Make up 8 wanawake zinazowachefua wanaume

Make up 8 wanawake zinazowachefua wanaume

Kuandika kila mtu anaweza. . . . huko mtaani mnawaambia? Au mnaishia kucheka cheka na kusifia?

Ya mitaani bora tuwaachie maana itaonekana kuingilia uhuru wa mtu binafsi. Jamii zina njia nyingi tu za kukosoa, kuonya na kutahadharisha kupitia njia mbalimbali tangu historia ya mababu zetu.

Katika tamaduni mbalimbali kumekuwa na ngoma za asili, na ukigundua nyimbo zao zilikuwa za kukosoa, kumsema fulani aliyetenda jambo ambalo si la wakaida iwe zuri au baya. Tathmini ya kizazi cha leo ni zaidi ya muziki pia kuna vyombo vya habari kama magazeti, TV na radio ambavyo hutoa michango mikubwa katika kujenga jamii.

Wananchi wenyewe wana nafasi ya kujifunza kutokana na vyombo mbalimbali vinavyousia, wasanii mbalimbali wanavyoonya na kushauri, si kusubiri mpaka mtu akunyoshee kidole kuonyesha upungufu wa kutokuwa na hulka ya kujitambua.

Nakumbuka wiki hii kuna picha fulani ya msanii wa taarabu kutoka kule Zenj alivyoshambuliwa pale jukwaa la picha, ingawa naweza kumjengea utetezi wa kwamba alikuwa na maana ya kuwa mzuka jukwaani kurusha juu juu mioyo ya wapenzi wake wa muziki, lakini ujumbe wa wengi wasivyopendezwa na too much make up ile anaweza kujifunza na kufanya masahihisho kupunguza kilichozidi aonekane kama kavaa mask.
 
Makeup nzuri ni ile mtu hawezi note. Huyu karundika hasa, ila it blends well. Unless uone before and after, huwezi jua ni kazi gani imefanyika.
2011-09-07-2.jpg

This is good! Bravo
 
images

Umeanika ukweli, maana wanawake wengi wanafikiri makeup ndio mvuto, na kupenda kusifiwa wakati hawatambui sifa zinazomwagwa na wanaume juu ya make up ya mwamake ni saikoloji tu kwa vile wanaume tunajua wanaofanya make up wanafikiria kuonekana wazuri zaidi, kumbe ndio wanajiumbua zaidi.

Natural is really beautiful. Watu hatupendi ile kitu ya kujipaka then baada ya dakika unabadilika kuonekana tofauti na ulivyo kuwa, bora kubaki na mwonekano wa kawaida ambao ndio natural beauty yako na hutashangawa na wanaokuona muda wote kwa vile ndo mwonekano wako ulivyo, kuliko huu wa too much make up kisha unachujuka ghafla, kulikoni?

Vipodozi ni hulka ya kawaida kwa mwanamke ile iwe kwa kiasi ili kulinda ule mwonekano wa natural beauty.

Hawa mahiri wa majukwaa ni kitu kingine maana wapo jukwaani anataka kuwazingua watazamaji aonekane mzuka usio wa kawaida ili kuamsha hamasa ya onyesho lake, lakini wengine ndio wanaiga ili kuonekana mitaani na makazini, matatizo ndio yapojitokeza kutojua maana na nafasi ya nani na wapi wanafanya hivyo na kwa ajili ya nini na nani.
Yeahhh ikizidi kweli inapoteza mvuto halisi.
Ila tuacheni tuwe tunajiremba walau kidogo. . .
 
Uzuri ni a kuzaliwa .
Naomba Wadau watuwekee hapa Wimbo MAYASA wa Jabali la Muziki Marijani Rajabu.
 
Lizzy, kuna ex colleague wangu fulani (wa kike) alinambia kua wanawake wanajiremba to impress other women because men don't know about makeup anyway. Unadhani ni kweli?
(she was refering to zile makeup tooooo obvious, sio discrete).
Mi sio Lizzy, lakini observation hii nakubaliana nayo kwa asilimia zote
 
Watu wengi hudhani kwamba wanawake hujipendezesha kwa ajili ya wanaume tu kwa kiasi kikubwa sio kweli.

......lakini kama unajipendezesha halafu ukamuuliza Mume, Boyfriend au hata rafiki wa kiume au hata wa kike kwamba, "Nimependeza?" naye akakwambia hujapendeza bali unaonekana kituko, je kuna ubaya kusikiliza/kufuata ushauri wa huyo uliyemuuliza bila kujali kwamba wanawake hawajipendezeshi kwa ajili ya Wanaume?


 
Kuandika kila mtu anaweza. . . . huko mtaani mnawaambia? Au mnaishia kucheka cheka na kusifia?

we lizzy wewe, Acha tu. Nishajaribu kumwambia mdada mmoja hivi kwenye Daladala,alikuwa kanidondoshea lipstick kwenye shati langu matusi niliyoambulia sintoyasahau. Ilinibidi nishukie kituo kisicho changu, tena mvua ikiwa kali balaa
 
huwa nawaambia sana coz sipendi hiyo mambo...na nitaendelea kusema mnatutia KICHEFUCHEFU

Hongera kwa hilo.
Ila sidhani kama wanawatia vichefuchefu. . . maana ingekua kweli mngekua mnatapika kutwa mara kumi!!
 
we lizzy wewe, Acha tu. Nishajaribu kumwambia mdada mmoja hivi kwenye Daladala,alikuwa kanidondoshea lipstick kwenye shati langu matusi niliyoambulia sintoyasahau. Ilinibidi nishukie kituo kisicho changu, tena mvua ikiwa kali balaa

Hahahahahaha. . . . pole Speedy (jina lako limenikumbusha mbali. . asante kwa hilo).
Nwy inategemea ulivyomwambia. . .labda alihisi umemdharau.
 
Hehehe, babaake, kuna wanaume wengine wana-discourage vitu shauri ya wivu tu. Kuna wanaume wako over-possessive hataki mwanamke wake avae sarawili, kimino, makeup etc. Muhimu ni mwanamke kufanya vitu for herself. Kama mtu yuko comfortable ajifantie tu. Tatizo letu waswahili vipodozi feki, foundation tsh 3000 na angel face sh 500! Mtu akipaka sura kama anachungulia! Mi nikikutana na mdada nikishamuangalia uso tu lazma nimuangalie miguuni. Inasikitishaga jamani! Urembo uandamane na pedicure na manicure ili kuleta balance!
......lakini kama unajipendezesha halafu ukamuuliza Mume, Boyfriend au hata rafiki wa kiume au hata wa kike kwamba, "Nimependeza?" naye akakwambia hujapendeza bali unaonekana kituko, je kuna ubaya kusikiliza/kufuata ushauri wa huyo uliyemuuliza bila kujali kwamba wanawake hawajipendezeshi kwa ajili ya Wanaume?


 
Kuna watu washajijua bila hayo mazaga zaga hawatazamiki! Lol.
 
Wanawake hawajirembi kwa ajili ya wanaume bali kutiana wivu wenyewe kwa wenyewe.
 
Mi napenda rangi ya chini ya jicho lakin iwe light hiv na pia demu awe na nywele ndogo aweke wave napenda sana halafu apige mapooodaaa kwa mbali yani hapo akija napiga hata tano

na hiyo avatar yako haha hahaaaaa.. utafikiri ndo ulitoka kupiga hzo 5 na ukaanza kusinzia hapo hapo l.o.l
 
Kuna watu washajijua bila hayo mazaga zaga hawatazamiki! Lol.


Haha ha haa.. Wameshazoeleka kwa muonekano wa hayo makitu... hivyo hawana confidence ya kutoka bila kuyapaka l.o.l.

BTW.... make up nyingine zinachosha ngozi zikipakwa sana mfano kama hayo Mafoundation n.k. lakiini binafsi huwa nafikiri wakati mwingine bora ma make up kuliko ma CAROLIGHT duh!
 
Hongera kwa hilo.
Ila sidhani kama wanawatia vichefuchefu. . . maana ingekua kweli mngekua mnatapika kutwa mara kumi!![/QUOTE

Kuna vichefuchefu vya aina nyingi, kwani kuna vile visivyotibua mfumo wa tumobni kufanya kilichoingia kurudie njia hiyo hiyo kilitotokea badala ya kutokea njia nyingine ya mfumo wa kawaida. Mbaya zaidi ile inayotia kakasi na kuururumumisha tumbo hata makalio yakawa na kazi ya ziada kusaidia cramps kutokana na kuzidiwa uchafuzi wa hali ya hewa.
 
Hongera kwa hilo.
Ila sidhani kama wanawatia vichefuchefu. . . maana ingekua kweli mngekua mnatapika kutwa mara kumi!!

Aveta yako inaonyesha kujali mwonekano wa natural, hivyo utetezi wako ni wa kuwatetea wanafanya hivyo wakati we uko kinyume cha wanaojirembusha.
 
Back
Top Bottom