpa swala hilo liwe ngazi za juu siyo bosi kuamua.
 
Hakuja bila taharifa,au katoa taharifa na kazidi siku nne alizopewa kisheria
analipwa kwa Pro rata. Kama inaathiri uzalishaji wa muajili wake, atamuita kwenye kikao cha nidhamu na kuchukua hatua dhidi yake ikiwepo kumuachisha kazi.
 
Mwajili alipewa taarifa kwa njia ya simu,hakukubaliana nayo kwa madai kuwa haikuwa official(ilikuwa dharura ya ugonjwa,mgonjwa hakuweza kufika offisini,pamoja na kuonyeshwa cheti mwajiri kang'ang'ania tu ruhusa haikuwepo). hakukuwa na hathari zozote za kiuzalishaji kwa kuwa ni office ya kawaida na si kiwanda cha uzalishaji na hasara ya kifedha haikuwepo kabisa, ndio maana swali linakuja kuwa mwajiri anaweza vipi ku justify deductions?
 
Back
Top Bottom