Makato na tozo yamefika pabaya, wahusika fanyeni hima mrekebishe hali

Mkuu tafuta njia mbadala nadala ya kuendelea kutumia miamala ambayo inaumiza mfuko wako. Serikali hii ina dharau kubwa sana kwa Watanzania. Wakati sasa umefika wa kupambana bila ya kumwaga damu. Hakikisha mapato ya Serikali yanapungua kwa kiasi chochote kile uwezacho.
 
Kama ni kodi za dhulma, hapana! - Mama Samia Suluhu.

Mwambieni Samia wananchi wanadhulumiwa huku - left, right and center. Leo nimemtumia mtu TZS. 65,000 kutoka CRDB Kutumia SimBanking app. Kucheck wamelamba service charge TZS. 5,307. Sijui yeye wakati anaitoa watakula ngapi. Ni Makato tu mwanzo mwisho
 
Kuwa mzalendo,viongozi wetu wanahitaji magari mazuri,malazi safi,matibabu,familia zao zile vizuri ili waweze kutuletea maendeleo
 
hebu niambie ukitaka kutoa hela bank kwa njia ya sim umtumie ili akanunue umeme wa luku (labda 10,000) hiyo hela itakatwa mara ngapi??
Mheshimiwa utakatwa unapotòa na kutuma pesa, lakin kwenye Luku pia utakatwa Eura ya Rea
 
Airtel naona bado naingia bure ila kwa mwendo huu siyo muda nako watakula kichwa but kwanini kuingia gharama zote hizi twendeni kwenye ma-ATM tu.

Mimi sasa hivi ikipunguwa million naingia kwenye machine hata elfu 50 mambo ya M-pesa sijui Airtel money nimeshaachana nayo na ikizidi million naingia kwenye teller ndiyo maisha waliyotuchagulia tutafanyaje?
 
Kuna watu hawatakuelewa,inashangaza hata huku mitaani wale wanaoonekana hela ndogo ndogo haziwasumbui nao wanalalamika nashangaa wanaoshadadia huu ujinga humu mitandaoni wanaishi Tanzania ipi!!!
 

Hapana mkuu. Serikali inahitaji pesa. Ingependeza kuongeza masurufu zaidi hasa kwa vigogo. Pesa itoke wapi sasa?

Serikali ongeza tozo tafadhali. Kwanza Mwigulu alisema tutakuwa na pesa nyingi sana hivyo kulipa vimalipo vidogo wala haitakuwa shida.
 
Wanatuibia bila kutuhurumia,CCM ni janga la Taifa.
 
Wafungue macho, wanaua biashara za watu na hata hayo mapato ya kodi yataishia kupungua kuliko kuongezeka, akili za matope tupu hawa
 
Hii tozo inatuumiza sana majuzi nlienda kutoa laki moja kupitia tigo pesa jumla ya makato nakuta elfu 6 na mashilling mbele wakat mwanzo ilikuwa elfu 2 na mia 7 dah
 
Eeeh hizi tozo ss ni umekuwa ni mtihani mkubwa Sana Yani. Hii serikali hii jmn, inajali mitumbo yao tuu
 
MAMA KAWAACHIA WAHUNI WAVIVU WALIOVIMBIWA KUFIKIRIA, WAMSAIDIE VYANZO VYA MAPATO. WAHUNI UKU WAKIWA NA BAKURI LA POP CORN WANABUGIA WAKAMWAMBIA " VIZIA WANANCHI, WAKITUMIANA TU PESA , KWAPUA HAPO HAPO" BASI MASIHARA MASIHARA NDIO IMEKUWA MTINDO SASA
 
Sasa tunaenda mbele au tunarudi nyuma? Teknolojia ipo ili kurahisisha na kuokoa muda.

Nachelea kusema hatuna viongozi wenye maono
Jack Ma wa alibaba....alisema ukiona biashara inaanza kufuatiliwa na serikali uza biashara hiyo anzisha nyingine ! Hapa dawa ni kuanzisha biashara huko Mars na wale Aliens!
 
Tafta pesa mkuu Tozo sio kubwa namna hio nafikiri waongeze kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…